USHAURI | MUME HATAKI DADA AINGIE CHUMBANI
Anapenda umwinyi sana, mimi nafanya kazi nayeye anafanya kazi, nyumbani tuna binti wa kazi, tukirudi wote tunakua tumechoka, lakini anataka bado mimi nifanye kazi za ndani. Kwenye chakula anakula chakula cha binti wa kazi, ishu inakuja kwenye kufua na usafi wa chumbani, mimi sio kama ni mvivu lakini kama mtu una binti wa kazi kwanini asifanye kazi za ndani wakati namlipa.
Sasa tatizo nikuwa, mume wangu hataki binti wa kazi kuingia chumbani kwetu, madai yake nikuwa yeye ni mtu mizima na binti wa kazi ni kama mtoto wake hivyo mazoea ya kuingia chumbani hataki. Kusema kweli tunagombana kwa vitu vidogo vidogo, mfano kazi zake nyingi anafanyia chumbani, kama binti wa kazi labda asubuhi wakati anatandika kitanda na kufanya usafi akiweka vitu vibaya basi mume wangua kirudi akaulizia kitu chake anataka ni mjibu mimi.
Kama ni kimuita binti wa kazi na kumuuliza labda kitu flani umeweka wapi basi mume wangu ataongea mpaka basi. Atalalamika na kusema kuwa nafanya makusudi kwakua namdharau lakini si kweli. Kaka mimi nafanya kazi, siwezi kufanya kazi za ndani pia, kufua mume wangu anafua mwenyewe kwani mimi nafuliwa na binti wa kazi ila yeye hataki na mimi namuachia anafua mwenyewe.
Sababu ya kuja kwako nikutaka kujua kama mimi nakosea au la? Hivi Kaka kama mwanamke anafanya kazi ni lazima kufanya na kazi za ndani wakati kuna binti wa kazi. Natana nijue kuna tofauti gani ya kitanda kutandikwa na binti wa kazi na mimi kutandika. Huoni kama ni mfumo dume kama wote tunafanya kazi kwanini mimi nifanye kila kitu, yeye hana shida na kwingine ugomvi wake mkubwa ni kwanini binti wa kazi anaingia chumbani kwetu?
Anataka afanye usafi kwingine lakini si chumbani na wala hataki nguo zake zifuliwe na binti wa kazi kwani anasema ni mtoto mdogo, naomba nisaidie hapo Kaka?
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Leave Comments
Post a Comment