WASANII WA DANSI WAKIMBILIA MONDULI, KUJIUNGA NA WISDOM MUSIC BAND
MASUPASTAA kibao wa Bongo Dansi hivi sasa wamekimbilia jijini Arusha katika kitongoji cha Munduli walipoanzisha bendi ya Wisdom Music Band inayofanya vizuri hivi sasa.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam, bosi wa bendi hiyo, Nyuchi amesema kuwa, alishawishika kuanzisha kundi hilo baada ya wasanii wengi kumfuata kutaka msaada wake kisanii.
"Nimeanzisha kundi hilo ambalo linakusanya wanamuziki wengi mahiri, ili kusapoti jitihada za kuinua muziki wetu wa Dansi, hivyo naamini kundi hili litakuwa poa muda si muda," amesema Boss huyo.
Baadhi ya mastaa wanaopatikana kwenye bendi hiyo ni pamoja na Rama Igwe, Jua Kali, Awadh Muhumba, Sele Muhumba, Komba Bass, Cath Cindy, Elias Ngoma na Awadh Muhumba.
Previous article
Leave Comments
Post a Comment