KWENU WADADA MSHAWISHI MUMEO KILA SIKU
Siku za mwanzo za uhusiano wa ndoa zetu, mambo huwa motomoto... 🍇Tunaposonga mbele zaidi, mazoea hayo hubadilika, hususan kama hakuna utaratibu wa kuyaamsha... Sasa ni namna gani unavyoweza kuendelea kumshawishi mumeo na kuufanya moto wa mahabba uendelee kuwaka ndani ya ndoa yenu...? ._⬇
_
1. Tabasamu la kudumu, tabasamu la kila siku... 🍇 Anaporudi nyumbani mpokee kwa tabasamu na umuulize kuhusu mihangaiko yake ya siku hiyo... mpe pole na umkumbatie hata kwa dakika nzima...mpaka ajiulize una nini...itaonesha ni jinsi gani umemmiss na kuamsha upya hisia za upendo juu yako.
_ 2. Daima mbusu, mbusu kila siku kwa mahabba, na lifanye hilo kuwa sehemu ya ndoa yako... _
3. Mtumie meseji za Mahabba... "Ninakupenda sana mfalme wa moyo wangu", "ninakutakia siku Maridhawa"... Katika kufanya hivyo uruhusu moyo wako uteme lulu za maneno ghali kutoka sakafu ya moyo... _
4. Ukiweza jitahidi sana kula pamoja nae, na lifanye jambo hili kuwa jambo adhimu la ndoa yenu...hata kama anachelewa kidogo...basi wewe kula kidogo kupunguza njaa...akirudi jipakulie na wewe tena mle wote.
_
5. Kuwa Maridhawa Mbele yake, jipambe kwa ajili yake, hata kama mkiwa hamfanyi chochote... Jirembe khaswaa, lifanye kuwa jambo endelevu katika kipindi chote cha uhai wako... _
6. Kutembea mkiwa mmeshikana mikono ni jambo muhimu sana... Daima mfanye ahisi kuwa wewe ni sahibu wake, badala ya kuwa inspekta wake... _
7. Jambo muhimu sana ambalo hutakiwi kulisahau daima, ni kumpikia chakula anachokipenda... 🍇Kama hujui kupika ulizia muongozo wa mapishi kutoka hata hapa au youtube kila aina ya mapishi yanapatikana.. Chakula hicho sio tu kwamba kinaenda tumboni, bali huelekea moyoni pia... _
Upendo wowote unahitaji kujitoa mhanga (sacrifice), tena kwa dhati, sio kwa majaribio... Hakuna maisha mabaya kwenye mahusiano kama kuishi kwa mazoea...Yaani ili mradi amerudi na mmekula basii...Wengine mkiongea basi pale mnaposalimiana tuh ndo imetoka. Matatizo ya namna hyo yanatatulika kabisa wali wangu.
.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Leave Comments
Post a Comment