STORY:PENZI GUMU EPISODE 01

Mpaka namaliza chuo nilikua nimeshajiandaa kwa ajili ya kuanza maisha mengine mpya ya mtaani na pia nlikua na mtaji wa kutosha kufungua biashara yangu ila bado nlikua sijafkria nifanye biashara gani huku bado nikiwa katika harakati za kutafta kazi. Nitafta chumba nikapanga nikanunua vitu vya ndani na kila kitu nilicho ona cha muhimu kwa wakati huo niliweka ndani..
Kazi haikua rahisi kupata hivyo nlipata wazo la kufungua duka la nguo za kike na viatu vya kiume. Na nikawa nakaa mwenyewe dukani huku naendelea na shughuli za kutafta kazi siku moja nikiwa pale dukani alinipigia simu rafiki angu mmoja "Haloo" nlisema baada ya kupokea simu.. "Nikaskia "Asia siku iz umenisusa sana yani" nikamwambia "Hamna mpenzi ila yani mambo yako tight sana na ukizingatia bado nahangaika hapa dukani yani peke angu napata tabu na nnachoka mno hata mda wa kupumzika sina" akasema "Hee kwaiyo vipi na mishe zako za kazi?" Nikamwambia "Bado mpenzi maana hapa siwezi kufunga" akasema "Kuna ndugu anatafta kazi ni kijana unaweza ukamuweka dukani wewe ukaendelea na mambo mengine" nikamwambia "Mgh vijana mimi nawaogopa nisije ibiwa hapa shoga angu" akasema "Ni ndugu yangu hana tabu bwana" nikasema "Kweli?" Akasema "Kweli" nikamwambia "Poa basi utaniunganisha nae tutaongea takwambia itakavo kuwa" akasema "Sawa"
Tukakata simu mimi nikaendelea na shughuli zangu za dukani jina langu naitwa Asia.. rafiki angu nlio kuwa naongea nae anaitwa meja.. Baadae Meja alinitumia namba za huyo kijana akasema niwasiliane nae..nikazisevu ili nimpigie badae nikitoka dukani..
Muda wa kufunga ulipo fika nilifunga na kuelekea nyumban nikapita kwenye ki hoteli nikala nikaenda nyumbani maana nlikua nimechoka sana wazo nlilo kua nalo kichwani ni kuoga na kulala tu.. Nilikua nimechoka sana.. Nilipofika nyumbani kweli nikaoga na kupanda kitandani kulala.. Sikukumbuka hata kumpigia huyo kijana..
Niliendelea na ratiba zangu yani sikuwa na kumbukumbu kama kuna mtu natakiwa kuongea nae. Nikiwa dukani nakuwa busy sana na wateja na nikitoka nakua nimechoka sana kwaiyo ni kupumzika tu.. hivyo ndo jinsi ratiba yangu ilivyo kuwa.. Baada ya wiki kadhaa kupita meja alinipigia tena na kuniuliza kama nimewasiliana na yule mtu hapo ndo nikakumbuka nikamwambia "Eeh yaan nlisahau kabisa hebu nitumie tena namba zake maana hata sikumbuki nilizisevuje" akanitumia na nikampigia wakati huo huo..
"Halooo" aliongea baada ya kupokea simu nikasema "Halo mambo" akasema "Poa" nikamwambia "Naitwa Asia nimepewa namba na meja kuhusiana na ishu ya kazi ya dukani" akasema "Anha sawa sister ndo mimi" nikamwelekeza duka lilipo ili aje tuzungumze.. akasema atakuja kesho..
Kesho yake alikuja na tukatambulishana na sikuwa na wasi wasi nae hivyo nilianza kumfundisha kazi taratibu kumwelekeza bei za nguo na viatu na kila kitu alicho takiwa kujua nilianza kumwelekeza..
Ila tatizo ni kwamba ana kaa mbali sana kwaiyo kwenda na kurudi kila siku haitawezekana akaomba akae kwangu mpaka mambo yake akiyaweka sawa ataenda kupanga.. Nikamwambia tampa jibu..
Jioni nikampigia meja "Vipi mama hapa tunafanyaje maana huyu anaishi mbali" akasema "Mmgh hapo sijui sasa labda umpe pesa akapange then utakua unamkata kwenye mshahara wake" nikamwambia "Hilo siwezi maana unajua gharama za kupanga kwanza hiyo hela naitoa wapi?" Akasema "Ye mwenyewe anasemaje?" Nikamwambia "Anh anasema eti akae kwangu mpaka mambo yake yakikaa sawa ndo akapange" meja akasema "Naona sio wazo baya" nikamwambia "Una maanisha nini sio wazo baya wakati mimi nimepanga chumba kimoja unadhani humo ndani tutaishije?" Akasema "Basi mlipie hela awe analala guest" nikamwambia "Hivi wewe umechanganyikiwa unajua gharama za guest huku au unaonge tuu" akasema "Asia wewe fanya maamuzi bhna chochote utakacho amua sawa wewe ndo boss" nikamwambia "Poa"
Nikamfata yule kaka alie jitambulisha kwa jina la zikomo.. Nikamwambia "Sasa naona hapa kuna mtihani maana mimi nimepanga chumba kimoja na hatutaweza kuishi pamoja kwaiyo kajipange kwanza ukishapata namna njoo tena" akasema "Mimi nitalala chini dada" nikamwambia "Hapana tutafte tu namna nyingine" akasema "Sawa"
Akaondoka na mimi nikaendelea na mambo mengine..
Zimepita kama wiki mbili nikapigiwa simu kuwa nimepata kazi katika taasisi moja ya serikali.. Na nna takiwa kuanza kazi nilifurahi kwa kupata kazi ila sasa hapo ndo linakuja wazo nikianza kazi atabaki nani? Na kama ni zikomo itakuaje? Itabidi niishi nae??...
Itaendelea...
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Leave Comments
Post a Comment