Jiulize, nini kimemfanya atamani kukurudia?
shule ya primary uliyosoma,hata ipambwe vipi huwezi kuacha kusoma chuo ukarudi primary.
Hakuna urafiki mzuri wa mtu na mpenz wake wa zamani (EX), sikuzote huwezi ukawa na manufaa yaliyo bora.
Kwanza jiulize, ni nini kilifanya mkaachana? Na nini kimemfanya atamani kukurudia sasa? Na una uhakika gani sababu iliyofanya mgombane na kuachana haitojirudia?
Kuna mwingine anasema amebadilika sasa, acha nikwambie kitu, maji ya moto asili yake ni baridi, na kurudi kwenye asili yake ni rahisi sana, labda tu uweze kuyatumia mapema.
Jiulize wewe utatumiwa mapema kwenye njia ipi? Kwa namna gani?
Tuache ule u Thomaso ngoja tuone, aisee ni bora ukashuka hapo ulipo na upande basi lingine, kuliko ung’ang’anie kupanda hilo hilo gari,na kumbe ni bovu na likuharibikie njiani hata nusu ya safari hujafika.
Na nyie mlio kwenye ndoa acheni kujidanganya na kutafuta nyumba ndogo, tambua hakuna jambo zuri bila changamoto,hvy upitapo kwenye changamoto,suluhisho kuu ni anguka miguuni pa Mungu hakika atakushika mkono na kukuonyesha njia ya kupita.

NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Leave Comments
Post a Comment