Serikali ya Mtaa yawashukuru wasaidizi wa kisheria kwa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Wasaidizi wa kisheria hapa nchini wamepogezwa kwa kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na pia kuwasaidia kuweza kupata haki ya mirathi.
Hayo yamesemwa na Afisa Maendeleo ya Jamii Zena Kapama wakati akizungumzia umuhimu wa na kazi za wasaidizi wa kisheria pamoja na kazi zao za kuzaidia jamii na hasa kwenye kupata haki zao za kisheria.
‘Wasaidizi wa kisheria ni watu muhimu sana kwenye jamii yetu. Wanawezesha wananchi wetu kujua haki zao za kisheria na sana sana kwa wanawake ambao mara nyingi wakumbana na changamoto nyingi kwenye kunyimwa haki zao na zaidi kwenye urithi,’ Kapama alisema.
Wakati huo huo, Afisa Maendeleo huyo wa Jamii wa Wilaya ya Mbalizi Mkoani Mbeya alitoa pongezi kwa Msaidizi wa Kisheria wilaya humu Abel Kibona kwa kumsaidia mwanamke mjane Matrida Masoko kupata haki yake ya urithi baada ya kuwa amefiwa na mume wake.
Baada ya kupata taarifa kuwa Masoko amenyima kupata urithi baada ya kuwa mume wake amefariki, Kibona alimpa na ushauri pamoja na kufungua shauri kwenye Mahakama ya Mwanzo huku akiorodhesha mali ambazo aliweza kuchana na mume wake.
Baada ya shauri hilo kusizikilizwa mahakamani, Masoko aliweza kushinda baada ya Mahakama hiyo kudhihirisha kuwa Masoko ndio mtu halali wa kurithi mali ambazo ziliachwa na mume wake na hivyo kuamuru kuweza kumilikisha mali hizo ikiwemo shamba na nyumba.
Vile vile, Wasaidizi wa Kisheria Wilayani Mbalizi wamekuwa Nyuma ya mafanikio ya chama cha wanawake cha Huyandola ambacho Masoko ni mmoja wa kikundi hicho. Kikundi cha Huyandola kwa muda mrefu kimekuwa kikitengeza chokaa na kusambaza kwenye wilaya yote ya Mbalizi.
‘Sisi kwenye kikundi chetu tuko akinamama 25. Wasaidizi wa kisheria walitupa maoni ya kuchuka mkopo kutoka Manispaa ya Mbalizi ili kununulia mashine ya kutengeza choka pamoja na kununua mali ghafi ili kuweza kupanua biashara yetu, anasema Pili Jacob ambaye ndiye mwenyekiti wa kikundi hicho.
Pili anaongeza kuwa waliweza kufanikiwa kupata mkopo na kupanua biashara hiyo ya chokaa. ‘Baada ya kuwa mradi wetu wa kutengeneza chokaa umeenda vizuri, tuliweza kuanzishwa miradi mingine ambayo ni ufungaji wa kuku wa kisasa pamoja kutengeza sabuni. Miradi hiyo yote mpaka sasa hivi inaendea vizuri na kwa kweli imeweza kutuwezeshwa sana kwa hali zetu za kiuchumi’, Jacob anaongeza.
Kazi za wasaidizi wa kisheria zimekuwa na manufaa sana kwenye jamii na hasa kwa wanawake na watoto ambao hawana uelewa wa na elimu ya sharia. Huku wakiwa na udhamini kutoka shirika la Legal Services Facility (LSF), wasaidizi wa kisheria wameweza kuwafikia takribani wananchi 4.5 milioni kwa kutoa elimu ya kisheria huku wakitatua kesi mbali mbali takribani 75,000 kwa mwaka. Kazi kubwa ya Wasaidizi wa kisheria ni kutoa msaada ya kisheria pamoja elimu kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kugharamia kesi bila malipo na pia kuhahakisha kuwa wananchi wanao uelewa wa sharia za nchi.
Leave Comments
Post a Comment