Ads Right Header

Buy template blogger

MNATA: YANGA KUNA USHINDANI WA NAMBA

MNATA: YANGA KUNA USHINDANI WA NAMBA
METACHA Mnata, mlinda mlango namba mbili wa Yanga amesema kuwa ndani ya kikosi hicho kuna ushindani mkubwa wa namba jambo linalomfanya azidi kupambana kuwa bora.

Ndani ya Yanga kuna makipa watatu ambao ni Farouk Shikalo, Ramadhan Kabwili pamoja na Mnata mwenyewe.

"Ushindani wa namba ni mkubwa kwani kila mmoja ana kitu cha kipekee, jambo hilo linanifanya nami nipambane kuwa bora kwani napenda kufikia malengo niliyojiwekea.

"Shikalo amekuwa akinipa darasa hasa kwa vile vitu ambavyo anavifanya tofauti na mimi, Kabwili pia nimekuwa nikimuona mazoezini akifanya kazi yake kwa umakini mwisho wa siku wote ni familia moja," amesema.


Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4