VIFUAVIWILI:WATANIELEWA TU SIKU MOJA LICHA YA KUNIBEZA KWA SASA
BRUNO Tarimo ‘Vifuaviwili’ bondia wa ngumi za kulipwa ambaye ni bingwa wa International Super Feather Weight alioupata nchini Serbia kwa pointi mbele ya bondia Scheka Gurdijeljac raia wa Serbia amesema kuwa ameamua kuwa wale ambao hawatambua anachokifanya kwa sasa watamuelewa baadaye.
Kwa sasa Vifuaviwili anaishi nchini Serbia ambapo anaendelea kufanya mazoezi ndani ya nyumba baada ya Serikali kuzuia watu kutoka nje ili kujikinga na Virusi vya Corona huku akiendelea kupeperusha Bendera ya Taifa ya Tanzania.
Akizungumza na Saleh Jembe, Vifuaviwili amesema kuwa wengi wamekuwa hawaelewi kile ambacho anakifanya kutokana na kutopewa thamani kubwa licha ya kufanya kazi kubwa ila anaamini wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.
"Wengi wanabeza na kusahau kwamba nami nipo ninapeperusha Bendera ya Taifa ya Tanzania kwa sasa, wakati ukifika kila kitu kitakuwa sawa na nina amini wataelewa tu kikubwa tuendelee kumuomba Mungu ili kila kitu kiwe sawa," amesema.

Previous article
Leave Comments
Post a Comment