Tuesday, 1 April

Ads Right Header

Buy template blogger

𝐒𝐈𝐌𝐔𝐋𝐈𝐙𝐈: 𝐍𝐈𝐓𝐀𝐊𝐔𝐅𝐀 𝐍𝐀 𝐁𝐈𝐊𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐔 𝐄𝐏.... 41





𝐒𝐎𝐍𝐆𝐀 𝐍𝐀𝐘𝐎....
Yaani mimi nilikuwa ninazo funguo za geti lakini huyu bint namuona akitoka ndani wakati alitoka hapa anaenda kutafuta kazi.. Aliingia kwa wapi humu..!!

Aliongea yule bibi.. Na hapo mimi ndio nilijua kuwa Omera kumbe alikuwa ni jini..

Omera alisogea katibu na bibi yake na kumwekea kidole mdomoni.. Bibi alinyamaza kimyaa...

Omera alinishika mkono na kunipeleka ndani..

"Asante jamani omera... Umenisaidia ningekufa mimi jamani...
Niliongea huku nalia..

"usujali... Lakini sikuingine uwe unaaga vizuri.. Kule ulipoensa ndio ulienda kutafuta kazi.???

"hapaana naomba nisamehe omera...

"Sawa ila kuwa makini sana ....
Ninahitaji msaada wako na mimi nitakupa msaada pia..

Hajraaa.. Wewe unao uwezo mkubwa kivita na akili za maisha na umeishi kwenye kila hali.... Najua changamoto zote umepitia .

Naomba msaada wako... Mimi nitakupa msaada wa kukugaia nguvu za kijini pia..

Kunabaadhi ya sehemu za kupigana siwezi mimi naomba uwe unanisaidia...
Aliongea omera

"Sawa omera mimi nitakusaidia katika hilo endapo na wewe utanipatia msaada wa nguvu za kupotea kama ulivyonisaidia leo....

"Usijali hajraaa. Ila tambua kuwa kupaa au kupotea na kutokea sehemu zingine inakula nguvu kubwa sana na tusipokuwa makini nguvu zinaweza kutuishia na kule ujinini hatutaweza kuingia maana mama amepafunga...

Alizidi kuongea Omera..... Duuuuhhhh kumbe vile majini au wachawi wakipotea nakutokea sehemu zingine huwa wanapoteza nguvu nyingi sana...
Niliwaza kimya kimya huku namtaza omera..

"Siyo kupotea nguvu tu.. Yaani tunazeeka haraka na kufa mapema..

Aliongea tena Omera kunijibu mawazo niliyokuwa nikiwaza kimya kimya...

"Sasa tunafanyaje mama yangu...
Nilimuuliza omera..

Omera alikuja kunishika kichwa na kuomba dua zake kwa muda..

Niliona kama moto unawaka mikoni mwake na kuteremka hadi kichwani mwangu ila nilikuwa nikihisi baridi sana..

Mwili ulipata kama ganzi na kuanza kujihisi tofauti... Nilijiona ninayo nguvu kubwa sana kwe mikono na miguu yangu na mwili kwa ujumla..

Nilianza kutetemeka na kudondoka pale kitandani.

Nilipoteza fahamu na kushtuka usiku sana nikiwa na njaa kupita maelezo..

Nilimkuta Omera bado yupo macho anachati tu kwenye simu yake..

Nilimtazama tu na kubaini alikuwa akichati na yule  kaka aitwae JUMA tuliekutana nae sokoni akatupa lift....

Sikujua hata nilitambua vipi.

Niliangalia njee na kuona hadi mtaani na baadhi ya mambo yanayo endelea...

"Omera hii ni nini.???

''hahahahahhaah.... Hahahahhaahahha.... Hahhahahhha ndio tayari dadaangu...
Umeshakuwa jini..

Aliongea omeea huku anacheka..

Nilinyoosha mkono wangu hadi jikoni na kupakua chakula na kuweka maji kwenye glasi kisha kuuleta hadi kitandani na kuendelea kula...

Nilibaki kuchea tu yale maajabu...

"Kuna watu wanafaidi sana hapa duniani... 'niliongea huku namtazama omera na kucheka....

"Hamna ni maisha tu ya kawaida ila  kila kitu kimezidiana na mwenzake..

Sokwemtu huwa anaona bimadam kapendelewa sana... Na binadamu huwa mnaona majini wamependelewa sana.. Na sisi pia tunaona Malaika wamependelewa sana na malaika wanamuona Mungu kajipendelea sana...

Haya ndio maisha...

Ila mwisho wa siku wote tutarudi kwa Mungu mmoja..Aliongea Omera kwa hisia sana...

"Sasa mbona watu wengi huwa wanaogopa majini.?? Na wewe naona unaroho nzuri kuliko majini wengine.???
Niliuliza na kumtazama zaidi..

"Sikia... Hujawahi kuona mwanadam anaroho mbaya na katili sana.???
Au tuchukulie huyo Renatus unaetaka kumuua.. Unadhani angekuwa ni jini angekuwa ni jini wa namna gani.???

Aliuliza omera na kuendelea kuongea..

Majini tupo wengi mara elfu moja ya wanadamu wote duniani na tunazaliwa kila siku... Ila wengi ni wastaarabu na wanaishi maisha yao kumtumikia Mwenyezi Mungi japokuwa kuna wachache wenye roho mbaya wanaokuja kuwadhuru wanadamu...

Aliongea Omera....

"Naanza kukuelewa mamaangu..

Niliongea na kuvuta blanketi kujifunika kulala ...

"kuna jambo nataka tujadili hajra kabla hujalala.. Aliongea Omera ...

"Ndio....

"sasa tunaanza na kazi yako au yangu.???.

Tunaanza na yeyote tu kwani yako inaukubwa gani.?? Au inachukua siku au miezi mingapi.???
Nilimuuliza omera..

"Kazi yangu inafanyiwa Naijeria na inaweza kuchukua siku saba..

Lakini hiyo siku saba ni  siku za kijini.. Ni sawa na miezi saba ya kawaida.. ..

Hembu pima basi yakwangu inaweza chukua siku ngaoi hii ya hapa dar...
Niliongea baada ya kusikia miezi saba kukaa nigeria..

Kazi yako ni kubwa na bado sana.. Inao mkanda mzito sana pia.. Inaweza chukua miezi na siyo wiki kama hii yangu...

"nilinyamaza nikitafakari mwezi mmoja kijini ni miaka mingapi na kubaini ni balaa kweli itakuwa ni kazi kubwa...

Sawa tuanze na yako mamy..

****



Tulilala na asubuhi tulipotea na kutokea lagos..

Tulichukua chumba Lodge na kuweka mizigo yetu kama mabegi..

Ilikuwa ni chumba namba 14..

"Shost.. Mbona tumetoka mlango namba 12 na kilichofuata ni 14.. Namba 13 ipo wapi..??

Nilimuuliza Omera.

"Hayo ni mambo ya kiroho...

Namba 13 huwa inaaminika ni namba ya mashetani..

Tarehe 13 ni tarehe mashetani wengi wanachukua kafara....

Zamani kulikuwa na Miezi 13... Lakini mmzungu baada ya kuona mwezi wa 13 unakuwa na ajali na nuksi nyingi waliufuta na kubakiza miezi 12.. Na zile siku walizisambaza kwenye miezi mingine..

Kawaida Mwezi mmoja ni siku 28 tu...

Mwezi unaandama baada ya siku 28..

Mwanamke huona siku zake baada ya siku 28..

Na zamani mwezi ulikuwa na siku 28 tu kwenye kila mwezi na ndio maana kukawa na miezi 13 kwa mwaka..

Hembu chukua siku 365 za mwaka alafu gawanya kwa 28.. Utaona inakuja miezi 13 net..

Na hiyo ndio sababu namba 13 inaogopwa sana kwenye maisha..

Ukipanda ndege nyingi hazina kiti namba 13.. Au kama ipo huwa hakai mtu..

Mabasi mengi pia hazina kiti namba 13...

Au mahoteli mengi huwa wanatumia majina ya wanyawa au nchi au miji au mbuga za wanyawa kwenye milango ili wasiweke namba ....

Kila namba inayo siri kubwa sana...

Alimaliza kuongea Omera

Uuuuuuubbbhhh.. Nilishusha pumzi na kuvua nguo kwenda kuoga baada ya kusikia siri nzito nisizozijua kuhusu namba... Namba niliyokuwa naisikiaga sana ni 666 tu..

ITAENDELEA....

Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4