Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

Cha Kuzingatia Kabla ya Tendo Lenyewe

Uumbaji wa Mungu ni wa ajabu sana hasa linapokuja suala la mahusiano Kati ya mwanamke na mwanaume katika Mapenzi.
Ili kuridhishana kimwili kati ya mwanamke na mwanaume jambo la msingi ni kufahamu vizuri hatua kamili ambazo ili tendo la ndoa likamilike lazima zifuatwe na hasara zake.
    


Hata hivyo wakati mwingine wapenzi au Wanandoa hujikuta katika mgogoro katika eneo lingine la penzi na matokeo yake masuala ya kitandani pia huwa ovyo na zaidi kuanza kulalamikiana kila mmoja akimlaumu mwenzake.


Kawaida tendo la ndoa hupitia hatua tatu muhimu ambazo ni vizuri kila mwanandoa kufahamu na pia ni muhimu kufahamu kwamba kila hatua huwa na vikwazo vyake na hili lisipozingatiwa unaweza kujisikia wewe tu ndiye unayepunjwa kwenye ndoa au mapenzi.

Hizi hatua tatu muhimu kila moja ina uwezo wake na mzunguko wake binafsi na pia vikwazo vyake.
Hatua ya kwanza ni:-

HAMU YA TENDO LA NDOA.

ili kupata hamu ya tendo la ndoa lazima ubongo uhusike kwani kwenye ubongo kuna mfumo maalumu wa fahamu ambao kutokana na hali iliyopo mtu hujisikia hamu.

Hatua ya pili ni :-

KUSISIMKA.

hii ni hatua ambayo baada ya kuwa na hamu damu huweza kusambaa sehemu muhimu kama vile maziwa, K au Mashine ya mwanaume kwa ajili ya kuhakikisha Tendo linafanyika.

Hatua ya mwisho ni:-

KUFIKA KILELENI.

hii hutokana na kukaza kwa misuli ya K au Mashine ya Mwanaume na kutoa raha isiyoelezeka na baada ya hapo ni kama mwisho wa furaha ya tendo lenyewe.

NINI VIKWAZO VYA HATUA HIZI MUHIMU?

Wasiwasi, hofu, mashaka, woga, kuogopa na uadui hupelekea mtu kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Vitu hivyo kuhusu Tendo hupelekea kukosa kusisimka na kuwa tayari kwa mapenzi pia kufikiria sana kwenye ujuzi na na kuwaza sana staili ya Mapenzi wakati mpo kwenye Mchezo hii pia huondoa kufurahia tendo lenyewe na hupelekea kushindwa kufika kileleni.

Kumbuka utendaji wa Tendo katika ndoa huonesha hali ya ndoa nzima katika mambo yote kwani mara nyingi ndoa ikiwa na mgogoro hata tendo la ndoa huwa ni bora liende, si kuridhishana bali wajibu na ukweli unabaki kwamba Tendo katika ndoa huelezea ndoa ipoje.

Kama kuna mgogoro ambao haujapata jibu au kutokuelewana katika ndoa/Mapenzi basi mfumo mzima wa Tendo hubadilika.

Je, unajisikia raha na hamu kubwa na kusisimka kwa ajabu kama zile siku za kwamba wakati mnaoana au mlipoanza penzi lenu?
Je, jinsi unavyoridhika na tendo la ndoa ni sawa na ulivyokuwa unategemea? Au ni kama wajibu na si kupeana raha?
Ukweli unao mwenyewe.

Uzoefu unaonesha jinsi wanandoa / wapenzi wanavyozidi kuishi pamoja; tendo la ndoa huwa zuri zaidi na la kuridhisha zaidi kuliko mwanzo au miaka ya mwanzo.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4