COASTAL UNION YAANZA KUZOEA MAZINGIRA YA MWANZA, LEO KUKIWASHA
COASTAL Union iliyo chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda imeshaanza kuyazoea mazingira ya Mwanza baada ya kutia timu rasmi tangu jana.
Leo, Juni 23 itashuka Uwanja wa Kirumba kusaka pointi tatu mbele ya Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro.
Mgunda amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo na watapambana kusaka pointi tatu.
Mchezo wake uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ilikubali sare ya bila kufungana huku Mbao FC ikitoka kupokea kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Azam FC.
Leave Comments
Post a Comment