Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MKANDALA AFUNGUKIA DILI LAKE LA KUWINDWA NA AZAM FC PAMOJA NA YANGA

MKANDALA AFUNGUKIA DILI LAKE LA KUWINDWA NA AZAM FC PAMOJA NA YANGA
CLEOPHANCE Mkandala, kiungo anayetimiza wajibu  wake ndani ya Tanzania Prisons iliyo chini ya Kocha Mkuu, Adolf Rishard amesema kuwa bado ana mkataba na mabosi wake hao kwa sasa.

Taarifa zimekuwa zikieleza kuwa kiungo huyo yupo kwenye hesabu za matajiri namba moja Bongo ambao ni
Klabu ya Azam FC pamoja na Mabingwa wa kihistoria Yanga.

Timu zote mbili zipo kwenye mpango wa kuboresha vikosi vyao ili kuwa bora msimu ujao kwenye michuano ambayo watashiriki.

Mkandala amesema:"Nimekuwa nikiskia taarifa zangu kuhitajika ndani ya timu za Azam na Yanga ila hakuna taarifa ambayo ni rasmi kwa sasa zote ni tetesi. "Bado nina mkataba ndani ya Prisons kwa sasa hivyo bado ninaitumikia Klabu yangu." Tanzania Prisons ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 41 baada ya kujikusanyia pointi 41 kibindoni.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4