Story ;SANGARE SEHEMU YA 31

Salu amekufa ,amefumaniwa na mke wa mtu amekatwa katwa na mapanga .
Watu kwenye msiba walivyomwona sangare ,kila mtu alianza kukimbia huku wengine wakikamata mikoba yao na kusema
Namba tatu karudi huyu si sangare tumekwishaa
Sangare akashangaa watu wanamwogopa na kukimbia
Minal ikabidi asimame na kuuliza kwa nini mbona watu wanakimbia "sangare kwani wanaogopa nini?,au wakuogopa wewe mbona wanataja namba tatu ,halafu namba tatu hio kama vile naikumbuka na mimi.
Sangare ikabidi aulize na wewe namba tatu unaijua ?,hebu niambie ni kitu gani hicho?,kabla minal hajamwelezea ndipo walisikia kilio cha mariamu akilia huku akisema " amka sasa kwanini umefariki bila kuona damu yako uliye iacha ,salu amka ,uweze kumjibu mwanao hakika anakuulizia ,
Tamaa zangu na shida ndio matokeo ya sangare amka umwone mwanao hakika amekua japo ameishi maisha ya tabu ,
"Hapo ndipo sangare akamwambia minal hebu twendeni mbona mama analia amepatwa na kitu gani ,mama aliweza kujipenyeza hadi mbele ndipo aliona jeneza la bwana salu likiwa mbele anaagwa ili akazikwe ,
Sangare akamuuliza mama huyu mtu aliyefariki unamjua?,mama alimshika mwanae na kuongea mbele ya umati ," sangare mwanangu hakika tumechelewa huyu ndie baba yako ,leo hii unamwona akiwa kwenye sanduku na ndio safari yake ya mwisho,huyu salu ndio alinipa ujauzito kisha nikapata na kazi kwenye baa yake ambae alikuwa anacheo cha umeneja ,
Sangare kuambiwa vile alifungua jeneza na kuona sura ya baba yake ,hakika alikuwa anafanana nae ,sangare alilia na kumwambia "baba kaapumzike mahali pema pepon sina cha kusema ila sura yako nimeiona na nimeikumbuka.
Pale pale
sangare alivuta kumbu kumbu kipind cha nyuma ,baada ya kuona maisha dar yamekuwa magumu ,aliamua kutafuta nauli aondoke kwenye jiji la dar es salaam ili kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.
Alipita maeneo ya banana ukonga kwenye vichochoro ,alikutana na bwana salu akiwa amesimama bila shaka alikuwa anamsubiri mtu.
Alimkaba roba na kumwekea misumari yenye ncha kali usoni na kumwambia " tulia hivyo hivyo ulivyo navyo ni mali yangu,sangare alizamisha mkono wake mfukoni alitoa burungutu la hela ,pamoja na simu ,
Alimtizama na kuona salum anatetemeka alimwambia "kawaida yangu nikikaba naua ila kwa sasa siui wala sichukui pesa zako kukukomoa ninachokitaka ndio nitakachokichukua.
Sangare alichomoa elfu 25 tu kisha pesa zingine akamtupia pamoja na simu yake na kumwambia haya potea,
Bwana salu mwenyewe alishangaa huyu ni kibaka wa namna gani amenikuta na zaidi ya laki saba yeye amechukue pesa kidogo na zingine kuzirudisha ,
Alimwacha hapo na wala bwana salu hakupiga kelele za mwizi aliamua kunyamaza na kuondoka
Leo ndio sangare amegundua alikuwa baba yake,sangare alitoa shukrani zake za mwisho na kumwambia baba " pesa zako nilizokukaba miaka ya nyuma ndio zilinipeleka singida na kukutana na mama yangu ,lait isingekuwa wewe huenda nisingemjua na mama yangu pumzika kwa aman,
Sangare akapangusa machozi yake.
Watu kwenye msiba walishangaa na kujiuliza huyu si namba tatu ndio mwenyewe ila sasa kabadilika ona kanyoa rasta zake halafu kwa sasa msafi.
Wakati watu wakijadili kuhusu namba tatu alisikia na kujisemea mbona kama vile na mimi namba tatu namjua,ila akapotezea ,
Sangare alifanikiwa kumzika baba yake walivyomaliza familia ya bwana salu ilikaa kikao kisha wakagawa mali kwa watoto wake watatu.
Walimkataa sangare na kusema hawamtambui sangare wala hakuwa na shida na pesa zao maana anayopesa nyingi ya madini bilion 14.5.
Sangare kwenye kikao aliwaambia sawa kama mimi hamnitambui ila mimi nitawatambua sababu pasina kuwa na baba wala nisingelizaliwa ,hata baba alifanya makosa ,ila si ya kumfanya nisimsamehe na nisimjue
Wote watoto wa baba mmoja ,nitawapenda na kwasasa nawapa milion kumi kama pole na huu ni mwanzo ,niwaambie ninyi msinitambue kama mmoja wa familia ya bwana salu ,ila mimi nitawatambua kuwa nimezaliwa na bwana salu na nina ndugu zangu watatu.
Sangare aliweka milion kumi kisha akamshika mkono mama yake pamoja na minal ,alimwinua na rabeka ili waondoke.
Walivyoondoka watoto wa marehem walianza kuzungumza inamana sangare alivyokuwa mwizi anajiita namba tatu ,leo kawa na pesa na amesema atazidi kutufahamu ,hii inawezekana kweli au kaiba,
Walijadili na kuona si vyema kumkataa sababu anayo hela basi ni ndugu yetu ,watoto wakaamua kukubali sababu. Sangare anayo pesa.
Minal aliwachukua moja kwa moja sangare hadi anakofanyia kazi mama yake wakati huo ishatimia saa kumi jion ,walikuta mama yupo kwenye kabanda chake ni mama nt'ilie ,alikuta ndio anaweka mchuzi wa maharage kwenye ukoko uliyobaki kwenye safuria,ili mama apate kupoza njaa maana tayari chakula ashamaliza "
Mara akasikia mamaaa nimerudiiiii ,mama akainua kichwa huyo ni nani alishangaa kumwona binti yake ,mama aliinuka upesi na kumkumbatia mwanae huku akitiririsha machozi
Mwanangu minal umerudi kipindi hichi ,kwanini umerudi angali mimi nina maisha magumu?,minal kwanini?
Minal ilibidi amuulize mama kunashida gani?
Mama kwanza akapakua ukoko alio utia maharage na kumwambia "mwanangu hichi ndio chakula kilicho baki,na pesa zote nimelipia chumba ,hapa sina hata senti ntano na bado nadaiwa pesa niliyokopa mchele ,maharage ,
Kwanza minal alicheka na kumkumbatia mama yake kisha akamwambia " mama ona kwanza mkufu nilio nao yaani huu nikisema niuze bei yake si chini ya milion kumi,huu mkufu ni wa madini matupu halafu mama kabla sijaendelea nimekuja na wageni ,huyu hapa mama mke wangu ,huyu hapa anaitwa sangare ni mchumba wangu na huyu anaitwa rabeka ni rafiki yangu.
Hapo ndipo mama minal alivyogeuka aliomba aridhi ipasuke ajifiche ndani,hasa alivyomwona sangare mama hakusubiri alianza kuporomosha matusi
Mwanangu huyu mchumba gani mwanaharamu mkubwa ndio sababu ya kukufanya wewe uache shule alinikabaga na kunipora pesa zako za ada huyu si sangare mwizi wa mtaa kila mtu anamjua
Kitendo cha mama minal kusema sangare ndiye aliyemkaba mama yake akampora hapo ndipo minal akakumbuka "
"Ni kweli siku hio walikuwa wanaenda shule na mama yake ,ndipo sangare akiwa amefunika uso na kitambaa chake kimeandikwa namba 3, aliukwapua mkoba wa mama yake kisha akakimbia ,minal alijaribu kumkimbiza mwizi aliyeiba mkoba wa mama yake
Alijitahidi kukimbizana nae lakin sangare aliruka ukuta na kutokea upande wa pili,minal hakufanikiwa kumkamata na ndio siku ambayo minal alikuwa anaenda kuandikishwa kidato cha kwanza,
Ilibidi mama yake aende shule kuwaeleza walimu kama watamkubalia mwane aanze masomo ili atafute ada taratibu
Lakin walimu waligoma kabisa na kumrudisha nyumbani hapo ndipo minal hakuendelea na masomo.
Mama minal alianza kumpiga sangare kwa mikono mara sangare alimshika mikono yote miwili " alianza kumwambia "mama kweli lengo la kisomo ni kuelimika na kupata uzoefu na mambo kadha wa kaza ,pia elimu ni ujira ambaye kila mwanadamu anautegemea ,asome ili awe na maisha mazuri
Basi lait mwanako angesoma leo hii angekuwa kidato cha tano ,leo mwanao hajasoma na anamiliki bilio kadhaa za pesa ,bora angesoma afeli kidato cha nne au bora hakusoma.
Mama alivyoambiwa vile alikumbuka ,mwanae hakuwahi kuwa na akili nzuri ya ufaulu wa kwenye masomo ila mtoto wake alikuwa na elimu nzuri ya maisha ,na hasa mama alivyosomeaga unesi miaka mingi na kuja kuzunguka kila kona akiomba kazi ,mwisho wa siku alikuja kuambiwa cheti chake ni cha kizamani inabidi arudi chuo cha unesi miaka mitatu ili apate cheti kizuri hapo ndipo alichoka hakuwa na kipato ,lakin alianza kufanya vibarua mtaani hadi alivyoolewa.
