MASOKO YA MADINI SINGIDA YALETA MAPINDUZI M
Wachimbaji wadogo wa madini wakiendelea na shughuli za uchenjuaji wa madini katika machimbo ya dhahabu ya Sekenke Wilayani Iramba Mkoani Singida tarehe 17 Aprili, 2020.

Mkaguzi wa Migodi katika machimbo ya dhahabu yanayomilikiwa na Chama chaUshirika wa Wachimbaji Wadogo wa Madini Kisonga-Shelui (UWAWAKISHE), wilayaniIramba mkoani Singida, Mohammed Salum akielezea manufaa ya masoko ya madiniyaliyoanzishwa mkoani Singida kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika wa Wachimbaji Wadogo wa Madini Kisonga naShelui (UWAWAKISHE), Masumbuko Jumanne (kushoto) akielezea changamotowanazokutana nazo kwenye biashara ya madini kwa waandishi wa habari (hawapopichani kwenye ziara hiyo.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo (kushoto) pamoja nawachimbaji wa madini akielekea kwenye machimbo ya dhahabu ya Sekenke WilayaniIramba Mkoani Singida tarehe 17 Aprili, 2020.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo akinawa mikonokabla ya kuingia katika machimbo ya dhahabu ya Sekenke Wilayani Iramba MkoaniSingida tarehe 17 Aprili, 2020.
……………………………………………………………………………………………………
Makusanyo yafikia shilingi bilioni 3.243 sawa na asilimia 216.2
Wachimbaji wa madini waipongeza Serikali.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mjiolojia Chone Malembo amesema kuwa kuanzishwa kwa masoko ya madini katika mkoa wa Singida kumeleta mapinduzi makubwa kwenye uchumi ikiwa ni pamoja na makusanyo ya shilingi bilioni 3.243 ambayo ni sawa na asilimia 216.2 kwa mwaka wa fedha 2019-2020 ambao haujamalizika.
Mjiolojia Malembo aliyasema hayo tarehe 17 Aprili, 2020 kwenye ziara ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Tume ya Madini na waandishi wa madini katika mkoa huo yenye lengo la kuangazia mafanikio ya Sekta ya Madini katika mkoa wa Singida.
Malembo alifafanua kuwa, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019 – 2020 ofisi yakeilipangiwa lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.5 na kuongeza kuwa hadikufikia katika kipindi cha mwezi Machi mwaka huu, Ofisi yake ilikusanya kiasi chashilingi bilioni 3.243 sawa na asilimia 216.2 na kufanikiwa kupewa cheti cha pongezikutoka kwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini .
Alisema siri ya makusanyo ni pamoja na usimamizi mzuri kwenye masoko mawili yamadini yaliyoanzishwa katika maeneo ya Shelui Wilayani Iramba na Manispaa yaSingida mkoani Singida.
Akielezea hali ya ukusanyaji wa maduhuli kabla ya kuanzishwa kwa masoko husika Malembo alisema kuwa, katika mwaka wa fedha 2018-2019, ofisi yake ilipangiwa lengola kukusanya shilingi bilioni moja na kufanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni804.5.
Katika hatua nyingine, Malembo alishukuru kwa ushirikiano aliokuwa akiupata kutokakatika vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa, ofisi yake imekuwaikishirikiana kwa karibu na vyombo vya ulinzi na usalama na Taasisi nyingine za Serikalichini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Aliongeza kuwa mafanikio yaliyopatikana ni mazao ya uwepo wa uwazi, uwajibikaji naushirikiano thabiti wa Serikali kwa ujumla wake na kwa msaada mkubwa wa viongoziwa Wilaya na Halmashauri zote.
Akizungumzia namna ofisi yake inavyodhibiti utoroshaji wa madini alisema kuwa mkoaumeanzisha Kikosi Kazi Madini (KKM) ambacho kina wajumbe kutoka taasisi muhimuikiwemo baadhi ya taasisi zinazounda kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Alisisitiza kuwa kikosi kazi hukutana mara kwa mara ili kupitia taarifa na kujadili nakisha kutengeneza mikakati madhubuti inayosaidia udhibiti wa utoroshaji wa madini naukwepaji wa kulipa tozo za Serikali.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Iramba Emmanuel Luhahula akielezea mchango wa sekta yamadini katika wilaya yake, mbali na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Magufuli kwa usimamizi mzuri wa sekta ya madini ikiwa ni pamojana uanzishwaji wa masoko ya madini nchini, alisema mapato katika halmashauri yaIramba yameongezeka hadi shilingi milioni 99 tofauti na awali ambapo walikuwawakipata shilingi 500,000 kwa mwaka.
Aliongeza kuwa, uanzishwaji wa masoko ya madini umepunguza kwa kiasi kikubwa chautoroshaji wa madini kwa kuwa wachimbaji wa madini wamekuwa na mwamko mkubwawa kuyatumia masoko ya madini yaliyoanzishwa na kupata faida huku Serikali ikipatakodi mbalimbali.
Luhahula alitaja mafanikio mengine ya masoko ya madini yaliyoanzishwa ikiwa nipamoja na kuongezeka kwa mzunguko wa fedha katika wilaya ya Iramba na kuwatakawachimbaji kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria na kanuni za madini hukuwakijikinga na ugonjwa wa korona.
Akielezea mikakati ya wilaya yake kwenye udhibiti wa ugonjwa wa korona hususankwenye maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa madini Lahahula alisema, Ofisi yakekwa kushirikiana na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida wameshaanzakutoa elimu kwa wachimbaji wa madini na kuhakikisha wachimbaji wanaendeshashughuli zao kwa tahadhari ikiwa ni pamoja na kuwa na maji tiririka na vitakasa mikono.
Wakati huohuo wakizungumza kwa nyakati mbalimbali wachimbaji wa madini katikamachimbo ya dhahabu ya Sekenke mbali na kuipongeza Serikali kwa kuwapatiamaeneo ya uchimbaji wa madini na uanzishwaji wa masoko ya madini walisema kuwamasoko ya madini yameleta mapinduzi makubwa.
Akizungumza kwa niamba ya wachimbaji wa madini, Mwenyekiti wa Chama chaUshirika wa Wachimbaji Wadogo wa Madini Kisonga na Shelui (UWAWAKISHE),Masumbuko Jumanne alisema kuwa kuanzishwa kwa masoko ya madini kumeletamanufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuuza madini yao kwa kufuata bei elekezi zinazotolewa na Serikali kila mwezi na kupata faida na usalama kwenye biashara yamadini.
Previous article
Leave Comments
Post a Comment