Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

BUWASA YAENDELEZA UTEKELEZAJI WA KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI

BUWASA YAENDELEZA UTEKELEZAJI WA KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI
Na Abdullatif Yunus  Michuzi TV
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Bukoba - BUWASA wanaendelea kutekeleza kwa vitendo adhma ya Serikali ya Kumtua Mama ndoo kichwani, kwa kuendelea kusogeza huduma ya Maji safi karibu na Wananchi waishio Manispaa ya Bukoba, baada ya kuzindua Vilula viwili vya Maji katika mtaa wa Kisindi Kata Kashai.

Uzinduzi wa Vilula hivyo venye thamani ya shilingi Bilioni 2.4 ikiwa ni mwendelezo wa usambazaji wa mtandao wa Maji katika maeneo ya Kata Nne zilizosalia katika mradi mkubwa wa awali, maeneo hayo ni Kibeta, Kahororo, Nshambya, Hamugembe, Ijuganyondo, Nyanga, na  Kashai ambapo kukamilika kwa mradi huo unatarajia kuhudumia idadi ya Kaya 18,103 sawa na wakazi 90,517.

Akizindua Vilula hivyo Mkuu wa Wilaya Bukoba Mhe. Deodatus Kinawiro Amesema kuwa Serikali inatambua Tatizo lililokuwepo la upatikanaji wa huduma ya Maji kwa Manispaa ya Bukoba, na hivyo iliamua kuleta Bilioni 32 za mradi mkubwa wa kusambaza mtandao wa Maji ndani ya Manispaa, na kwamba maeneo yaliyokuwa yamesalia kutokana na mradi huo, tayari Serikali imeongeza fedha nyingine Bilioni 2.4 kuhakikisha huduma inawafikia Wananchi, na kuongeza kuwa Serikali itazidi kuongeza fedha kwa BUWASA ili kuhakikisha Wananchi wrote wanafikiwa na huduma ya Maji safi na salama.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi mtendaji wa BUWASA Ndg. John Sirati wakati wa uzinduzi huo, amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa na MBESSO Construction Co. Ltd na COSMOS Engineering Co. Ltd ulianza kutekelezwa mwaka 2017 na ulitakiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka 2018, lakini kutokana na changamoto mbalimbali mkandarasi aliongezewa muda hadi Desemba 2019 na hivyo kufikia sasa mkandarasi huyo anakamilisha baadhi ya mapungufu madogo madogo, na tayari nusu ya fedha zote kaishalipwa.
 Mkuu wa Wilaya Deodatus Kinawilo (mwenye miwani) akikata utepe pamoja na viongozi wengine kuashiria Uzinduzi wa Vilula viwili vya Majisafi katika mtaa wa Kisindi Manispaa ya Bukoba.
 Mkuu wa Wilaya Bukoba Deodatus Kinawilo akifungulia Maji kwenye kilula kimojawapo kati ya Viwili vilivyozinduliwa ikiwa ni ishara ya mwanzo wa upatikanaji wa Huduma ya Majisafi mtaa wa Kisindi Manispaa ya Bukoba.
 Pichani wanaonekana Wananchi wakazi wa Mtaa Kisindi wakifurahia huduma ya Maji Mara baada ya kuzinduliwa kwa Vilula viwili vya Maji.
Mkurugenzi Mtendaji wa BUWASA Ndg John Sirati akikabidhi Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Bilioni 2.4 kwa maeneo yaliyosalia Ndani ya Manispaa ya Bukoba.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4