Sunday, 16 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SIMULIZI MPYA: TANGA RAHA 05 & 06 (Return Of Olivia Hitler)



Eddy kwa haraka akasimama na kuanza kukimbilia jukwaani, huku baadhi ya waandaji wa shindano hilo nao wakimuwahi Xaviena eneo hilo alilo lala. Madaktari wa shindano hilo nao hawakuwa nyuma kuhakikisha kwamba wana mpa Xaviena huduma ya kwanza. Madaktari wakambeba Xaviena kwa haraka na kumuingiza kwenye gari la wagonjwa huku Eddy akiwa miongoni mwa watu walio panda kwenye gari hilo la wagonjwa na kuelekea katika hospitali ya Bombo.
Xaviela kwa haraka akamshika mkono mama yake ambaye ameishiwa hata nguvu za kusimama. Hakutarajia kumuona mwanaye akianguka katika hatua za mwisho za mashindano hayo.
“Olvia kama umefanya jambo kwa mwanangu ninakuomba uweze kuligairisha, tafadhali”
Maneno ya Rahma yakamshangaza Xaviela ambeya bado haelewi kwa nini mama yake amezungumza hivyo.
“Sijafanya chochote Rahma”
“Sawa kwa nini mwanangu amekuwa hivyo?”
“Twendeni hospitali”
Wakatoka nje na kuingia katika gari la Olvia Hitler na kuanza safari ya kuelekea hospitali ya Bombo. Baada ya taharuki ya Xaviena kuanguka kupungua, majaji wakaanza kujadiliana juu ya kumtaja mshindi kwani Xaviana ndio ameongoza kwa maksi kati ya washiriki wote.
“Hata kama angepeta maksi sifuri kwenye huu mzunguko bado angekuwa ni mshindi”
Jaji mmoja alizungumza huku akionyesha karatasi yake.
“Kwa hiyo tumekubaliana kwamba Xaviena ndio mshindi?”
“Yaa tumpe haki yake, yeye ndio mshindi”
“Sawa kama ni hivyo”
Wakajumlisha maksi za washiriki wote kisha matokeao hayo akakabidhiwa mkurugenzi wa mashindano hayo. Matokeo yakanza kusomwa kuanzia mshindi wa tatu, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Asha ambaye alihisi kwamba ataishikilia namba moja. Hiyo ni kutokana na Xaviena kuto shiriki hatua ya mwisho ya mashindano hayo. Kutangazwa kwa ushindi kwa Xaviena, hapakuwa na mtu aliye pinga juu ya ushindi wake. Kila mtu aliweza kuridhika kwa ushindi wa binti huyo kwani juhudu aliyo ionyesha toka mwanzo wa mashindano hayo ndio umimpa nafasi ya ushindi.
***
Xaviena akapokelewa na madaktari na kwa haraka akakimbizwa katika chumba cha matibabu. Eddy pamoja na baadhi ya waandaaji wa shindano la miss Tanga wakabaki nje ya chumba hicho.
‘Huyu shetani ameamua kumdhalilisha mwanangu’
Eddy alizungumza kimoyo moyo huku akizunguka zunguka kwenye kordo hiyo. Xaviela na Rahma wakafika kwenye eneo hilo huku wote wakishindwa kujua ni wapi walipo muacha Olvia ambaye walishuka naye kwenye gari.
“Eddy mwanangu ana endeleaje?”
Rahma aliuliza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Madaktari bado wapo ndani wana mshuhulikia”
“Ohoo Mungu amsaidie”
Rahma alizungumza huku akimkumbatia mume wake. Olvia Hitler, akaingia katika chumba alicho lazwa Xaviena pasipo mtu yoyote kumuona. Akamtazama Xaviena na kuona jinsi sumu ikiwa imetapakaa kwenye mwili wake na amebakisha muda mchache sana kupoteza maisha. Madaktari wanao hangaika na kumpima kila aina ya vipimo na kumtundikia dripu za maji, hakika hakuna wanacho weza kumsaidia.
Olvia kwa haraka akaisogelea shingo ya Xaviena na kuanza kuinyonya sumu hiyo ambayo imeingia kimazigara. Zoezi la kuitoa sumu hiyoikamchukua dakika kumi na akaimaliza. Xaviena akastuka kutoka katika janga la kifo na kuwafanya madaktari kujawa na furaha wakiamini kwamba juhudi zao ndio zimemfanya binti huyo kurudi katika hali yake ya kawaida.
“Hei unajisikiaje?”
“Nipo wapi hapa?”
“Upo hospitalini umeletwa mara baada ya kuanguka jukwaani”
Xaviena taratibu akavuta kumbukumbu na kukumbuka hatua ya mwisho alivyo kabidhiwa maiki jukwaani na baada ya hapo hakuweza kuelewa ni nini kilicho tokea.
“Wazazi wangu wapo wapi?”
“Wapo hapo nje”
“Nawaomba”
Daktari mmoja akatoka na kuwajulisha Eddy na familia yake kwamba binti yao amezinduka. Wakaingia ndani ya chumba hicho, wote walipo mkuta Xaviena yupo kwenye hali ya kawaida, wasiwasi na mashaka yakapungua. Olvia alipo ona Eddy na familia yake wapo salama salmin akaondoka katika chumba hicho pasipo mtu yoyote kuelewa juu ya uwepo wake ndani humo.
***
Olvia Hitler moja kwa moja akaelekea hadi ukumbini walipo washiriki wengine huku lengo na nia yake ni kuhakikisha ana wababanisha Khadija na Asha. Akaifka ukumbini kwa wakati sahihi, kwani warembo wote bado hawajarudi hotelini. Oliva Hitler moja kwa moja akaelekea katika eneo alilo simama Asha na shosti yake ambao wanaendelea kusherekea zawadi walizo pewa.
“Habari zenu warembo?”
Olvia alizungumza huku akiivua miwani yake.
“Salama habari yako dada”
“Safi, nina weza kuwaomba kitu”
“Bila shaka”
“Nahitaji munipeleke kwa mganga ambaye amempatia sumu Xaviena hadi akaanguka jukwaani”
Maneno ya Olvia Hitler yakamstua sana Asha na Khadija ambao wanaamini kwamba siri ya kumdhuru Xaviena wao pekee ndio wanao fahamu.
“Una…una…una zungumza nini?”
Khadija alijibu huku akijing’ata ng’ata.
“Munatambua fika mulicho kifanya. Mulihitaji kumfanya Xaviena kuwa kipofu na kufa kabisa. Wewe Asha ndio ulipaka dawa mkononi mwako na kumshika Xaviena kwa lengo la kumdhuru. Ili niwaache salama na nisiwadhuru, nina hitaji munipeleke kwa huyo mganga. Lasivyo, adhabu muliyo mpatia Xaviena ndio nitakayo wapatia ninyi”
Asha na Khadija wakajikuta wakianza kutetemeka kwa woga.
“Nipelekeni wakati huu”
“Sa…sa…sa…yeye ana ishi mbali”
Khadija aliendelea kuzungumza kwa wasiwasi mkubwa sana.
“Umbali sio jambo la kuhofia. Tuondokeni sasa hivi na nina gari langu hapo nje”
“Wewe ni nani?”
Asha alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama Olvina Hitler usoni mwake. Olvia akamshika Asha tumbo lake, maumivu makali sana, mithili ya tumbo la hethi, yakalitawala tumbo la Asha na kumfanya uso wake utawaliwe na mikunjoya maumivu iliyo mstua sana Khadija. Olvia Hitler akamuachi Asha tumbo lake na akarudi katika hali yake ya kawaida.
“Nina imani kwamba umesha nitambua mimi ni nani. Haya nipelekeani alipo mganga wenu”
Asha na Khadija hawakuwa na uwezo wa kupinga tena na ikawabidi kukubaliana na ombi la Olvia Hitler kuelekea alipo mganga wao.
***
“Dokta mwanangu alikumbwa na tatizo gani?”
Eddy aliuliza huku akimutazama daktari aliye simama naye pembeni mwa kitanda alicho lazwa Xaviena.
“Ni mstuku tu ndio umemfanya kupoteza fahamu”
“Mstuko huo umesababishwa na nini?”
“Nahisi kwa kusimama kwa muda mrefu, au alifanya kazi kwa muda mrefu”
“Itakuwa ni vile alivyo kuwa anacheza pale jukwaani”
Xaviela alizungumza na kuwafanya watu wote kumtaza.
“Je tunaweza kwenda naye nyumbani leo?”
Rahma naye aliuliza huku akimtazama dokta Masawe.
“Ndio inawezekana”
“Tutashukuru”
Baada ya musu saa Xaviena akaruhusiwa kutoka hospitalini hapo. Wakarudi nyumbani kwao huku wakiwa wamejawa na furaha kwa kusikia kwamba Xaviena ndio ameshinda taji hilo la miss Tanga.
***
“Huyo mganga wenu ana ishi wapi?”
Olvia Hitler aliwauliza mara baada ya wote kuingia ndani ya gari.
“Anaishi Pongwe, kijiji kimoja kina itwa Maranzara.”
Asha alijibu kwa unyonge. Safari ikaanza huku ukimya ukiwa umetawala ndani ya gari hilo. Wakafika katika mji wa Pongwe na kuzidi kusonga mbela hadi kwenye kijiji hicho cha Maranzara. Wakafika katika nyumba moja majira ya saa tisa usiku.
“Shukeni”
“Olvia Hitler aliwamrisha na taratibu wakashuka. Khadija akagonga kwenye mlango huo wa bati wa nyumba hiyo iliyo tengenezwa kwa nyasi na kuezekwa kwa makuti. Baada ya dakika kadhaa mlango ukafunguliwa na mzee mmoja mfupi na mwenye mvi nyingi sana kichwani mwake.
Mzee huyo mara baada ya kumuona Olvia Hitler mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa woga. Olvia Hilter akanyoosha mkono wake wa kulia huku akiwa amemuelekezea mzee huyo, huku Olvia akiwa amesimama eneo alilo simamisha gari lake.
Asha na Khadija wakashikwa na mshangao mara baada ya kumuona mzee huyo akinyanyuliwa juu kisha akabamizwa chiini kwa nguvu sana na kupoteza maisha hapo hapo. Asha na Khadija wakajikuta wakianguka na kupoteza fahamu, kwani kwa maisha ya kawaida si rahisi kwa mtu kuweza kuhushudia vitu kama hivyo. Olvia Hitler akawabeba Asha na Khadija na kuwarudisha hotelini walipo wezao.
***
Siku iliyo fwata, Xaviena akakabidhiwa taji lake la miss Tanga mbele ya waandishi wa habari. Akakabidhiwa zawadi zake huku akisaini mkataba wa kucheza filamu na mastaa kutoka nchini Marekani.
Xaviena akapata mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya Cocacola kwa Afrika mashariki kwa miaka miwili, huku kila wiki akilipwa kitita ya dola za Kimarekani laki moja.
“Mdogo wangu maisha yako yamebadilika sana”
Xaviela alizungumza huku wakiwa chumbani kwao.
“Yemebadilika kwetu sisi na si kwangu peke yangu”
“Sasa wewe ndio mwenye mikataba ya kufanya mambo mengi sana na makampuni makubwa. Hapo unahisi kwamba mimi nina nafasi ya kusema kwamba maisha yamebadilika hadi kwangu?”
“Usijali Xaviela, nitakuachia uweze kuigiza kwenye filamu hiyo ya Wamarekani kwa maana wewe ndio una penda sana kuigiza kuliko mimi”
“Hee si watajua kwamba mimi sio muhisika?”
“Xaviela, mimi na wewe ni kitu gani ambacho tumetofautiana? Kuanzia kutembea, kuzungumza, kuandika, kucheka yaani vyote tumefanana na hakuna mtu wa nje ambaye ana weza kututofutisha zaidi ya baba na mama.”
“Ila ni kweli”
“Tofauti ya mimi na wewe ipo kwenye kupenda. Mimi sipendi mambo ya kupambana na kuminyana minyana. Wewe hupendi mambo ya urembo na tofauti hiyo ni ngumu sana kwa mtu wa nje kuweza kututofautisha.”
“Sawa nimekueewa, ehee ninaanzia wapi kukutana na watu hao?”
“Wewe jiandae katika hilo dili likija utafanya wewe pasipo mtu mwengine kufahamu kwamba wewe sio mimi”
“Sawa, ila kuna jambo nina hitaji unishauri”
“Jambo gani?”
“Nahitaji kuwa jasusi”
“Nini?”
“Ndio nahitaji kuwa jasusi. Yaani kila ninapo kaa moyo wangu wote una tamani kwenda huko”
“Xaviela una jua madhara ya kuwa jasusi?”
“Ndio nayatambua”
“Unatambua wewe ukiwa mpelelezi, mimi utaniweka kwenye hali gani endapo watu wabaya wakitambua kwamba wewe ni mpelelezi?”
Swali la Xaviena likamfanya Xaviela kukaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akikosa la kumjibu mdogo wake.
“Moja ya matokea mabaya ni kwamba wata nidhuru mimi, lazima watahitaji kunia wakiamini wewe ni mimi. Wakiniua ni nini utakacho kipata kwenye hiyo kazi yako. Ukiachilia kuniua tu, je baba na mama watakuwa kwenye hali gani juu ya kazi yako. Kama kweli una nipenda basi chagua kazi nyingine ya kufanya. Nimekupa dili hilo la kucheza filamu, fanya hivyo kwa maana nina imani utalipwa kiasi kikubwa sana kuliko hata hizi pesa nilizo zitengeneza mimi katika kipindi hichi”
Maneno ya Xaviena yakakatisha kabisa ndoto za Xaviela ambaye siku zote hawezi kufanya jambo lolote kinyume na pacha mwenzake.

SEHEMU YA SITA


“Nimekuelewa. Je utaendelea na masomo ikiwa umesha kuwa maarufu?”
“Hapo ndipo ninapo pata wakati mgumu kwa kweli. Ila tutaangalia jinsi itakavyo kuwa dada yangu.”
“Ehee kuna jambo sijakuambia Xaviena”
“Jambo gani?”
“Tulio kuwa ukumbini, tulikaa na dada mmoja anaitwa Olvia Hitler. Ila baba na mama walionekana kuwa na mahusiano mabaya na huyo dada”
“Olivia Hitler!!?”
Xaviena alizuliza huku akiwa amejawa na mshangao.
“Ndio anaitwa Olvia Hitler. Baba alimtupia lawama kwamba aachane na sisi watato wake. Sasa sijajua kuna uhasama gani unao endelea kati ya wazazi wetu na yule dada”
“Sasa hapa ninaanza kupata picha”
“Picha gani?”
“Unakumbua ile siku ulipo kuja kunitembelea hotelini?”
“Ndio nina kumbuka”
“Ile siku nilipo toka kukusindikiza tu, nikakutana na huyo Olvia Hitler. Alimuulizia baba na akawa rafiki yangu na hata mulivyo chelewa kuja ukumbini siku ile, yeye ndio alinifariji na nikajikuta nikiwa na amani moyoni mwangu hata nyinyi sikuweza kuwafikiria kabisa.”
