Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

BEKI ANAYEZICHANGA SIMBA NA YANGA AFICHUA SIRI YA KUTUSUA

BEKI ANAYEZICHANGA SIMBA NA YANGA AFICHUA SIRI YA KUTUSUA
BAKARI Mwamnyeto, beki chipukizi ndani ya Coastal Union iliyo chini ya Juma Mgunda amesema kuwa siri kubwa ya kiwango chake ni juhudi pamoja na nidhamu ndani na nje ya uwanja.

Mwamnyeto amekuwa bora ndani ya Coastal Union ambapo ikiwa imecheza mechi 28 imeruhusu kufungwa mabao 19.

"Kikubwa ni nidhamu nje ya uwanja na ndani ya uwanja ni mambo ambayo yananifanya ninakuwa katika ubora wangu muda wote kwani hakuna kinachowezekana ikiwa hautaweza kufuata ile miiko iliyowekwa," amesema.

Beki huyo inaelezwa kuwa anawindwa na Simba pamoja na Yanga ambao wanahitaji saini yake huku dau lake likitwaja kuwa ni milioni 100.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4