HUYU NDIYE AJIBU WA SIMBA TOFAUTI YAKE NA YULE WA YANGA
Ibrahim Ajibu, kiungo huyu mshambuliaji wa Simba alikuwa na wakati mzuri alipokuwa ndani ya Yanga msimu wa 2018/19 tofauti yake na yule wa Yanga ambaye alikuwa anapewa nafasi kikosi cha kwanza.
Usajili wake ulitikisa Bongo kutokana na dili lake la kujiunga TP Mazembe kuja wakati wa usajili ila danadana zikawa nyingi akaibukia Simba.
Wakati akiwa Yanga alitupia mabao sita na alikuwa ni namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho alitoa 17.
Mambo yamekuwa magumu kwa sasa ndani ya Simba amecheza mechi 16 kati ya 26 na ametumia dakika 948 ana pasi nne za mwisho na bao moja alililowafunga Polisi Tanzania, Uwanja wa Taifa.
Leave Comments
Post a Comment