“Mmmmm ngoja kwanza”
Xaviela alizungumza huku akijaribu kuvuta kumbukumbu zake. Akakumbuka siku walipo kuwa wakienda ukumbini gari nyekundu iliyo kuwa ina wapigia honi na kuwawashia taa kwa fujo, ndio gari hiyo hiyo ambayo waliipanda yeye na mama yake wakielekea hospitali ya Bombo kumuona mdogo wake.
“Unafikiria nini?”
“Siku ambayo tunakuja ukimbini tulipata ajali”
“Ajali?”
“Ndio na gari lililo tusababishia ajali ni hilo gari la Olvia na gari hilo hilo ndio tulienda nalo hospitali”
“Aliwasabishia ajali majira ya saa ngapi?”
“Kama saa tatu usiku hivi.”
“Mbona muda huo nilikuwa naye ukumbini”
“Mmmm”
“Ndio tena muda huo nilikuwa nina wasiwasi mkubwa sana kuhusiana na nyinyi. Ila mara baada ya kuzungumza naye kila kitu kuhusiana na nyinyi kikapotea”
“Kuna haja ya kuwauliza baba na mama ni nini kinacho endelea”
“Kweli”
Xaviela na Xaviena mara baada ya kushauriana wakatoka chumbani kwako na moja kwa moja wakaelekea katika chumba cha wazazi wao. Wakagongwa na kuruhusiwa kuingia ndani. Wakamkuta mama yao akiwa tayari amesha amka huku Eddy bado akiwa usingizi. Wakawasalimia wazazi wao kisha wakakaa kwenye sofa zilizomo chumbani humo.
“Mbona asubuhi asubuhi, hamjalala nini?”
“Tumelala mama ila tumewahi kuamka”
“Haya ni nini kilcho walete asubu asubuhi yote hii.”
“Mama tunahitaji kujua ni kitu gani kinacho endelea kati yenu na Olvia Hitler?”
Swali la Xaviela likamfanya Rahma kukaa kimya kwa sekunde.
“Olvia amejenga urafiki na mimi kabla hata ya mashindano. Niambieni nini ni kinacho endelea”
Xaviena akazidi kumchanganya Rahma.
“Eddy hembu amka uwajibu wanao”
“Nimewasikia”
Eddy alijibu kwa unyonge huku akikaa sawa kitandani mwake.
“Hembu njooni mukae hapa”
Xaviena na Xaviela wakakaa kitandani na kumtazama baba yao.
“Siku zote tumekuwa ni watu ambao hatuwezi kuficha siri au kuficha kila kinacho endelea kwenye maisha yetu. Ila katika hili wanangu ninaomba niweze kuwajibu kwa jibu moja tu. Olvia Hitler ni mtu mbaya kwenye hii familia”
“Ni mbaya kivipi na ikiwa hakuna kitu kibaya alicho kifanya. Kwanza alinifariji na kunipa ujasiri wa kushiriki yale mashindano ya umiss. Kwa nini nimuone ni mbaya”
Xaviena alizungumza kwa ujasiri, Rahma macho yakamtoka kwani hakutarajia kwamba Olvia Hitler tayari alisha tengeneza mazingira ya urafiki kwa mwanaye.
“Ubaya alio ufanya kwetu, ni kutusababishia ajali, siku ambayo tulikuwa tuna kuja ukumbini”
“Ila baba ile ajali si yeye aliye tusababishia”
“Ni nani kama si yeye?”
“Wewe ndio ume sababisha ile ajali. Mama alikuwa akikuomba, upunguze mwendo na umuache Olvia Hitler apite na gari lake ila wewe uling’ang’ania kuenda naye sambamba hadi matokeo yake tukaacha barabara na kugonga mti”
Maelezo ya Xaviela yakamfanya Eddy kukosa cha kujitetea.
“Olvia ni nani na kwa nini baba ulimuambia aachane na sisi wanao”
Xaviela aliendelea kuhoji na kumfanya Eddy atamani kuwafokea, ila kutokana alisha tengeneza malezi ya haki mbele ya wanawe, akajikuta akishindwa kabisa kujibu swali hilo.
***
Uwekezaji wa makampuni makubwa ya burudani aliyo yafungua Olvia Hitler, nchini Tanzania na katika jiji la Tanga. Vikabadilisha kabisa muonekano wa jiji hilo. Kumbi kubwa za starehe pamoja na mahoteli makubwa na ya kuvutia, yakawafanya watu kutoka mikoa mbali mbali, kufika jiji la Tanga kwa ajili ya kupumzika siku za weekend.
“Kuna mambo mawili nahitaji kuyafanya juu ya Eddy”
Olvia alizungumza na msaidizi wake, ambaye naye si binadamu bali ni jini mwenye kukaribia uwezo kama wake.
“Kitu gani?”
“Nahitaji kuvuruga amani katika familia yake. Nahitaji wanaye wenyewe ndio wampotezee amani”
“Kwa jinsi watoto wake wanavyo mpenda baba yao una hisi kweli hilo linaweza kufanikiwa?”
“Umesahau kwamba sisi ni kina nani?”
“Sijasahau mkuu”
“Hivyo hakuna ambalo lina shindikana. Nahitaji kuhakikisha kwamba familia yake ina gawanyika vipande vipande.”
“Ehee jambo la pili ni lipi?”
“Nahitaji kumsaidia kwenye ubunge”
“Nini? Unataka kumpa nguvu Eddy akawa mbunge?”
“Ndio?”
“Kwa nini sasa?”
“Kupitia ubunge wake ni lazima tuhakikishe kwamba ana kutana na skendo kubwa na mbaya sana ambazo zitakimbilia kumteketeza kisaikolojia na ikitokea hivyo. Basi mambo yatakwenda poa na kila jambo litakwenda vile ninavyo hitaji”
“Hapo nimekuelewa kwa maana endapo atakumbana na skendo mbaya basi ata kufa kwa mstuko wa moyo?”
“Wala sinto ruhusi afe kwa mstuko wa moyo. Ila nina taka kumfanya aonekane kuwa ni takataka kama vile toilet pepar na akifikia hatua hiyo, basi hakuna ambaye ata muheshimu kama anavyo heshimiwa wakati huu”
“Je mke wake Rahma uta mfanya nini?”
“Rahma mmmmmm…..Nitajua cha kumfanya mbele ya safari. Ila huyu panya aliye nifanya nirudi dunia ni lazima nihakikishe nina mvuruga taratibu”
Olvia Hitler alizungumza huku akiwa amesimama kwenye gorofa refu sana la hoteli yake. Huku akilitazama jiji la Tanga kwa chini.
***
“Ni hivi Olvia Hitler sio binadamu”
“Sio binadamu. Hahaa baba haupo serious”
Xaviena alizungumza huku akicheka.
“Nipo serious na si mme hitaji kufahamu ukweli wake. Basi ninacho kizungumza ndio hicho”
“Sasa baba kama Olvia si binadamu. Yeye ni nani?”
Xaviela naye aliuliza swali lililo zidi kumbananisha Eddy.
“Ni jini”
“Jini!!?”
“Jini gani ambaye anaweza kuishi na watu na kuzunugmza na watu. Mbona chini hana kwato kama hao majini wengine tunao wasikia?”
“Xaviena nielewe mwanangu. Nina wapenda ndio maana nina wakataza kuwa na mahusiano ya karibu na Olvia Hitler”
“Mama una ona tunadanganywa na baba hapa na wewe ume kaa kimya. Ehee?”
“Hadanganyi anacho kizungumza baba yenu ni ukweli kabisa.”
“Tudhibitishieni kwamba Olvia Hitler ni jini?”
Swali la Xaviela likamfanya Eddy kukurupuka kitandani kwa hasira sana. Akawatazama mabinti zake hawa.
“Pumbavu sana. Tunapo zungumza kitu muna paswa kutuelewa na si kuhoji. Munahoji kama kina nani. Kumbukeni sisi ndio wenye amri juu yenu na si nyinyi kuwa na mri juu yetu mume nielewa?”
Eddy alifoka hadi kila mtu ndani ya chumba hicho akabaki akiwa ameshangaa. Toka wazaliwe hawakuwahi kumuona baba yao akikasirishwa na maswali yao.
“Nimesema Olvia Hitler ni jini basi. Tambueni hilo na hakuna mtu yoyote ambaye ana paswa kukutana naye na endapo mutafanya hivyo nita wafukuza ndani kwangu. Shenzi nyinyi”
Kauli ya kuwafukuza watoto ndani ya nyumba ikamshangaza sana Rahma. Hakutarajia kinywa cha mume wake kutoa matamshi kama hayo.
“Eddy hayo sio maneno mazuri ya kuwaambia watoto”
“Kaa kimya na wewe. Watoto watoto nini? Nimepitia mateso na shida hadi nyinyi watatu kuishi maisha ya amani kama hivi. Sasa hivi munataka kufukua makaburi ambayo yamesha fukiwa miaka mingi kwa nini?”
Eddy aliendelea kufoka huku macho yake yakitawaliwa na uwekundu utokanao na hasira.
“Toka na hawa panya wako kabla sijafanya kitu ambacho sijatarajia kukifanya kwenye maisha yangu”
Maneno ya Eddy yakaanza kuwaliza Rahma na wanae. Taratibu Rahma akawashika mkono wanaye na kuanza kutembea nao kuelekea mlangoni. Taratibu Xaviela akauachanisha mkono wake na mkono wa mama yake. Akageuka na kumtazama baba yake huku akiendelea kulia kwa uchungu.
“Baba leo hii umetuonyesha rangi yako halisi. Huna upendo na sisi, huna mapenzi na sisi. Umekiri kwa kinywa chako kwamba sisi ni panya. Mama amekuzalia wewe panya, acha tuondoke nyumbani kwako kwa hiyari. Kwani siku ukitufukuza hatuto jua ni wapi kwa kwenda”
Xaviela alizungumza kwa upole na unyonge mkubwa sana. Taratibu mama yake akamshika mkono wake na wakatoka chumbani humo.
Xaviela akaanza kutembea kwa haraka akielekea chumbani kwake. Hadi Rahma na Xaviena wanafika chumbani hapo, tayari wakamkuta Xaviela akiwa tayari amesha kusanya nguo zake wa ajili ya kuondoka nyumbani hapo.
“Xaviela mwanangu. Tafadhali punguza jazba?”
“Jabza mama? Ni nini kibaya tumekifanya kwa baba hadi atuite sisi panya mara hoo atatufukuza ni nini mama? Kuhoji kwetu kume kuwa ni tatizo. Tazama hadi wewe mke wake wa ndoa ana kuzalilisha mbele yetu ni haki kweli. Au kisa yeye ni mwanaume basi kila anacho kizungumza ndio kionekane sawa mbele za wengine hata kama kina umiza moyo eheee?”
“Nalitambua hilo mwanangu. Ila baba yenu ana hasira, toka akutane na Olvia Hitler kichwa chake hakipo sawa. Mueleweni basi wanangu”
“Sina haja ya kumuelewa mtu kama huyo mama. Acha niondoke zangu”
“Hakuna kwenda sehemu yoyote na ukifanya hiyo. Nitakuua kwa mikono yangu mimi mwenyewe.”


Sauti ya Eddy ikawastua watu wote ndani ya chumba hicho. Woga ukawatawala mara dufu baada ya kumuona Eddy akiwa ameshika bastola na taratibu akamnyooshea Xaviela sehemu alipo simama.


ITAENDELEA

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4