Mama alivyokumbuka vile ,alimwambia sangare samahani,kweli uko sahihi ,kisha akageuza macho kwa mama yake na sangare hapo ndipo alichoka.
Alijikuta akimrukia na kumkumbatia kwa nguvu huku ameita mariamuuuuuuuu
Minal na sangare wakashangaa na kuulizana inamaana wanafahamiana?,hakika ilikuwa furaha kubwa kwa mama minal alianza kuzungumza
Mariamu wewe ndiye tuliyeanzisha huu mgahawa na wewe ,hili banda nilishirikiana kujenga na wewe ,hakika ulikuwa mpishi mzuri wa chapati.
Ilibidi wakae kwenye viti ili awasimulie walikutana vipi na mariamu.
"Miaka ishirin sasa imekwisha pita ,baada ya mariamu kung'ata mwanae mgongoni na kumtelekeza alikimbia kutoka vingunguti hadi buguruni na alikutana na mama minal kipindi hicho alikuwa na ujauzito.
Alimkuta anawaza kuhusu kulea mimba baada ya mme wake kusafiri na kwenda kongo,wakati anatafakari asubuhi na mapema alimwona mariamu akikimbia huku akimwona mwenye wasi wasi ,alimwita ,kwa ishara ya mkono ,mariamu hakusita na kumfuata ,alivyofika alimuuliza kulikoni mbona unakimbia?
" mariamu alidanganya hapa nilipo sijui nipo wapi nilichukuliwa kutoka singida sijitambui na kuletwa dar ,na mwanaume amakuja na kuniingilia ki mwili kisha akanitelekeza sipajui dada yangu hapa niko wapi?
Mama minal alimwambia tayari upo dar nikuombe kitu kimoja hebu kaa tulia ukijifanya unakimbia kimbia utakutana na mambo mazito karibu ingia ndani wewe ni mwanamke mwenzangu leo kwangu kesho kwako.
Hapo ndipo alipomkaribisha mariamu ,walizungumza mambo mengi na kumshauri atulie hadi watakapo pata pesa basi atampa arudi nyumbani mariamu alikuwa msiri hakusema kama amekimbia mtoto ,
Na kila maziwa yake yakijaa ,anakimbilia chooni baasi anaenda anayakamua yakirudi sawa anarudi ndani
Hapo ndipo walivyoanzisha urafiki , na hatimae waliamu kufungua banda la kuuza chakula ,na walikuwa wanawateja sana
Mama minal alivyokaribia kujifungua ndipo walifunga banda ama mgahawa wao kwa muda ndipo mariamu aliamua kurudi singinda.
"Hivyo divyo ilivyokuwa alimkumbatia tena na kumwambia " karibuu dar es salaam kwa mara nyingine pia karibu kwenye mgahawa wako,na sasa sina kipingamizi kama mwanangu ameridhia kuolewa na sangare sitojali kama ni mwizi ama jambazi .
Hebu niambie mariamu hili dume lako sangare umemzaa lini ?maana ulivyokuja kwangu ulisema hujawahi kuzaa.
Mariamu akacheka na kumwambia "ulivyoniona nakimbia ndio nilikuwa nimemtelekeza jaman mwanangu.
Wakiwa wanapiga story bara barani waliona watu wamejikusanya huku wakishangaa jambo ,sauti ilisikika ya mtu akilia
" nimepata sasa ukweli kumbe mwanangu selemani hakuuliwa na mjukuu wangu ,nilimfukuza mjukuu wangu niliyemlea kwa tabu sana ,nilihangaika nae kwa shida ,leo hii sijui kama yupo salama
Nimezunguka kila makaburi yote yaliyoko dar hii sijaona hata jina lake
Basi watu wanazidi kuniandama mimi ni mchawi nawanga mchana kweupe kwenye makaburi ,jaman siwangi namtafuta mjukuu wangu,
"Sauti zilisikika " jamani huyu bibi mchawi kabisa ,amekuja jana kwangu alianza kuchimba shimo kwenye pembe ya nyumba yangu anasema anamtafuta mjukuu wake auliwe tu huyu bibi mchawi
Watu kusikia mchawi ,vijana walibeba zana za kuua ,mipini ya jembe ,nondo mbao ,walimzunguka bibi ili wamuue
Kuna kijana mmoja alinyanyua shoka ili apasue kichwa cha bibi
Kisha akashusha kwa kwa nguvu ,sauti ya shoka likazama ilisikika kooooo,bibi tuliii akanyoosha na miguuu
Je nini kitaendelea?
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment