Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SIMULIZI MPYA: TANGA RAHA 03 & 04 (Return Of Olivia Hitler)




TANGA RAHA 03
(Return Of Olivia Hitler)
Muandishi………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(Genius Author)
Simu………………………………………………….0657072588(Whatsapp)au 0768516188
Website……………………………………………… 
ILIPOISHIA
“Mbona unalia?”
Olvia Hitler alizungumza huku akiwa amesimama nyuma ya Xaviena aliye simama pembezoni mwa jukwaa, huku akitazama mlango wa kuinguilia ndani ya ukumbi huu kupitia uwazi mdogo wa pazia lilizo ziba upande wote wa nyuma ya jukwaa.
“Familia yangu hadi sasa hivi haijafika?”
Xaviena alizungumza kwa sauti iliyo jaa majonzi kana kwamba ni mtu aliye fiwa
“Ohhh usilie my dear, watakuja tu, ninaimani watakuwa wapo njiani”
“Tangu saa mbili, kwani kuna umbali gani kutoka Sahare hadi hapa Raskazoni jamanii?”
“Sawa usijali watakuja, kwani hata mimi pia nipo, hakuna kitakacho haribika, wewe kuwa na amani”
Olvia Hitler akamkumbatia Xaviena.

ENDELEA
“Ohhh baby nyamaza kulia eheee”
Olvia alizungumza huku akiishika shika shingo ya Xaviena, taratibu kisha akamapulizia pumzi ya baridi, iliyo usisimua mwili wa Xaviena na kujikuta akirudi katika hali yake ya kawaida, huku mawazo juu ya familia yake yakipote gafla kichwani mwake.
“Nenda kashindane mwanangu, waonyeshe kwamba wewe ni mkali kupita wao wote”
Olvia Hitler alizungumza huku akimuachia Xaviena kutoka mikononi mwake, alipokua amemkumbatia
“Sawa Madam”
“No usiniite Madam, wewe niite Aunt Olvia”
“Sawa Aunt Olvia”
Xaviena alizungumza na kwa furaha na kuelekea walipo washiriki wazake ambao, wanajiandaa kwa pamoja kutoka mbele ya watazamaji, kwa ajili ya kutambulishwa kama desturi ya mashindano hayo. Karibia washiriki wote walitoa kitu kidogo kwa majaji pamoja na waendeshaji wa shindano hilo ili kila mmoja akiamini atapata chochote katika mashindano hayo, zikiwemo hatua kuu tatu ambazo ni mshindi wa kwanza, wapili na watatu, ambao kidogo zawadi zao ni tofauti na washiriki wengine wa nafasi za chini, kuanzia nne hadi wa mwisho. Ila ipo tofauti sana kwa Xaviena ambaye hakutoa kitu cha aina yoyote na siku zote majaji wawili wakiume, walikuwa wakimsumbua wakihitaji kupata rushwa ya ngono au pesa kidogo ili wamfanye mshindi, jibu la Xaviena, la kukataa, lilizua chuki kati yake na majaji wote wanne ambao wawili ni wanawake, na wawili ni wanaume.
Kauli mbiu ya majaji hao, ni kuhakikisha Xaviena hapati hata nafasi ya tano bora, japo wakuu washindano hilo hawatambua ni kitu gani kinacho endelea kwa majaji hao wanne. Wakuu hao wa mashindano mategemeo yao yote kumuona Xaviena Eddy kuwa mshindi wa taji hilo kutokana na vigezo walivyo viangalia kwamba Xaviena anaweza kuiwakilisha Tanzania katika mashindano makubwa ya dunia.
Mkuu wa mkoa ni mgeni rasmi, amealikwa kuja kushudhuria shindano hilo na yeye ndiye atakaye mtangaza mshindi wataji hilo.
***
Gari ndogo aina ya Ferrali yenye rangi nyekundu, ikaanza kupiga honi zenye fujo, huku ikiwa nyuma ya gari analo endesha Eddy, akiwa amempakiza mke wake Rahma, pamoja na mtoto wake Xaviela
“Huyu naye ni nani na mikelele yake?”
Eddy alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake, na kuwafanya Xaviela na mama yake kutazama nyuma kwani, gari hiyo ndogo na yakifahari ilizidi kuwapigia honi nyingi, huku dereva wa gari hilo akiziwasha taa za gari hilo zote kwa pamoja(full light)
“Baba Xaviela si umpishe tu apite”
“Ngoja nimuonyeshe kwamba mimi pia ni kichaa, kwenye undeshaji wa wa gari”
“Jamani mume wangu tambua kwamba…..”
“Tulia mke wangu”
Eddy akazidi kukanyaga mafuta ya gari lake na kulifanya, gari lake lizidi kwenda kasi, ila dereva wa gari ya Ferrari akalazimisha hivyo hivyo kulipita gari la Eddy, na kwenda nalo sambamba katikati ya barabara. Eddy akaanza kupiga honi akimushiria dereva huyo kupita na atangulie mbele yake, kwani endapo kutatokea gari jengine mbele ni lazima dereva wa gari ndogo atapata ajali mbaya itakayo sababisha mambo mengine ambayo hawayatarajii kuyaona kwa wakatio huo.
“Wewe mpumbavu hembu pita”
Eddy alizungumza huku, akiwa amefungua kioo cha upande wake, huku Xaviela na mama yake wakiwa wameketi siti ya nyuma wakitazama mashindano hayo.
Dereva wa gari ilo akashusha kioo taratibu na macho ya Eddy, yakakutana na macho ya Olvia Hitler anaye endesha gari hiyo ndogo ya kifahari jambo lililo mfanya Eddy kushikwa na butwaa, na kujisahau kwamba yupo barabarani na gari lake lipo katika mwendo kasi. Olvia Hitler akafunga kioo chake, huku akitabasamu na kuachia busu la mbali na kumalizia kukifunga kioo chake cha gari lake, akaongeza mwendo wa gari lake na kukata kona kali iliuyo mbele yao, na kuliacha gari la Eddy likienda kuvamia miti midogo midogo iliyopo pembezoni mwa barabara na kwenda kugonga kwenye mti mkubwa aina ya mvule, na kusimama hapo hapo huku likiharibika vibaya kwa mbele
Ukimya ukatawala ndani ya gari huku mapigo ya moyo yakianza kumuenda mbio Eddy aliye pigwa na bumbuazi la muda huku airbag kubwa lililo toka kwenye mskani wa gari hili ukimfunika usoni mwake. Rahma akaanza kukohoa kutokana na mstuko alio upata, taratibu akaufungua mkanda wa siti aliyo ikalia na kushuka huku akihema sana, akaka kwenye nyasi za pembezoni mwa gari hilo. Xaviela naye akajikongoja kongoja na kutoka ndani ya gari huku akiweweseka kwa kizunguzungu kikali. Rahma alipo jichunguza vya kutosha, akanyanyuka kiuvivu uvivu kutoka katika sehemu aliyo keti na moja kwa moja akeelekea lilipo gari, ambapo hadi sasa hivi mumewe hajatoka ndani ya gari.
“Eddy, Eddy”
Rahma aliita huku akiufungua mlango wa gari, kwenye upende wa dereva alipo kaa mumewe. Kwa kutumia mkono wake wa kushoto akamtingisha Eddy begeni kuweza kumtoa kwenye hali ya bumbuwazi.
“Ehee, eheheeee”
Eddy aliweweseka huku akijifungua kwa garaka mkanda wa siti na kutoka ndani ya gari.
“Kaa chini kidogo mume wangu”
Rahma akawahi kumshika mkono Eddy anaye onekana kuchanganyukiwa na kwa kile alicho kiona. Rahma akafanikiwa kumtuliza mumewe, akamchunguza kila sehemu ya mwili kumtazama kama kuna sehemu ameumia ila hakukuwa na jeraha lolote kwenye mwili wa Eddy ambaye hadi sasa hivi mawazo yake yote kwa Olivia Hitler
“Mumeumia?”
Eddy aliwauliza Rahma na mwanae Xaviela huku akijikung’uta kung’uta majani kwenye suruali yake, baada ya kukaa chini kwa muda ili mwili wake kuwa sawa.
“Mimi nipo poa”
Xaviela alijubu huku akimtazama baba yake machoni
“Mimi pia sijaumia, sijui wewe?”
“Mimi nipo salama”
Eddy alizungumza huku akilisogelea gari lake kulichunguza kama kuna hitilafu yoyote iliyo weza kutokea. Hakuamini kuona gari lake la kifahari likiwa limeharibika vibata mno kwa mbele.
“Ohoo itakuwaje sasa?”
Eddy aliuliza swali ambalo hapakuwa na aliye lijibu kwa haraka kila mmoja akawa anatafakari kujua ni kitu gani wanapaswa kuweza kukifanya kwa muda huo. Xaviela akatoa simu yake kwenye kipochi chake kidogo na kuanza kuminya minya baadhi ya namba, kisha akaiweka simu yake sikioni kusikilizia.
‘Namba unayo ipiga kwa sasa inatumika, tafatha…….’
Xaviela akakata simu huku akiachia msunyo mkali, ulio wafanya wazazi wake kumtazama.
“Vipi?”
Eddy alimuuliza huku akimtama Xaviela
“Kuna fundi nilikua ninampigia, jisimu lake nalo linatumika”
“Hembu jaribu kumpigia tena tuone”
Rahma alizungumza huku akiwa katika sura ya masikitiko, Xaviela akaipiga tena namba ya simu, ila safari hii akaachia msunyo mkubwa zaidi.
“Halipatikani, mijitu mingine kama imerogwa vile”
“Basi tufunge vioo vya gari, tuliache hapa tutakuja kulifwata asubuhi”
“Baba Xaviela na wewe mawazo yako muda mwengine ni yaajabu sana. Hivi kuacha gari la kifahari kama hili hapa porini, hivi huoni kama ni hatari. Kesho ukija hapa asubuhi taa zote utakuta zimeng’olewa”
“Sasa hapa tutafanyaje mke wangu?”
“Cha kufanya, jaribu kama linawaka kisha tuendelee na safari, hapa ninahisi kwamba huko Xaviena atakuwa analia kwa kuto kutuona kwa wakati”
Eddy akafwatisha ushauri wa mke wake, akaingia ndani ya gari na kujaribu kuliwasha gari likawaka, akajaribu kulirudisha nyuma likarudi pasipo kua na shida yoyote. Akaliweka gari sawa, Rahma na mwanae wakaingia ndani ya gari, taratibu wakaianza safari kuelekea Mkonge Hotel kunapo fanyika mashindano hayo ya ulimbwende, huku mtoto wao Xaviena akiwa ni miongoni mwa washiriki wa shindano hilo.
***
Olivia Hitle, baada ya kuachana na Xaviena, akatafuta sehemu yenye kiti chake, kilichopo kwenye eneo la viti vya watu wenye hadhi ya hali ya juu walio lipia kiwango kikubwa cha pesa katika kukaa katika eneo hilo ali maarufu V.I.P. Sehemu aliyo keti ilimuwezesha kuweza kuona jukwaa zima, hamu yake kubwa ni kumshuhudia rafiki yake kipenzi akifanya mambo makubwa yatakayo washangaza majaji walio panga kumuangusha binti huyo aliye shindwa kutoa hongo ya aina yoyote, ikiwemo pesa au penzi kwa majaji wa kiume
“Mabibi na mabwana karibuni katika shindano la kumsaka miss Tanga ambaye ataiwakilisha Tanga kwenye mashindano makubwa ya miss Tanzania”
Sauti laini ya mtangazaji wakike, aitwae Judith, ilipenya kwenye masikio ya watu wote walio kuwemo ndani ya ukumbi wakitamani kuweza kushuhudia mashindano hayo ya kukata kwa shoka.
“Mc wenu leo nina itwa Judith Fredy na nipo na Laurence Mgaya”
“Matangazo yetu yanaruka moja kwa moja kwenye tovuti yetu yawww.storyzaeddytz.com. Pia munaweza kutazama matangazo haya kwenye chanel yetu ya Youtube inayo itwa Story Za Eddy-tz na pia tupo mubashara kupitia page yatu ya Facebook, @StoryZaEddy-tz.”
