DC ATAKA MTUMISHI KERO KWA WAFANYABIASHARA AONDOLEWE TPA
Na shushu joel
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Zainabu Kawawa ameitaka mamlaka ya Bandari nchini(TPA) kumuondoa mtumishi ambaye amekuwa ni kero kwa wafanyabiashara katika wilaya hiyo.
Akizungumza na wafanyabiashara wa bandari ya Bagamoyo mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mfanyakazi huyo wa TPA amekuwa ni kero kubwa kwa wafanyakazi hao kutokana na manyanyaso makubwa anayowafanyia wafanyabiashara wa eneo hilo.
Aidha alisema kuwa awali serikali ya wilaya ilikuwa ikipambana na wimbi la vijana ambao walikimbia kwenye bandari hiyo na kukimbilia mtaani ambako walikuwa wakifanya mambo ya ovyo ingawa serikali iliwachukulia hatua kali za kinidhamu.
"Wafanyabiashara pitisha mizigo wamekuwa wakisumbuliwa na mtumishi huyo na hivyo kupelekea Wafanyabiashara hao kuhama hama hivyo mtu huyu hafai kuwepo kwenye wilaya ya Bagamoyo kwani ananyanyasa Wafanyabiashara wangu kwa kuwafanya wakimbilie kwenye msituni "Alisema Kawawa.
Pia Kawawa aliongeza kuwa amewaomba wafanyakazi hao kuendelea na shughuli zao za kila siku katika eneo hilo kwani mtumishi huyo ni lazima aondoke kutokana na kuwanyanyasa wafanyabiashara kwenye eneo hilo.
Aidha Kawawa amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na TAKUKULU kwenda kwenye bandari hiyo.
Alisema kuwa mambo yote haya yanayofanywa na TAKUKULU pamoja na huyo mtumishi kumekuwa na sintofahau na hivyo kuwataka kutoendelea na shughuli za kila siku.
Hehena ya Madumu ya Mafuta yaliyo kamatwa baada ya wafanyabiashara kukibilia polini kushusha mizigo yao, jana wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Zainabu Kawawa (wa mbele) akiwa katika Bandari ya Bagamoyo kukaguwa shehena ya mafuta yaliyo kamatwa baada ya wafanyabiashara kukimblia poli.(Picha na Emmanuel Massak wa Michuzi Tv).
Leave Comments
Post a Comment