𝐒𝐈𝐌𝐔𝐋𝐈𝐙𝐈: 𝐍𝐈𝐓𝐀𝐊𝐔𝐅𝐀 𝐍𝐀 𝐁𝐈𝐊𝐈𝐑𝐀 𝐘𝐀𝐍𝐆𝐔 𝐄𝐏.... 53
𝐒𝐎𝐍𝐆𝐀 𝐍𝐀𝐘𝐎.…
"nani mwanao.. huna haya wewe mwanamke.. wewe na baba yako umeona haitoshi kumuua baba yangu na mama yangu lakini bado unamuwinda binamu yangu mr Renatus umuue, wewe mwanamke ni shetani.. niache usinizoee mimi… aliongea cyprian huku analia na kukimbia nje ya darasa…
Nilijitahidi kumfuata kwa kumkimbiza lakini Marim alikuwa akilia.. Ilibidi nirudi tena kumfuata mwanangu.. Ile natoka njee sikumuona tena alipoelekea cyprian.. Niliuliza baadhi ya walim wakaniambia kakimbilia maeneo ya uwanja wa shule kwasababu kulikuwa na baadhi ya michezo. Nilienda lakini sikufanikiwa kumpata..
Ilinibidi nirudi kwa mwalim mkuu msaidizi ili nimuelekeze hali halisi kwasababu yeye mda mwingi yupo shule.. "Samahani mwalimu... 'Bila samahani mama. Karibu ukae. Aliongea yule mwalimu.. "Samahani kuna mgeni yeyote aliwahi kuja hapa shuleni kwenu siku za karibuni na kuongea na mwanangu.? Niliuliza na kukaa kumsikiliza kwa umakini... " alikuja nabii Renatus yule aliewahi kuwa mkuu wa mkoa.. Alikuja kuonana na mwao akisema ni binamu yake... Aliongea nae sana siku hiyo... Sasa sikujua nini waliongea..
"Ahsante mwalimu.. Huyu mtoto anamatatizo sana.. Kwasasa sijui kakimbia wapi.. Nimekuja kumtembelea lakini naona furaha yangu imeharibika.. Niliongea na kumuaga Mkuu kisha kumwachia namba zangu za simu ili kama atarudi cyprian nipewe taarifa.. Nilimbeba mwanangu na kumpakia kwenye gari.. Kwa mwendo wa haraka na hasira nyingi niliondoa gari pale na kufika nyumbani mchana ule.
Nilitoa machupa ya juice na baadhi ya biskuti na keki nilizokuwa nampelekea cyprian shuleni na kuanza kuzila mwenyewe.. Nilipewa kampan na mwanangu Mariam.. Tulikula tukashiba hata hayukupika tena mchana huo..
" mr Renatus kaja lini Tanzania na anatumia mfumo gani hadi asijulikane ni wapi alipo jamani.?? Tayari kamharibu na kumjengea mtoto chuki dhidi yangu, niliwaza kwa mda huku nambembeleza mwanangu hadi akalala...
Nilimlaza na kuchukua simu kumpigia mkuu wangu wa kazi.. Mr Reginald.. Alipokea sim lakini alikuwa kwenye kelele sana.. "Sema Hajraa ninakusikiliza..
'Mkuu nasikia mr Renatus yupo Tanzania... Kaniharibia kunitangazia chuki kwa mtoto mmoja ambaye nilikuwa nikimtunza.. Kwasasa yule mtoto ananichukia sana mimi.. Niliongea na kunyamaza kimya....
" Hajraa.. Uwe mwelewa.. Nimekwambia Renatus hayupo Tanzania labda kama kuna kundi baya tu linataka kukuvuruga. Kuwa makini.. Renatus hayupo huko..
Alimaliza kuongea boss na kukata sim.. Inamaana mimi nimekua mjinga.. Huyu mtoto hawezi ambiwa uongo akasikiliza.. Ni mtu gani mwenye kufuatilia haya mambo yetu jamanii..
Nilizidi kuumiza akili lakini wapi.. Umri wangu pia ulishaanza kusogea na baadhi ya vitu nilianza kusahau.. Sikuwa na uwezo wakufikiria sana.. Nilikuwa na miaka kama 34..
Nilikuwa nikiwaza sana nahisi hadi kichwa kuuma.. Nilipanda tu kitandani na kumkumbatia mwanangu kisha kulala mchana ule..