Mtangazaji Laurence Mgaya mwenye sauti nzito kiasi yakuvutia alizungumza, huku akiachia tabasamu pana usoni mwake.
“Unacho takiwa ni kuingia kwenye simu yako ya smart phone, laptop, desktop au tablate, andika www.storyzaeddytz.com broweser yako, nawe utafwata maelekezo ya kuweza kutazama mashindano haya kwa mwenzi huu ni free, kwa new subscribers. Usichelewe kuipata ofa hii, popote pale ulipo ndani na nje ya Tanzani basi hakikisha una tufwatilia moja kwa moja”
Watu walio kuwemo ndani ya ukumbi hawakusita kuwapigia makofi watangazaji hao walio valia mavazi ya kuvutia machoni wa watu, huku wakijua kuzitumia sauti zao katika kuwaburudisha walio hudhuri.
Kipengele cha kwanza kikaanza kwa warembo kuweza kutambulishwa mbele ya waalikwa. Kila mmoja aliweza kutoka akiwa amevalia gauni lake refu alilo andaliwa na mwanamitindo wake. Kitendo cha Xaviena kutoka kwenye pazia kubwa lililopo jukwaani, ukumbi mzima ukafurika kwa shangwe hadi majaji walio muwekea kinyongo wakajikuta wakishangazwa huku mmoja wao akijikuta naye akipiga makofi ya chini chini.
“Wewe vipi, makofi yako ya nini?”
Jaji mmoja alimuuliza mwenzake kwa sauti ya chini, huku akihisi mwenzao huyo ameanza kuwabadilika
“Wewe mtoto wa watu kapendeza, kwanza cheki anavyo tembea, hao walio tangulia wametembea kama mijizigo ya kuni”
Jaji huyo alijikuta akizungumza kwa furaha kubwa, bila hata ya kujishauri mara mbili mbili, akaandika asilimia mia moja kwenye jina la Xaviena Eddy, kwenye kipengele cha kwanza. Ujasiri ukazidi kumjaa Xaviena kila alipo yapeleka macho yake kwa Olivia Hitler, ambaye kila alipo tazamana naye aliachia tabasamu pana na busu kubwa mdomoni mwake. Tabasamu la Xaviena likazidi kuwakosha wahudhuriaji wote, wakazidi kupiga ndelemo na vifijo.
Jambo hilo likaanza kumkwaza Asha, yeye na timu yake hadi wakajikuta wakianza kukunja sura zao, jambo lililo wafedhehesha majaji walio wahonga pesa na kujikuta wakiandikiwa maksi chache ambazo ni ishirini, huku kiongozi wao Asha, akiandikiwa maksi ishirini na tano.
Taratibu wakaanza kurudi nyuma ya jukwaa kwa mstari kama walivyo ingia ndani ya jukwaa, Xaviena yeye niwa mwisho kabisa, jambo lililo wafanya watu wengi kuweza kumfaifaidi kwa nyuma maungo yake jinsi anavyo tembea kwa madaha, na kuzidi kuzikonga nyoyo zao.
“Huyu mtoto hata sijui nimuandikie maski ngapi?”
Jaji mmoja wa kike aliuliza huku peni yake ikiwa mkononi
“Wewe weka mia bwana, hao mambulula wetu walio tupa pesa wamesha tudhalililisha. Mwanzo ni hivi huku mbeleni itakuaje, si ndio utakua mwanzo wakupigwa mawe”
Jaji aliye anza kumkubali Xaviena alijikuta akiwashauri wezake walio onekana kukosa maamuzi sahihi ya kufanya.
Kila mmoja akaijikuta akiweka maksi kuanzia tisini kwenda juu, huku wakionekana kujisikia vibaya kwa kulifanya hilo. Ila siri kubwa ya shangwe na nderemo hizo, anaijua Olvia Hitler, aliye endelea kuhasikisha kwamba Xaviena Eddy anashikilia nafasi ya kwanza, ili aweze kumtumia vizuri kwenye mpango wake alio upanga tena hapa duniani, dhidi ya Eddy na mkewe Rahma.
“Mabibi na mabwana kipengele kinacho fwata sasa hivi……..”
Mtangazaji wa kike alizungumza na kumuacha mwenzake wa kiume amalizie sentensi hiyo
“Warembo wetu kucheza ngoma za asili kwa pamoja, ambapo majaji wetu wataendelea kutuchagulia ni nani ambaye ni hodari katika hilo”
“Tumawakumbusha muedelee kutembelea www.storyzaeddytz.com ujipatie matangazo haya mubashara mwezi huu ni bure kabisa.”
“Pia tusiwasahau wazamini wetu wa onyesho hili E and F Production, watengenezaji mahiri wa filamu duniani. Bitreace hivi una habari?”
“Nijuze Laurence wangu”
“E and P Production, watampa mkataba mono mshindi wetu na kufanya naye kazi moja kubwa Tanzania haijawahi tokea, kwani master karibia nane kutoka Hoolly wood Marekani, watatua bongo kufanya kazi kati ya hao mmoja wao ni CALVIN HEART, sasa washindani kazi ni kwenu, kwani ukishinda hapa basi dunia itakufahamu”
“Waoooo it’s so amaizing, am wait for that bigest movie”(Waoooo inashangazaa, ninaisubiria hilo bonge la filamu)
Tangazo la washereheshaji, likawafumbua masikio washindani wote walio kua wakiendelea kubadilisha nguo zao haraka haraka na kuvaa baadhi ya nguo za asili, wakisubiria kwenda kucheza ngoma.
***
Eddy akajitahidi kuliendesha gari lake aina ya Range rover sport, hivyo hivyo japo lilitoa mlio wa mkwaruzo fulani, ila hakujali. Wakafika Mkonge Hotel, akaliegesha gari lake sehemu ya maegesho, wote wakashuka na kuanza kuingia ndani kwa mwendo wa haraka kwenda kuwahi kukaa kwenye viti vyao ambavyo tayari walisha vikatia tiketi siku nyingi za nyuma.
Rahma akajikuta akiachia tabasamu pana, baada ya kumuona mwanae Xaviena akiingia jukwaani akiwa na kiguo chenye nyasi nyasi, na kuanza kucheza, huku ukumbi ukitawaliwa na kelele za nyingi za shange
“Mama twende tukakae bwana”
Xaviela alimstua mama yake na wote wakaelekea sehemu alipo kwenda Eddy. Kutokana watu walikua wamesimama kwa shangwe nao, wakajikuta wakisimama pembezoni mwa viti vyao wakishangilia kwa furha kubwa. Xaviena akazidi kukicheza kiuono chake jambo lililo wafanya mapaparazi kila mmoja kuielekezea kamera yake kwa Xaviena na kuwaacha wengine walio kua wakionekana si lolote wala si chochote mbele ya Xavienea
“Karibuni mukae”
Eddy akawa wa kwanza kumtazama mwanamke anaye mkaribisha wakae kwenye viti vyoa, hakuamini kumuona Olvia Hitler akiwa ndio mwenzao, katika meza hiyo nyenye viti vinne, jambo lililo ikatisha furaha yote ya Eddy.

TANGA RAHA 04

Xaviena akazidi kukicheza kiuono chake jambo lililo wafanya mapaparazi kila mmoja kuielekezea kamera yake kwa Xaviena na kuwaacha wengine walio kua wakionekana si lolote wala si chochote mbele ya Xavienea
“Karibuni mukae”
Eddy akawa wa kwanza kumtazama mwanamke anaye mkaribisha wakae kwenye viti vyoa, hakuamini kumuona Olvia Hitler akiwa ndio mwenzao, katika meza hiyo nyenye viti vinne, jambo lililo ikatisha furaha yote ya Eddy.

ENDELEA
Olvia Hitler akaachia tabasamu lililo mtatiza sana Eddy. Kwenye maisha yake hakutarajia kukutana na Olvia. Ajali waliyo ipata muda mchache ulio pita, chanzo ni Olvia Hitler. Taratibu Rahma akageuza uso wake na kumtazama mwanadada huyo. Rahma mdomo ukambaki wazi, kwa wasiwasi ulio mtawala akajikuta akikaa kwenye kiti huku akiendelea kumtazama Olvia.
“Shikamoo”
Xaviela alimsalimia Olvia na pasipo kujua ni kitu gani kinacho endelea kati ya wazazi wake na mwana dada huyo.
“Marahaba, yule ni pacha wako?”
“Ndio ni pacha mwezangu”
“Mumefanana kwa kweli. Naamini wazazi wako wanafurahia kwa kuwapata nyinyi”
“Nashukuru sana”
Xaviela alizungumza huku naye akikaa. Baada ya shangwe za mashabiki kuisha, taratibu watu wote wakaka kwenye viti vyao. Ukimya kwenye meza hii aliyo kaa Eddy pamoja na Olvia Hitler, ukatawala.
“Wewe kwa nini hukushiriki mashindano haya kama mwenzako?”
Swali la Olvia Hitler, likamfanya Eddy na Shamsa kumtazama Olvia ambaye wana mfahamu vizuri.
“Ahaa mimi sipendelei sana maswala hayo ya urembo.”
“Wewe una pendelea nini?”
“Napendelea sana maswala ya ngumi ngumi na ikiwezekana huko baadaye nije kuwa jasusi hatari wa kike”
“Xaviela”
Shamsa aliita huku akimtazama Xaviela kwa macho makali, ikiwa ni ishara ya kumfanya asiendelee kuropoka ropoka.
“Ila kazi ya ujasusi ni ngumu sana?”
“Yaa ndio naipendelea sana”
Xaviela wala hakujali onyo alilo pewa na mama yake.
“Inabidi wazazi wako wakufanyie mpango wa kuingia kwenye vitengo ambavyo vitakufanya uwe jasusi mzuri”
“Naamini wana sikia. Eti baba utanitafutia ehee?”
“Ndio mwanangu”
Eddy alijibu kwa unyonge huku akimtazama Olvia kwa macho makali sana, yaliyo jaa hasira na uchungu ndani yake.
“Unaitwa Xaviela ehee?”
“Ndio naitwa Xaviela na pacha wangu anaitwa Xaviena”
“Ahaa….sawa sawa. Jitahidi kukamilisha ndoto zako”
“Nitafanya hivyo. Wewe una itwa nani?”
“Olvia, Olivia Hitler”
“Waoo jina ni zuri.”
“Nashukuru sana Xaviela, hata nyinyi majina yenu ni mazuri sana. Wazazi wenu hawajakosea kuwaita hivyo”
“Olvia tafadhali una weza kumuacha mwanangu?”
Eddy alizungumza kwa sauti ya ukali na ya chini chini ambayo wao wanne tu ndio waliweza kuisikia. Jambo hilo likamshangaza sana Xaviela.
“Kuna tatizo mimi kuzungumza na mwanao?”
“Sihitaji uzungumze na wanangu na laiti kama ningefahamu nina kaa na wewe kwenye hii meza wala nisinge thubutu kukalisha makalio yangu hapa”
“Hahaa Eddy. Umekuwa sasa hembu acha hayo mambo yako”
Taratibu Shamsa akapitisha mkono wake chini na kumshika Eddy anaye tetemeka mikono yake kwa hasira kali sana.
“Baba ni nini kinacho endelea?”
“Xaviela tulia”
“Siwezi kutulia mama. Inakuwaje baba ana mfokee dada wa watu?”
Jicho alilo tazamwa Xaviela na baba yake, likamfanya akae kimya huku akitambua kwamba baba yake hayupo sawa.
“Jamani hii ni siku nzuri sana kwenu. Mtoto wenu anakwenda kuchukua taji la miss Tanga. Basi tofauti zetu tuziweke pembeni na tumuunge mkono”
Olvia Hitler alizungumza huku akitabasamu, tabasamu la kinafki lililo mfanya Eddy kushusha pumzi na kuliweka vizuri koti la suti yake. Mashindano yakazidi kupamba moto huku washikiri wakizidi kuchuana vikali. Olvia akanyanyuka kwenye kiti chake na kuanza kutembea kuelekea chooni.
“Nina kuja”
Eddy alizungumza huku naye akinyanyuka kwenye kiti chake.
“Baba Xaviela uwe makini”
“Usijali”
“Mama baba ana kwenda wapi?”
“Chooni”
“Mbona anakwenda mara baada ya Olvia kunyanyuka. Hembu mama niambieni ni nini kinacho endelea?”
“Ni historia ndefu mwanangu. Ila tuendelee kutazama”
“Mama nitaendeleaje kutazama ikiwa wazazi wangu nyinyi hamupo sawa. Hembu kuweni wawazi basi mama”
“Xaviela hembu nipe basi nafasi ya kutafakari kichwani mwangu”
Rahma alizungumza huku akitazama jinsi Eddy anavyo tokomea kwenye eneo hilo la ukumbini. Eddy akamkuta Olvia Hitler akiwa amesimama nje ya vyoo vya kike huku akivuta sigarete.
“Kumbe Eddy bado huja kua kiakili?”
Olvia alizungumza huku akitoa fumba zito la moshi puani mwake.
“Umerudi kufanya nini kwenye maisha yangu?”
“Kwenye maisha yako. Nimekufwata kwako, au nimekuuliza chochote juu ya familia yako?”
“Olvia tafadhali kaa mbali sana na familia yangu. Sitaki siku hata moja uwasogelee wanangu. Nitakufanya kitu ambacho hujawahi kufanywa kwenye maisha yako”
“Mimi, wewe unifanye kitu ambacho sijafahi kufanywa? Eddy umenisahau mimi ni nani eheee?”
Olvia Hitler alizungumza huku macho yake yakibadilika badilia rangi ya mboni zake na kumfanya Eddy kuzidi kujawa na uwoga japo ana jikaza kishujaa.
“Potea mbele ya macho yangu kabla sijakusambaratisha.”
Olvia Hitler alizungumza kwa sauti yenye mitetemo kama ya radi. Eddy hakutamani kabisa akumbane na matatizo aliyo wahi kusababishiwa na Olvia Hitler. Akarudi ukumbini huku jasho likimwagika usoni mwake.
“Baba nini kimekupata?”
“Hakuna kitu?”
“Mmm!! Baba una nidanganya, tupo pembezoni mwa fukwe za habari. Inakuwaje una mwagikwa na jasho kiasi hicho ikiwa eneo hili lina upepo wa kutosha?”
“Xaviela una maswali mengi, hembu tusubiri matokeo ya dada yako”
“Mmmmm”
Olvia Hitler akarudi eneo hilo huku uso wake ukiwa umetawaliwa na tabasamu pana sana. Kitendo cha Xaviena kuwaona wazazi wake wakiwa wamekaa meza moja na Olvia, akazidi kujawa na ujasiri. Hatua wanayo kwenda hivi sasa ni ya mwisho kabisa katika mtanange huu. Hatua ya kuulizwa maswali ya hapo kwa hapo ina hofiwa na kila mshikri kwani unaweza ukawa ume kamilika kwenye kila idara ya urembo, ila eneo hilo likakupunguzia maksi.
‘Lazima nishinde, nimemla ng’ombe mzima kwa nini nishindwe kwenye mkia?’
Xaviena alizungumza huku akijiamini sana.
“Asha asha”
“Beee”
“Huu ndio wakati wa mwisho, utamuachia yule mpuuzi aweze kushinda kirahisi hivi?”
Khadija alizungumza huku akimnong’oneza Asha rafiki yake wa karibu na wote wapo kwenye kinyang’anyiro hichi cha urembo.
“Ile dawa aliyo isema mtaalamu ipo wapi?”
Asha aliuliza huku akimtazama Khadija usoni mwake. Siku kadhaa zilizo pita waliweza kumuita mganga wa kienyeji kambini kwao na akawakabidhi dawa ambayo endapo mmoja wao atafanikiwa kumshika nayo mkono mtu waliye kusudia kumshinda basi, mtu huyo ata hudhurika kwa kuto kuweza kuona tena.
“Ninayo hapa”
“Hembu naiomba”
Asha na Khadija wakasogea pembeni, eneo ambalo hakuna mtu ambaye ana weza kuwaona wakifanya uhalifu wao. Asha akajipaka dawa hiyo ya unga unga mkononi mwake. Kisha akamfwata Xaviena sehemu aliyo simama.
“Xaviena ninaweza kuzungumza na wewe japo kwa dakika hii moja”
Asha alizungumza kwa sauti ilio jaa upole na ustarabu mkubwa sana hadi Xaviena akabaki ameshangaa kwani siku zote Asha amekuwa ni mtu wa vitimbwi kwake.
“Zungumza”
“Unajua mimi ni binadamu. Kuna mambo mengi sana ambayo nimekufanyia, leo ni siku ya mwisho na hakika nisipo weza kukuomba msamaha nitakuwa nime kukosea”
Asha alizungumza kwa upole japo moyoni mwake hamaanishi hicho kinacho mtoka mdomoni mwake.
“Asha leo umekubwa na nini?”
“Kwa nini Xaviena?”
“Sijui kwa nini una niomba msahaha ikiwa ulikiri kwa kinywa chako kwamba una nichukia”
“Xaviena hembu tuachane na hayo yalyo pita. Nakuomba sana uweze kunisamehe mpenzi”
Xaviena akashusha pumzi huku akimtazama Asha.
“Sawa mimi sina shida na wewe. Natambua baadhi ya mambo ulikuwa una yafanya kutokana na wivu, ila siri moja kubwa katika maisha ambayo nakuomba uwe nayo popote utakapo kwenda. Hakikisha kwamba una jibidiisha sana. Hakuna mafanikio yanao kuja pasipo juhudi, wivu pasipo jitihada rafiki yangu hakuna kitu”
“Nashukuru sana Xaviena, hakika sijawahi kukuatana na mwanamke mwema na mkarimu kama wewe”
Asha alizungumza huku akimpa mkono Xaviena, aliye utazama kwa sekunde kadhaa huku akiwa na wasiwasi na mkono huo.
“Nisamehe rafiki yangu”
Asha aliendelea kumshahiwishi Xaviena huku akimpa mkono. Taratibu Xaviena akaupokea mkono huo na wakakumbatiana. Warembo wengine wakapiga makofi, taratibu wakaachiana na huku kila mmoja akiwa na tabasamu pana usoni mwake.
Kitu kilicho mshangaza Asha ni kuto kuona dalili yoyote kwa Xaviena. Hadi kipengele cha kuulizwa maswali kinaanza Xaviena bado yupo vizuri kabisa.
“Mbona kama dawa haifanyi kazi?”
Asha alimuuliza Khadija kwa kumnong’oneza huku wakimsikiliza mshiriki mwezao jinsi anavyo hojiwa na majaji jukwaani.
“Hata mimi nina shangaa, kwa maana mtaalamu alisema tukimshika tu basi ataanguka”
Hadi wana baki Asha na Xaviena kwenye eneo walilopo, hapakuwa na dalili yoyote ya Xaviena kuanguka au kuudhurika kwa mbinu za kishirikina walizo zitumia. Asha akaitwa jukwaani na akahojiwa maswali yake kisha ikafwatia zamu Xaviena.
Xaviena akiwa amevalia gauni refu la rangi ya maziwa huku, likitawaliwa na vimeto meto vya kung’ara, akaanza kukatiza jukwaani huku akitembea kwa mwendo wa kuvutia sana. Shangwe zikazidi kurindima ukumbi mzima. Xaviela akakabidhiwa maiki, akawapungia mashabiki wake mkono huku akisubiria swali kutoka kwa jaji aliye andaliwa kuuliza maswali.
“Xaviela Eddy, nianze na swali kwenye upande wa michezo. Tutajie refaa aliye chezesha fainali za kombe la dunia mwaka 2002. Na ni timu gani ziliingia fainali katika kombe hilo mwaka 2002”
Swali hilo likazua minong’ono mingi ukumbini kwani wengi wao wana hisi ni swali gumu. Xaviena akatabasamu huku akiwatazama wazazi wake pamoja na dada yake. Gafla akaanza kuhisi kizunguzungu kikali sana huku macho yake yakianza kutawaliwa na giza. Akajaribu kusimama wima ila akashindwa na kujikuta akianguka chini mzima mzima na kufanya watu wote ukumbini kujawa na taharuki kubwa.
ITAENDELEA

Usisahau kushare post hii.👍 Share facebook, twitter, Google+ n.k bila kusahau WhatsApp! Share kote wenzio nao wasome

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4