Ads Right Header

Buy template blogger

KANTE NA JORGINHO WAPO KWENYE MPANGO WA KUUZWA

KANTE NA JORGINHO WAPO KWENYE MPANGO WA KUUZWA

FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea inaelezwa kuwa yupo kwenye mpango wa kumuuza N'Golo Kante na Jorginho.

Inaelezwa kuwa mpango wa Chelsea ni kupata saini ya Hakim Ziyech wa Ajax na Timo Werner anayekipiga RB Leipzig hivyo wanataka mkwanja wa kuwalipa wachezaji hao.

Licha ya kueleza kuwa kuwauza wachezaji wote wawili kwa wakati mmoja ambao ni viungo ni hatari kwa Chelsea bado mabosi hao wanaamini haitakuwa tatizo kwao mahitaji yao makubwa ni kupata mkwanja.

Jorginho anaweza kuibukia ndani ya Juventus huku Kante akitajwa kuweza kuibukia ndani ya Klabu ya PSG.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4