MTIBWA SUGAR YAWATUMA WACHEZAJI KUWA MABALOZI KWA JAMII
UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa umewatuma wachezaji wao wa Mtibwa Sugar kuwa mabalozi kwenye jamii kuhusu janga la Virusi vya Corona.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema kuwa wamewambia wachezaji wao wawe makini na wahakikishe wanachukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
"Tupo kwenye wakati mgumu kwa sasa ila imani yetu ni kwama hili litapita pia na maisha yataendelea, ila kikubwa ambacho tumewaambia wachezaji wetu wahakikishe wanakuwa mabalozi katika jamii katika kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
"Wachezaji wapo nyumbani na wameambiwa wawe makini katika kazi wanayofanya na wawe makini kwani Virusi vipo na vinaua hivyo wanapaswa wawe mabalozi katika hili bila kusahau dua," amesema.
Leave Comments
Post a Comment