Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MAMA WA KAMBO 28


Here Comes The Movie About Africa's Most Scandalous Love Story ...

Baada ya dakika 12 tayari walikuwa wamefika nyumbani kwa Dokta maeneo ya Isanga,ajabu walipofika mle ndani ya uzio walishangaa kuona jeneza ambalo alikuwepo Mama Linna linawaka moto mbaya zaidi ambulance haipo na hamna dalili kama kuna mtu ama watu wapo.
Haraka Dokta alichukua simu yake nakumpigia dereva ili aulize kulikoni tena maana jeneza limechomwa,sekunde kadhaa tangu apige simu ilipokelewa na dereva.
"Boss nipo nje hapa nakuona kata simu,"Aliongea na Dokta akakata simu nakugeuka nyuma kuangalia.
Kweli alipogeuka alimuona dereva anakuja na tayari ameshaingia ghetini.
"Vipi dereva umetokea huko na hili jeneza linawaka moto kulikoni,"Dokta alimuuliza dereva na ndipo akajibiwa kuwa asihofu kabisa ye ametoka kupaki gari hospital na mama Linna yupo ndani na Nesi,kuhusu jeneza wamechoma sababu wasingeweza kuliacha tu wakati kazi limemaliza.
"Wawoooo mmetumia akili sana,basi tuingie ndani tumalizane,"Aliongea Dokta nakuwapongeza kwa mbinu waliyofanya.
Basi waliingia ndani,mle ndani walimkuta Nesi akiwa na Mama Linna ambaye alikuwa hajitambui kabisa maana alichomwa sindano ya usingizi ambayo yamebaki masaa 4 ili azinduke.
"Jamani kazi imeenda vizuri kabisa na nawapongeza kwa kufanya vizuri pia kila mmoja nampa milioni2.5,"Aliongea Dokta nakuanza kuwapa pesa,baada ya nusu saa tayari kila mmoja alikuwa na mgao wake mkononi.
"Asante sana boss hakika tumefurahi sana na tunakuahidi kutunza siri hii,"Waliongea madereva wote wawili na manesi wote wawili baada ya kupewa pesa.
"Asante kwa kushukuru pia asante kwa kuniahidi kutunza siri hii pia niwahurusuru kila mmoja aendelee na shughuli zake,"Aliongea Dokta na wote wakainuka nakuondoka huku wakiwa na furaha kubwa sana.
Baada ya madereva na manesi kuondoka nyumbani kwake haraka alimpigia Mchungaji Petro nakumwambia yupo kwake hivyo afike mara waanze safari ya kwenda Dar Es Salaam ambako wanaenda kumpeleka mama Linna akaishi huko kwa muda wakati wanapanga wajue cha kufanya?.
Mchungaji Petro nae baada ya kupigiwa simu akaahidi kufika nyumbani kwa Dokta baada ya robo saa sababu hapakuwa mbali.

Wakati Dokta Magnus anamsubiri Mchungaji Petro alimpigia simu mkewe Sophia nakumwambia ile ishu ya Mama Linna kwa ufupi sana na mwisho akamaliza kwa kusema aandae mazingira tu huyo Mama Linna anakuja nae.
Mkewe Magnus alikuwa ni mwelewa mno na ile ishu ya Mama Linna licha tu ya kuambiwa kwa ufupi ye aliielewa vizuri kabisa,alimhurumia sana Mama Linna kiukweli.

Dokta nae baada kuongea na mkewe Sophia akaanza kujiandaa ili Mchungaji Petro akifika safari ianze mara moja ili mama Linna akashtukie Makambako au Iringa kabisa.

