MBELGIJI WA YANGA YAMKUTA HUKO, AKWAMA KUTUA BONGO MARA MBILI
LUC Eymael, Koc
ha Mkuu wa Yanga amekwama mara ya pili kurejea Bongo kutokana na Serikali kuzuia ndege kupaa ili kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona.
Eymael alikwea pipa mpaka nchini kwao Ubelgiji ili akapate mapumziko mafupi pamoja na mpango wake wa kuoa baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
Kocha huyo awali alipanga kurejea Bongo Jumamosi mambo yakawa magumu akajipa muda mambo yakakwama tena.
"Nimeshindwa kurejea Bongo kutokana na Uwanja wa ndege wa huku Ubelgiji kufungwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona, hali ikiwa shwari nitarejea kuungana na timu," amesema.
Previous article
Leave Comments
Post a Comment