Sunday, 16 March

Ads Right Header

Buy template blogger

Kuwahi Kumaliza Shughuli Haraka (Sehemu ya 2)

Kawaida baada ya mwanaume kuwa na tabia ya kumaliza haraka kinachofuata ni kuanza kukwepa Tendo la Ndoa kitu ambacho inakuwa ngumu zaidi kudhibiti tatizo, mwanaume akiwa anauwezo wa kudhibiti kumaliza mapema pia huweza kuwa na hamu zaidi ya kufanya mapenzi.


  


Wengine hutumia njia ya kuondoa mawazo kujihusisha na tendo lenyewe kwa kuwaza vitu vingine hata hivyo hapo ni kujinyima raha na huweza kupelekea vitu kuwa ovyo zaidi.
Si vema kuhamisha mawazo yako kutoka kwenye akili zako wakati wa tendo la ndoa kwani ni Tendo la muunganiko wa roho, mwili na nafsi.
Jambo la msingi ni kuwa na ufahamu wa viwango tofauti vya msisimko wa kimapenzi kuhusiana na kiungo chako (Mashine).
Unatakiwa kujua ni namna gani unajisikia unapokaribia kufikia hatua ambayo hakuna kurudi nyuma.

Ukishakuwa umefahamu unavyojisikia kuelekea point of No return hapo haitakuwa vigumu kufanya marekebisho ambayo yatakuruhusu kubaki umesisimka lakini bila kumaliza (kukojoa).

Kusisimka kimapenzi huwa ni mzunguka wa hatua 4 muhimu ambazo ni:-

KUPANDA KWA MDADI.
Huu ni wakati ambao kupumua huongezeka, Mashine husimama (hudinda). hatua ya pili ni:-

KILIMANI- hii ni hatua ambayo Mashine huwa imebaki imesisimka kwa kiwango cha juu.
Hatua inayofuata ni hatua ya tatu ambayo ni:-

KUMALIZA au KUKOJOA na hatua ya mwisho ambayo kupumua hurudi kama kawaida na Mashine hurudi na kuwa kawaida.
Ufunguo muhimu katika kudhibiti kumaliza mapema ni kuimudu hatua ya pili yaani kubaki hapo kilimani bila kupiga risasi hata kama umelenga vizuri na unajisikia kuachia, hapa ndipo panahitaji imani na kujikana maana huwa ni kuelekea kwenye raha kamili ya Tendo kwa mwanaume, ila kumbuka uliye naye anahitaji uendelee zaidi.


NINI KIFANYIKE KUDHIBITI HALI HII?
Usitumie Madawa au kilevi eti ndo unaweza kudhibiti hii hali, vitu kama hivi huweza kukupa muingiliano na kupunguza uwezo wa kuelewa wakati muhimu wa wewe kuthibiti kumaliza mapema.
Kwanza jikubali, wanaume wengi huamini kwamba sex ni kwenye uume tu na pia kufanya mapenzi ni pale Mashine ukiingia kwenye uke tu.
Kufikiria hivyo ni tiketi ya moja kwa moja ya mwanaume kuwahi kukojoa au kumaliza.

Kufanya mapenzi kunakoridhisha ni pamoja na kupeana mahaba kuanzia juu kichwani kwenye nywele hadi kwenye kucha za vidole miguuni.



Mwanaume anayejifunza kujipa raha kimapenzi kupitia sehemu zote zinazompa raha (chuchuu, lips, shingo, midomo, ulimi, nk) huweza kujiweka tayari kupitia hizo sehemu na kutosubiri sehemu moja tu yaani Mashine ndo iwe sehemu ya kupata raha ndo maana huweza kukojoa mapema.



Ni kwamba mwanaume anakuwa amefunga sehemu zingine na kubaki na Mashine tu hivyo ni rahisi kufikia point ya hamna kurudia tena (Point no Return) kwa haraka mno.
Ukishajifunza kupata raha ya mapenzi kuanzia nywele kichwani hadi kucha miguuni maana yake mwili mzima unachukua raha ya mapenzi badala ya Mashine peke yake na matokeo yake utabaki ndani ya mke wako kwa muda mrefu.