Robo saa aliyoahidi Mchungaji Petro iliwadia na kweli akawa amefika nakukuta Dokta amekaa kwenye sofa anamsubiri.
"Ashukuriwe Mungu kwa kumuokoa huyu mwanamke maana dah mi moyo ulikuwa unaenda mbio sana kule makaburini nikijua watu wanaweza gundua kinachoendelea,"Mchungaji Petro alimwambia Dokta.
"Haha haha nilijua tu ila tumshukuru Mungu mpango wetu umeenda vizuri,sasa tuanze safari ili tuwahi kufika Dar na kesho tugeuze,"Aliongea Dokta.
"Kabisa tumpakie kwenye gari safari ianze."
Bila kupoteza muda walimchukua mama Linna nakutoka nae nje kisha wakampakia kwenye gari siti ya katikati.
Wakati Mchungaji Petro anamuweka vizuri mama Linna pale kwenye siti Dokta alirudi kufunga mlango kisha akawasha gari na safari ikaanza.
"Mafuta yaliyopo humu Makambako tunafika hivyo hapa Mbeya hatuweki maana tunaweza shtukiwa,"Aliongea Dokta akikanyaga mafuta.
"Sawa sawa nakuaminia kanyaga mafuta,sindano siumechukua eeh ili akizinduka umchome tena,"Aliongea Mchungaji Petro nakuuliza.
"Ooh! Zana za kazi ndio zipo kwenye begi humo siwezi kusahau ndugu,"Alijibu Dokta na muda huo tayari walikuwa wanaitafuta Uyole.
Basi safari iliendelea huku wakipiga story za hapa na pale,sekunde,dakika,saa zikazidi kukatika hatimae  masaa manne yalitimia tangu waanze safari na tayari walikuwa mjini Mafinga.
"Naona anajitikisa vipi ndio anataka kuzinduka au,"Mchungaji aliuliza baada ya kuona Mama Linna anajitikisa.
"Ndio aisee anataka kuzinduka kwa nisimamishe gari nimdunge ya masaa sita ili akazindukie Dar,"Alijibu Dokta nakusimamisha gari pembezoni mwa barabara.
Alivyosimama wala hakupoteza muda alichukua bomba la sindano akafyonza dawa akamchoma.
"Hapa mpaka Dar Es Salaam sema namuonea huruma njaa tangu jana hajala,"Aliongea Dokta akianza kuendesha gari.
"Ooh! Sasa tutafanyaje itabidi avumilie tu maana tunamuokoa ye mwenyewe,"Alisema Mchungaji Petro akimshikilia vizuri Mama Linna.
"Ndio hivyo aisee akifika atafidia,halafu itabidi tumueleze kila kitu ajue na atulie wakati tunapanga tufanyaje,"Aliongea Dokta.
"Kabisa aisee inabidi awe anakaa ndani tu mpaka ajifungue,na kingine tumshauri afanye juu chini pesa za mmewe zote azihamishe maana yule hawara yake ni ana roho mbaya sana,"Aliongea Mchungaji Petro.
"Hilo umeongea itabidi tumueleze afanye hivyo?,"Walizidi kuongea mambo kadha wa kadha huku safari ikiendelea.





Huku nyumbani kwa Baba Linna msiba ulikuwa unaendelea na watu waliokuwepo asilimia kubwa walikuwa ni majirani na marafiki wa karibu.
Mziki pia wa kuwafariji ulikuwa unaendelea kama kawaida,licha ya kuendelea Joyce pekeake hakuufurahia kabisa ule mziki.Aliona kama msiba utachelewa kuisha ni kheri usingekuwepo ili watu waanze kuondoka na wale wanaofikiria kuja waache kabisa.
"Baby huu mziki mi siuhitaji naomba ukawambie wanaopiga wauzime ikiwezekana waondoke maana msiba umeisha mi naona wanatupigia kelele tu,"Joyce alimwambia Baba Linna.
"Mh! Lakini watu unawafariji si vibaya kuuzima nakuuondoa,unaonaje tuuache,"Aliongea Baba Linna kwa sauti ya upole.
"Baby mi unanipigia makelele bhana,unawambia wazime waondoke au huwambii,"Aliongea Joyce kwa ukali?.

Inaendelea



  NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4