Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

KUTOSAFISHA MIUNDOMBINU CHANZO CHA MAFURIKO BUKOBA

KUTOSAFISHA MIUNDOMBINU CHANZO CHA MAFURIKO BUKOBA
Na Abdullatif  Yunus  Michuzi TV.
MVUA zinazoendelea kunyesha maeneo mengi nchini zimeendelea kuibua hisia na maswali kwa wengi, huku baadhi ya maeneo yakifurika Maji na kusababisha usumbufu kwa wakazi wa maeneo husika ikiwa ni sambamba na uharibifu wa Mali na miundo mbinu.

Hali kama hiyo inaonekana kujitokeza mara kwa mara katika viunga vya Manispaa ya Bukoba kufuatia kutosafishwa mara kwa mara baadhi ya mifereji, pamoja na mkondo wa Maji wa Mto Kanoni unaotirikia kuelekea Ziwa Victoria, ambapo Maji hayo hutiririka na taka nyingi ambazo husababisha kuziba kwa njia ya Maji hali ambayo hupelekea mafuriko.

Akizungumza kuhusu suala hilo la mafuriko Mmiliki wa Sky Motel na Mint Club za Bukoba Bwn. Muganyizi Zachwa  amedai kuwa Wananchi wanatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu mvua hizo zinazoendelea kunyesha na kuongeza kuwa mvua hizo hazifanyi Mkoani Kagera tu bali maeneo mengi Tanzania. 

Hata hivyo Zachwa ameongeza kuwa Mafuriki hayo  baada ya muda mfupi huwa yanatoweka baada ya taka kuondolewa licha ya kuwa Serikali pia inafanya utaratibu wa namna ya kuendelea kusafisha mifereji na chanzo hicho cha Maji ili yaweze kutiririka vizuri, ingawa Ziwa Victoria linaonekana Maji yake kuongezeka.

Katika hatua nyingine Zachwa amewataka wateja wanaofika Sky Motel kuendelea kujipatia huduma zao kama kawaida, kwani Maji yanayoingia katika Bustani hayana athari yoyote, na hukauka baada ya muda mfupi, huku akiwaomba wateja hao kutoyasikiliza maneno ya kizushi yanayosambazwa na baadhi ya wanahabari, na wale wasiopenda maendeleo lengo likiwa ni kuharibu biashara yake, na kuwa eneo la Sky linatosha kukaa bila Msongamano katika kuchukua tahadhari juu ya Ugonjwa wa CORONA.
Muonekano wa Daraja la Kanoni Hamugembe, ambapo Taka zinazojaa chini ya Daraja hilo husababisha Maji kutotiririka vizuri na kupelekea mafuriko.
Mmiliki wa Sky Motel Bwn. Muganyizi Zachwa Akiwaonesha wanahabari mkondo wa Maji wa Mto Kanoni unaopita jirani na Bustani ya Sky Motel, ukiwa umerejea katika hali ya kawaida baada ya Maji yaliyokuwa yamejaa kuondoka.
 Muonekano wa Garden ya  Sky Motel ambapo mafuriko husababisha Maji kujaa eneo hilo na kisha kuondoka.
 Wanaonekana baadhi ya Wateja wakiendelea kula maisha baada ya hali kurejea na Maji kuondoka katika Garden yao pendwa ya The Sky Motel.
Muonekano wa THE SKY MOTEL kiwanja maarufu cha kuoumzika Ndani ya manispaa ya Bukoba kama panavyoonekana upande wa Mbele.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4