HATMA YA NYOTA WA ZAMANI WA YANGA IPO KWA MROMANIA WA AZAM FC
Ngoma ambaye alisajiliwa na Azam FC, msimu wa 2018/19 akitokea Yanga kwa sasa kandarasi yake imebaki miezi miwili ili kumeguka.
Mtendaji mkuu wa klabu hiyo Abdulkarim Amin amesema mwenye maamuzi juu ya hatma ya Ngoma ni Kocha Mkuu, Cioaba.
"Mkataba wake unakaribia kuisha ila kuhusu kumuongezea ama kutomuongezea hilo lipo mkononi mwa Kocha Mkuu na benchi la ufundi yeye anajua aina ya wachezaji ambao anawahitaji," amesema.
Ngoma msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara ametupia mabao mawili kati ya 37 huku Azam FC ikiwa nafasi ya pili na pointi zake 54 kibindoni.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment