Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

RIWAYA: Sorry Madam – Sehemu ya 07



ILIPOISHIA
Mapigo ya moyo yakazidi kunienda mbio na kujikuta nikianza kuomba sala ya kuniepusha na kukamatwa kwetu kwani ni muda mchache ulio pita baba alitoka kunionya kwa ujinga kama huo.Nikamtazama Salome na taratibu nikamuona mwenzangu akilegea kabla hajaanguka nikamuwahi kumkumbatia ili asianguke chini na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa
ENDELEA
Nikaendelea kumshikilia Salome ambaye anahema Kwa pumzi za taratibu kutokana na giza sikujua kama ameyafumba macho yake.Mlango ukatingishwa kidogo kama mtu anayetaka kufungua na kuingia.
“Eddy…..Eddy”
Nikasikia ni sauti ya chini ya John ikiniita nje ya mlango, Nikawa na wasiwasi huenda atakuwa yupo na walinzi au mwalimu ili iwe rahisi kwa kunikamata endapo nitaitiaka.Akarudia kuniita tena ila nikakausha kimya nikamsikia akiendelea kufjngua fungua vyoo vingine na baada ya muda sikumsikia tena.
“Salome Salo”
Nilimuita Salome huku nikimtingisha taratibu ila mwenzangu hakunijibu kitu chochote.Nikakumbuka baba alinipa simu nikaitoa mfukoni na kuiwasha nikammulika Salome nikakuta mwenzangu macho yake yamebadilika na kiini cheusi cha kati kati ya jicho sikukiona na kulifanya jicho lake lote kuwa jeupe.Mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku taratibu nikihisi umoto moyo kwenye mapaja yangu na kuifanya suruali yangu kulowana nikajua moja kwa moja mtu mzima nimesha limwaga mbele ya Salome ambaye sielewi amepatwa na nini.
Kwa jinsi miguu inavyotetemeka nikashindwa kuizuia hali ya kulimwaga kojo ambalo linachuruzika kwenye mapaja kwa kasi huku likiwa la moto moto na mbaya zaidi nimetoka kuchimba mgodi muda si mrefu na sikufiki mwisho wa uchimbaji.Kwa uzito wa Salome na kukosa kangu muhimili wa kusimama nikajikuta nikianza kushuka chini taratibu huku mgongo ukiwa una buruzika ukutani hadi nika kaa chini,Nikaendelea kumnong’oneza Salome ila mwenzangu hakuitika sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kumkumbatia huku kichwa chake akiwa amekilaza juu ya kifua changu,cha kumshukuru Mungu ni vyoo tulivyopo hakuna hata kimoja ambacho kimetumika kwani ndio kwanza vipya vinamsubiria diwani aje kuvizindua siku mili mbeleni.Nikaanza kumlaani John kwa masihara yake nikahisi kwamba ilikuja kunitania na utani wake umweniachia majanga ambayo sijui niyamalize vipi kwani hata kusimama ninashindwa kwa jinsi suruali yangu ilivyo lowana na mbaya zaidi mwili mzima unanitetemeka
Nikatazama saa ya kwenye simu nikakuta ni saa tano kasoro usiku,nikaendelea kusubiri huku mara kwa mara nikiwa ninamtingisha Salome ili azinduke.Baada ya masaa mawili kupita huku nikiwa nipo macho gafla Salome akaiga chamfya nikaiwasha simu na kummulika Salome usoni nikakuta anaanza kufumbua fumbua macho na matumaini ya kuto kulala chooni yakaanza kunijia kwani nilishakata tama nikajua ni lazima nitalala chooni.
“Salome”
“Mmmm”
“Unajisikiaje”
“Mmmmm”
“Unajisikiaje….?”
“Kidogo afadhali”
“Unaweza kusimama?”
“Mwili hauna nguvu”
Ikanilazimu kusubiri ili Salome nguvu ziweze kumrudia.Masaa yakazidi kukatika huku kila nikimuuliza Salome juu ya kurejewa na nguvu anadai bado.Nikaanza kupata wasiwasi kwani hadi sasa hivi imesha timu saa tisa usiku.Kijimwanga kikaanza kuchomoza na kuingia katika uwazi wa chini katika choo.Nikashangaa Salome akikurupuka na kusimama kama mtu aliyekuwa akiota ndoto mbaya
“Eddy tupo wapi?’
“Chooni”
“Tupo chooni Eddy…..bwenini kwetu hawajachukuliwa rollcal?”
Swali la Salome sikujua nilijibu vipi kwani hata mimi mwenyewe sikujua kama bwenini kwetu watu wamehesabiwa namba
“Salome cha msingi wewe uende mbwenini kwenu sasa hivi mambo mengine tutazungumza baadaye tukionana”
“Kwani ni saa ngapi Eddy?”
“Saa kumi na mbili kasoro”
Nikafungua mlango wa chooni nikachungulia nje,nikaona kupo salama hakuna mtu nikampiga busu Salome kisha nikatoka na kuelekee kwangu bwenini kwa ajili ya kujiandaa kwa ajili ya msomo.Nikamkuta John akiwa bado amelala sikutaka kumsumbua nikapanda kwenye kitanda changu ambacho kipo juu nikajilaza ili kuupuumzisha mwili ila nikakumbuka kuwa nimejikojole.Nikaivua suruali pamoja na boxer yangu japo kuna baridi kali ila ikanilazimu kwenda bafuni kuoga
Nikarudi na kukuta watu wengeni wakianza kuva nguo za darasani huku wengine wakiwa wanaelekea kupiga mswaki
“John vipi hembu amka kwanza?”
“Eddy mwanangu nina umwa?”
“Una umwa na nini?”
“Eddy wee acha tu mwanangu jana yaliyo nikuta nimakubwa”
Kwa jinsi ninavyo mjua John kweli nikagundua anauwmwa kwani hata kuzungumza kwake ni kwa shida
“Sasa nikufanyie mpango kwa Patroni(Mlezi wa kiume) akupeleke hospitali”
“Ndio mwanangu hapa sijielewi kabisa”
Nikavaa nguo za darasani na kwenda katika chumba cha Patron na kumueleza juu ya kuumwa kwa John.Ila Patron akaniomba nimsindikize John hospitali kwani yeye anakwenda kushuhulikia kumtafuta msichana mmoja aliye potea jana usiku.Moyo ukaanza kunienda mbio huku nikiwa na wasi wasi
“Patroni huyo msichana aliye potea ni wakidato cha ngapi?”
“Kidato cha tano”
Sikutaka kujitia mawazo kwani moja kwa moja msichana aliyelala nje ya bweni alikuwa ni Salome na kwa jinsi wasichana wanavyo lindwa huwa huesabiwa kila mara wakati wa usiku nikamuaga Patroni na kutoka kwenda bwenini kumchukua John.Nikaikuta hali yake ikiwa imezidi kuwa mbaya kwani mwili mzima ulikuwa ukimtoka jasho.Nikasaidiana na rafiki zangu wengine kumuwahisha John hospitali huku moyo ukianza kupata mashaka juu ya hali ya John.Tukafika hospitali ya shule akapokelewa na manesi na kumtundikia dripu la maji.
Wezangu wengine wakaenda darasani mimi nikabaki hospitali huku nikiwa na kazi ya kumfuta John jasho linalo mwagika huku wasiwasi ukizidi kunijaa juu ya afya ya John
“Eddy”
“Niambei ndugu yangu”
“Eddy ninakufa kaka”
“John husi kamanda wangu”
John akacheka taratibu huku akinishika mkono huka anatetemeka.Nikazidi kupata wasi wasi huku machozi kwa mbali yakianza kunilenga lenga.Dokta akaanza kumfanyia John vipimo vyote ila hakumkuta na ugojwa wowote
“Eddy jana mwenzako ni….nili…..kuwa nipo na Clau…..”
“Ndio kaka”
“Tulikuwa darasa la kule chini basi kuna ki…..tu ki….linipiga kifuani il…a siku..jua ni ni..ni”
“Ikawaje kaka?”
“Nikaja kukufwata kule ulipo ila sikukupata wakati naru…I pale darajani nikao…….oo….oo..”
Gafla John akaanza kutingishika kama mtu mwenye kifafa huku akiwa amening’ang’ania mkono wangu.Manesi wakaanza kumshika ili kuutuliza mwili wake huku nikisaidiana naye.Machozi yakaanza kunimwagika kwani hali ya John ikazidi kuwa mbaya,Puvu jingi likaanza kumtoka huku puani akiwa anatokwa na damu
“ED…….”
John akajitahidi kuniita ila kinywa chake hakikuweza kufunguka na suati yake ikakata gafla na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.Sikuweza kuyazuia machozi yangu baada ya kumuona John akiwa ametulia kimya kitandani huku vidole vyake vikiwa vinajifungua taratibu kwenye mkono wangu alio ushika.
“John…..John…..John kaka please wake up you can not die brother you my soujar please”(John…..John……John kaka amka huwezi kufa kaka wewe ni mwanajeshi wangu tafadhali)
Nilizungumza huku machozi yakinitoaka nikiwa najitahidi kumtingisha huku kichwa chake kikiwa nimekiweka kwenye mapaja yangu.Dokta akampima John mapigo ya moyo na nikamuona akitingisha kichwa akimaanisha John amefariki dunia
“John amka rafiki yangu nitasoma na nani mimi”
Manesi wanishika na kunitoa nje huku nikiona wakimfunika John kwa shuka mwili wake mzima.Nikazidi kuchanganyikiwa na kujua hiyo ndio safarai yangu ya mwisho ya kumuona rafiki yangu John ambaye kwangu amekuwa zaidi ya ndugu.Manesi wakanikalisha kwenye benchi huku wakiendelea kunibembeleza
Nikaona kundi kubwa la wanafunzi wa kike wa kidato cha tano likija hospitali huku wakiwa wamembeba mwenzao ambaye anaonekana kupoteza fahamu.Nikasimama na kumuona ni Salome aliye bebwa huku akionekana kuwa na hali mbaya kupita maelezo

ITAENDELAE

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4