MAMA WA KAMBO 7
Mama Linna aliingia chumbani akakuta chupi na sidiria zipo juu ya kitanda.
"Baba Linna ebu njo huku chumbani,"Alimuita mmewe.
Baba Linna kule sebuleni baada ya kuitwa na mkewe alimwambia Linna.
"Mwanangu leo nitachokufanya ndio utajua sikio huwa halizidi kichwa."
Linna baada ya kuambiwa hivyo alikaa kimya?.
Baba Linna aliondoka pale sebuleni nakwenda chumbani.
"Mme wangu nini hiki,yani unafanya mapenzi na dadako tena chumbani kwangu,"Mama Linna alimuuliza mmewe.
Baba Linna ndio kwanza akabaki anashangaa.
"Mme wangu nakuuliza wewe."
"Apa mchawi wangu ni Linna amna mwingine,"Baba Linna aliwaza moyoni huku akijiandaa kujibu swali toka kwa mkewe.
Baba Linna alivyomhisi mwanae ingawa hakuwa na uhakika akajiongeza akajibu hivi.
"Mke wangu usiwaze sana hizo nguo wifi yako amekupa ye zinambana."
"Mme wangu toka lini nikapewa nguo za ndani na mtu tena dadako,"Mama Linna aliuliza?.
"Mke wangu bhana si ndio leo umepewa wifi yako anakupenda sana ujue,"Baba Linna alijibu.
"Mh! Mme wangu dadako hana heshima hivi kweli anipe nguo za ndani inakuja kweli."
"Ila mke wangu bhana huyo kaishi sana ulaya kwa hio mambo yake niya kizungu."
"Hata kama ni kizungu mme wangu sio vizuri alivyofanya ameona mi sina hela au."
"Apana mke wangu basi yaishe nitamuonya tu asinanii tena."
"Ee mme wangu mwambie asirudie tena mrudishie chupi zake mi sitaki."
"Apana mke wangu tusirudishe ila nitamuonya tu yule ni mdogo wangu."
"Aya mme wangu nakupenda sana."
"Mi pia mke wangu nakupenda sana."
Hivyo ndivyo Mama Linna alivyotulizwa na mmewe.
"Mh! Mama una nini wewe unapuuzia vitu ninavyokwambia,nikwambieje ili uelewe mamangu,"Aliongea Lina moyoni baada ya kuona mamake kakubali kudanganywa na Babake.
"Saizi simwambii tena lolote,maana nikimwambia naambiwa mmbeya,"
Mle chumbani baada ya Mama Linna na mmewe kuelewana wakakumbatiana nakuanza kupigana mabusu,wakiwa wanaendelea na mabusu simu ya Mama Linna iliingia massage.Mama Linna alipofungua ujumbe uliotumwa ulisomeka(bosi mkaguzi amekuja njo mara moja)Ulitoka sehemu anayofanyia kazi.
"Samahani mme wangu naomba niende ofisini mara moja,"Mama Linna alimwambia mkewe.
"Sawa mke wangu nenda,"Aliongea Baba Linna.
Mama Linna alijiweka vizuri akatoka chumbani akakuta mwanae yupo mlangoni.
"We nini hapa,"Linna aliulizwa.
"Mama njaa inauma,"Linna alijibu kuwa njaa.
"Nyoo ebu toka hapa liongo wewe umesema Aunt alikuwa chumbani kumbe uongo tu,hivi mwanangu kwanini muongo hivyo?."
Linna alikaa kimya.
"Mwanangu sitaki uchonganishi tena uache,"Mama Linna aliongea kwa ukali.
Bado Linna alikaa kimya tu.
Mamake aliondoka pale mlangoni akaenda sebuleni akamkuta Aunt analia.
"Wifi usilie yule mtoto ni muongo sana,"Mama Linna alimwambia Aunt.
"Wifi inaniuma sana kuambiwa nilikua chumbani kwako,"Aunt au Joyce alilia nakuongea kinafki.
"Jamani wifi Linna ni muongo msamehe tu,"Mama Linna alimwambia Aunt.
"Wifi mwanao anatuchonganisha sana."
"Wifi nisamehe mimi msamehe Linna nitamuonya."
"Aya wifi muonye mwanao."
"Sawa nitamuonya basi usilie."
Aunt aliacha kulia akainuka nakwenda chumbani kwake.
Mama Linna alitoka nje aliwasha gari lake akaondoka.
Linna nae aliondoka pale mlangoni
nakwenda sebuleni.
Akiwa anaelekea sebuleni babake alimuita.
"Abee Baba,"Linna aliitika.
"Linna niambie ukweli nani kaweka nguo chumbani,"Linna aliulizwa.
Linna alikaa kimya?.
"Nauliza mara ya mwisho nani kaweka hizi nguo za ndani."
"Baba nisamehe ni mimi nimeweka,"Linna alijibu.
"Kwanini umeweka."
"Baba niliweka ili mama aone amfukuze Aunt mi simpendi."
"Kwanini humpendi Aunt."
"Baba huyu Aunt anavuruga familia simpendi."
"Mwanangu ulichofanya sijapenda umeskia."
"Ndio baba nimesikia ila umfukuze Aunt nitakuwa nawaheshimu."
"Kwanza kaa kimya saizi nakuonya mara ya mwisho,ukirudia umbeya nakupeleka shuleni sawa."
"Baba sirudii tena nisamehe Baba."
"Nimekusamehe nenda kakae sebuleni."
Linna alienda sebuleni na Babake aliingia chumbani kwa Aunt na huko alimkuta baby wake amekaa tu.
"Vipi baby."
"Safi tu vipi mkeo alikuitia nini."
"Linna alichukua nguo zako za ndani akaweka juu ya kitanda,ndio maana mamake aliniita ila nimemwambia ulimpa tu kama zawadi,"Baba Linna alimjibu Joyce.
"Jamani kwa hio kasemaje."
"Hajasema kitu ila tu hajapenda kupewa chupi na sidiria,"
"Mh! baby we noma ila Linna anaakili sana."
"We Linna noma,ebu tuache hayo nipe tamu kabla hajarudi."
"Sawa baby,"Aunt aliongea,walivuana nguo wakapanda kitandani wakaanza kuvunja amri ya sita.
Linna akiwa pale sebuleni ghafla mlango wa nje ulifunguliwa akaingia mamake akiwa anahema.
"Mama umesahau nini?,"Linna alimuuliza mamake.
"Funguo mwanangu,"Mama Linna alijibu.
"Mama!!!!!"Linna alimuita mamake.
"Mwanangu kuna umbeya gani tena maana wewe liongo sana,"Aliongea Mama Linna.
"Baba na Aunt wapo chumbani tena."
"Mwanangu ebu niache hivi kwanini muongo."
"Mama niukweli kama huamini nenda kachungulie uone,hata mlango hawajafunga."
"Mh! Kwa nikaangalie ukinidanganya nitakunyoosha."
"Mama we nenda kaone."
Mama Linna alienda ulipo mlango wa Aunt,ile anakaribia akasikia miguno ya Aunt ama wifi yake ikimaanisha jogoo la mmewe linamdonoa haswa.
Mama Linna bila kuchelewa alisukuma mlango,akaingia akakuta wapo kufanya mapenzi.
"Mme wangu unanisaliti haaa!!!"
Aunt na Baba Linna wakashtuka na mama Linna akaanguka chini puu!!.
Inaendelea
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment