Monday, 17 March

Ads Right Header

Buy template blogger

DC LUDEWA AKEMEA WATU WANAOHUSISHA MASUALA YA MAENDELEO NA SIASA

DC LUDEWA AKEMEA WATU WANAOHUSISHA MASUALA YA MAENDELEO NA SIASA
Na Shukrani Kawogo, Njombe

Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Andrea Tsere amekemea watu wanaohusisha masuala ya maendeleo na siasa na kusababisha wilaya hiyo kubaki nyuma kimaendeleo.

Hayo ameyasema wakati akipokea msaada wa mashine ya kutolea copy iliyotolewa na mdau wa maendeleo ambaye pia ni mzawa wa Ludewa Dk. Primus Nkwera.

Alisema kuwa watu wanafikiri kila maendeleo yatakayofanywa na mdau wanasema ni siasa badala ya kumpa sapoti ya mchango wake.

"Mimi namshukuru Dk. Nkwera kwa kutimiza ahadi yake ya mashine hii ambayo aliahidi na sitaki mtu aje anihoji kwanini nimepokea msaada huu kama Bali nategemea kujitokeza wadau wengine zaidi kuchangia maana idara ya elimu bado inahitaji printer, computer na vinginevyo", Alisema Tsere.

Akikabidhi mashine hiyo kwa niaba ya Dk. Nkwera, Nicksoni Mahundi amesema  Dk. Nkwera ametoa mashine hiyo ili kutimiza ahadi yake aliyoitoa katika mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika February 2 mwaka huu.

Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Sunday George amempongeza Dk. Nkwera kwa hatua hiyo na kuwaomba wadau wengine wazawa na wasio wazawa kusaidia kukuza maendeleo ya wilaya hiyo kwakuwa bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika elimu, maji na nyanja mbalimbali.

" Nikiwa kama mtendaji mkuu nitahakikisha mashine hii inatunzwa na kufanya kazi iliyokusudiwa kwa lengo la kuongeza ufaulu zaidi ambapo kwa sasa umekua kwa asilimia 83 kutoka asilimia 34", Alisema George.

Aliongeza kuwa idara ya elimu ni kubwa na bado inakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya utendaji.

Dk. Nkwera amekuwa mdau mzuri wa maendeleo ya wanaludewa hasa katika nyanja ya elimu ambapo ametoa fulsa kwa wanaludewa kusoma bure katika chuo chake cha St. Thomas kilochopo Songea na mpaka sasa wanaludewa wengi wameshanufaika na fulsa hiyo.
 Photocopy mashine aina ya Canon iliyotolewa na Dk. Primus Nkwera
 Baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe na wadau mbalimbali wakipokea mashine ya kutolea copy ( kutoka kulia ni mkurugrnzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday George, mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, muwakilishi wa Dk. Nkwera  Nickson Mahundi na  afisa elimu msingi Blantina Mlelwa
 Mkururugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Sunday George, Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, Afisa elimu msingi Blantina Mlelwa, muwakilishi wa Dk Nkwera Nickson Mahundi na wadau wengine wakiangalia mashine ya copy iliyotolewa na Dk. Primus Nkwera

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4