Kujipa raha ya mapenzi ya mwili mzima ni njia ya ku-relax na kurelax ni moja ya njia muhimu za kujipa Tendo Tamu.
Kwa mfano kuoga pamoja kwanza au kufanyiana massage kwanza kabla ya kuanza kwa tendo la ndoa husaidia mwanaume kurelax na zaidi kuupa mwili mzima Hisia nzito ya Mapenzi matokeo yake ni kufanya mapenzi kwa muda unaotosha na bibie kuridhika.



Kuwa na uwezo wa kupumua vizuri (deep breath) hii haina maana kwamba wakati unafanya mapenzi huwa hupumui, la hasha bali upumuaji wako inawezekana si ule usiotakiwa kwani wanaume wengi huzuia kupumua wakiwa kwenye Tendo.


Wengine huogopa kusikika wanapumua tofauti, Tendo la Ndoa ni kazi kama kazi zingine sasa usipopumua unadhani kitatokea nini, ikiwezekana pumua huku unatoa visauti, achia kupumua usijivunge kwani unapoficha kupumua maana yake unakaribisha uume ukusaidie kupumua na njia sahihi kwa uume kupumua ni kukojoa mapema.
Wengi baada ya kujifunza kupumua kwa kujiachia wamefanya mabadiliko makubwa sana katika muda wa kuwa ndani bila kumimina risasi.
· .
Ukishajua kuutumia mwili mzima kuhusika na raha ya mapenzi pamoja na kupumua sasa inakuja technic nyingine ya kujipiga stop.
Unaweza kuwasiliana na mpenzi wako jinsi ya kupeana alama kwamba nakaribia kile kituo ambacho nikifika sitarudi tena, hakuna break.



Unaweza kutoa Mashine nje huku ukiendelea kupumua na ukiona unapata zile hisia kwamba huwezi kukojoa basi unaweza kurudi na kuendelea tena, kiasi cha kujipiga stop na kuendelea ni uamuzi wa ninyi wawili mnaohusika hasa baada ya mke kuridhika.


Pia aina ya milalo wakati wa mapenzi huchangia mwanaume kumaliza mapema, Mfano (mwanaume juu mwanamke chini) huu huwezesha mwanaume kumaliza haraka kuliko mwanamke kuwa juu na mwanaume chini, vinginevyo mwanaume ni vizuri ukafanya utafiti wako kujua ni mlalo gani huwa unajisikia kuchelewa kumaliza na mke wako kuwahi kufika kileleni.

Pia ni vizuri kufanya mapenzi bila kuwa mabubu,kufanya mapenzi huku mnaongea husaidia mwanaume kurelax (na mwanamke pia) na husaidia mwanaume kuchukua muda mrefu kumaliza
Kujifunza kuthibiti kumaliza mapema kunaweza kuchukua muda mrefu na mazoezi ya kutosha, unaweza kujisikia kusumbuka tu wakati unajitahidi kuthibiti hata hivyo kwenye nia njia ipo na wewe utaweza tu nakuamini.

Mwisho, kujifunza mwanaume kumaliza mapema kutampa mpenzi wako raha kubwa sana kimapenzi. Wanawake hupenda Tendo Tamu ambalo ni starehe, tamu, mwili wote, massage kwa wingi.



Na wanawake wengi hulalamika kwamba wanaume huwa na haraka tukiwa kwenye miili yao, tupo too much mechanical, tunakimbilia kule chini tuingize tumalize na tuishie zetu kwa usingizi, tuna focus maziwa na maeneo ya K tu.
Wanawake hujisikia mwili mzima ni uwanja wa kucheza kimapenzi na hushangazwa na wanaume kugundua visehemu kidogo tu katika uwanja mzima na kuvipenda.
Hata Mashine pia imeumbwa kwa ajili ya Starehe, kuchezewa, mapenzi ya mwili mzima, massage ya mwili mazima ndipo Tendo lenyew, kuwa focused (Kuweka Mawazo ) kwenye Mashine peke yake huweza kuipa mashine mgandamizo ambao hupelekea kutoa risasi mapema.

Kimsingi kama wanaume wangekuwa wanafanya mapenzi kwa namna ambayo wanawake wanapenda basi kusingekuwa na malalamiko na wanaume wangekuwa na matatizo kidogo yanayohusiana na tendo la ndoa.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4