UINGEREZA KUFANYA MAJARIBIO YA CHANJO YA CORONA WIKI HII
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
CHANJO dhidi ya virusi vya Corona (Covid-19) iliyochakatwa katika Chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza itafanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi wiki hii, katibu wa Afya nchini humo Matt Hancock ameeleza.
Kwa mujibu wa DailyMail imeelezwa kuwa Hancock amesema kuwa chanjo itakua ni njia sahihi ya Kupambana na virusi hivyo.
Chanjo hiyo itafanyiwa majaribio kwa watu wapatao 510 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 55 huku ikielezwa kuwa watafiti hao wanaimani ya kuwapa watu ulinzi dhidi ya Covid -19.
Aidha imeelezwa kuwa Serikali nchini humo itatoa fedha za ziada zipatazo Euro milioni 20 kwa wanasayansi kutoka ili kuwezesha majaribio yao pamoja na Euro milioni 22.5 kwa chuo cha Imperial London.
Chanjo hiyo iliyochakatwa na chuo kikuu cha Oxford inajulikana kwa jina la ChAdOx1 nCoV-19 na itafanyiwa majaribio kwa watu 510 kutoka makundi 1,112 wenye umri kati ya miaka 18 hadi 55 ambao walijitolea kutoka London, Bristol, Oxford na Southampton.
Imeelezwa kuwa Uingereza inakua nchi ya kwanza kutengeneza na kufanya majaribio ya chanjo hiyo Jambo ambalo linaleta matumaini ya watu kutoka katika karantini na kuidhibiti Covid -19.
Pia Hancock amesema kuwa licha ya ugonjwa huo kuwa mpya kila jitihada zitafanyika ambapo hadi sasa wanasayansi kutoka Oxford na Imperial wameongoza katika zoezi hilo na Serikali itafanya kila liwezekanalo katika kushiriki na kufanikisha hilo.
Hadi Sasa watu walioathirika na virusi hivyo nchini Uingereza imefikia 125,000 pamoja na vifo 17,339 jambo ambalo limewasukuma Uingereza kupambana janga hilo ambalo linatikisa dunia.
Leave Comments
Post a Comment