***
***
LAGOS NIGERIA
Jioni ilikuwa imeanza kuingia kwa siku hiyo.. Kulikuwa na sherehe ya kutoa baadhi ya tuzo kwa maafisa wakubwa walio wahi kulitumikia kitengo cha usala wa umoja wa mataifa....
Alikuwa ni afisaa mmoja tu mashuhuri aliekuwa akifanya kazi kwenye taifa la tanzania.. Ilifika mda wa kupewa tuzo hiyo ya heshima na zawadi kedekede ..
Ojala na maafisa wengine ambao na wao kwa siku hiyo walikuwa wakipewa baadhi ya maneno kwaajili ya kwenda kulitumikia taifa... Na wengine kusambazawa kwenye nchi zao hasa za somalia na libya ambayo yalikuwa na machafuko sana..
Baada ya chakula vinywaji na mziki mkubwa aliitwa afisa huyo wakupewa heshima, MC kwa madaha aliagiza mziki uzimwe na kumuita mzee wakukabidhiwa tuzo..
"Mr RENATUS kutoka Tanzania tunakuomba.. Mzee huyu kafanya kazi kubwa sana hasa kwenye kundi hili la usalama wa umoja wa mataifa.. Aluwahi kuwa mkuu wa mkoa kule Tanzania.. Aliwahi kuwa hadi mchungaji lakini yote ni kupata taarifa za wauzaji tu wa madawa. Na biashara hii inaenda kufikia hitimisho..
Alimaliza kuongea Mc na mda huo renatus alikuwa anaelekea kupewa taji lake la heshima..
Vigelegele vilienea kulikuwa na wageni wengi sana wakubwa kwa siku hiyo.. Baada ya hapo kila afisa alipewa eneo lake la kazi kwa wale waliokuwa wakihitimu mafunzo kama akina Ojala.. Kwa yeye Ojala alipelekwa Tanzania kumsaidia HAJRAA..
Mambo yalikuwa ni tafrani.. Kumbe na Renatus pia alikuwa ni askari wa umoja wa mataifa.. ila hayo yote tuyaache.. Sherehe iliisha na usiku wa siku hiyo Ojala alibeba vitu vyake na kwenda kukulala lodge..
Asubuhi na mapema aliwahi kupanda ndege inayoelekea tanzania kulingana na teket aliyopewa inavyosema na kwenda kumshusha kwenye uwanja MWALIMU NYERERE INTERNATIONAL AIRPOT.. Walianza safari majira ya saa mbili alfajiri.. Hadi saa kumi nambili kasoro jioni alifika Tanzania.. Alikwenda kutafuta chumba jioni ile na kujiandaa upesi ili akapate chakula cha usiku..
Wakati huo Ojala alikuwa tayari ni jini.. Alikuwa na jukumu la kumsaidia shostiake tu..
Alitoka na kwenda hadi kwenye Pub moja inayoitwa Sarafina ipo maeneo ya Magomeni Mikumi.. Aliagiza chakula na kinywaji kisha kutulia kula taratibu.. Alitamani aende kwa Hajra usiku ule lakini aliona siyo vyema na alishasikia kuwa hajra kaolewa na anae mtoto..
Kama ilivyo kawaida ya wanaume wengi wa Tanzani huwa hawapendi kuona mwanamke yeyote kakaa mwenyewe bar anakula na kunywa.. Huwa wanahisi huenda wanajiuza..
Haikuchukua dakika kadhaa alikuja mkaka mmoja na kukaa karibu ya ojalaa.. Alitoa funguo ya gari lake na kuweka mezani kwa mbwembwe..
"Naitwa Daudi.. Nafanya kazi ofisi za uhamiaji.. Naishi Hapa mtaa wa bibi nyau... Mambo yako vipi dada sijui unaitwa nani.. Aliongea yule kaka..
" Naitwa ojala..
Ojala alijibu na kukaa kimya..
'Bei gani sasa kwa usiku wa leo mrembo au kuna mtu unamsuburi.?? Aliongea zaidi yule kaka...
Ojala alikaa kima kwa sekunde kadhaa akitafakari.. ,'inamaana hawa watu wanaona kila mwanamke ni malaya jamani.. Mbona dunia inaenda vibaya hivi.. Ngoja nianze nae kwa leo.. Aliwaza ojala
"Kwani wewe unataka unipe shingapi.?? Ojala aliuliza..
" ntakupa elfu ishiri na tano... Aliongea jamaa. 'Poa usijalia.. Namaliza kula tutoke.. Ojala aliongea na kula upesi..
Kwa haraka waliongozana hadi lodge kwakutumia gari la yule jamaa na kuchukua chumba.
Ojala hakuwaza kabisa kwasababu ya nguvu alizo nazo za kijini.. Waliingia na kukaa kitandani ..
"Lipia kwanza kaka.. Weka hela mezani hapo ndio mengine yafuate.. Ojala aliongea huku anavua nguo zake.. Yule kaka alikuwa yupo kasi sana alishavua nguo na kuweka pesa mezani alianza kumpapasa ojala taratibu... " inamaana hatuogi baby... Ojala aliongea...
Unataka tukaoge.?? Utaniogesha mpenzi.?? Aliongea yule kaka..
Unataka kuogeshwa.??
Ndio mke wangu nataka kuogeshwa.
Basi ingia bafuni nakuja.. Fumba macho yako nitakuogesha hadi utakate sawa... Ukifumbua macho sikuogeshii... Aliongea ojala..
Jamaa aliingia bafuni na kuvua taulo kisha kufumba macho na kukusubiri wakumuogesha aje..
Sekunde kadhaa alisikia maji yamefunguliwa na kuanza kuogeshwa kwa kupakwa sabuni na kusuguliwa tatibu... Jamaa lifurahia sana lakini alishaangaa anapapasa haoni mtu mule bafuni lakini mikono tu inamuogesha...
Jamaa aliogopa na kufumbua macho.. Ojala alicheka sana akiwa kitandani na kuanza kuirudisha mikono yake ambayo alikuwa ameinyoosha hadi kule bafuni..
Yule kaka alikuwa tayari yupo chini kazimia na alikuwa hata haelewi nini kinaendelea...
"Mjinga ww. Ojala aliongea na kupotea kisha kwenda kutokea kwenye lodge yake..
Alioga zake na kulala.. Kesho yake mapema alijiandaa ili aendele nyumbani kwa Hajraa..
***
***
Asubuhi na mapema niliamka na kumwandaa mwanangu.. Nilimtoa na kumpakia kwenye gari lao la shule kisha mimi nikawa narudi nyumbani kuendelea na majuku yangu mengine. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Cyprian kwanini anikimbie pamoja na mimi kumlea miaka yote hiyo na kumsomesha shule za gharama lakini leo hii ananichukia..
Nilikuwa nawaza sana huku narudi nyumbani..
Kabla sijafika nyumbani nilisikia nimeitwa " Hajraa.... Ilikuwa ni sauti ya kike.. Niligeuka na kukutana na Ojala uso kwa uso..
Nilicheka sana na kumkumbatia rafikiangu.. Tuliongozana hadi nyumbani na kukaa kuanza kupiga story mbili tatu...
"Shost mafunzo yamekuingia eti naona umeridhika sana.. Niliongea na kumtazama ojala..
Hamna mamy.. Tumepigika kweli huwezi amini.. Hapa kila mahali inauma.. Na vile juzi kulikuwa na tuzo ya heshima kwa mfanyakazi mmoja wa zamani sana wa taasisi yetu hii...
Nilisikia wasifu wake pale walisema aliwahi kuwa mkuu wa mkoa huku Tanzania.. Anaitwa Rwnatus...
Aliongea ojala huku ananitazama machoni...
" khaa.. Wewe ojala.. Unamsemea renatus yupi.???
Ni mzee fulani sio mnene wala sio mwembamba ila tu ni mchapakazi sana na mpole sio mwongeaji hata kidogo.
"Nilianza kuogopa sana na kutoa simu yangu mfukoni na kuanza kutafuta picha za renatu...
'Hembu angalia hii picha ojala.. Ni huyu.???
" Ndio shosti ni huyo huyo mzee.. Ni afisa wa usalama.. Kumbe unamjua.. Au uliwahi fanya nae kazi shosti.??
Aliuliza ojala...
Uuuhhhhh.. Nilishusha pumzi na kuingia ndani kwangu.. Inamaana huyu mzee ni askari alafu kaua watu kiasi kile na ameharibu wengine kwa kuwalawiti.. Kwanini jamani huu umoja wa mataifa unanitesa mimi.. Kwahiyo mkuu alikuwa anajua mtu ninae mtafuta ni huyu lakini alinificha.. Kuna njama gani ndani ya hili suala jamani.. Niliwaza sana huku nalia...
MWISHO WA SEASON ONE
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment