Tuesday, 18 March

Ads Right Header

Buy template blogger

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUAPISHWA RAIS MPYA WA BURUNDI

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE KUAPISHWA RAIS MPYA WA BURUNDI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya kumuwaklilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye  leo Juni 18,2020. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais  Mpya wa  Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega Nchini Burundi  alipowasilisha salam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa Rais Ndayishimiye leo Juni 18,2020. kushoto ni Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete  wakiwa katika picha ya pamoja na  Rais  Mpya  wa Burundi Mhe.  Evariste Ndayishimiye Ikulu ndogo Gitega nchini Burundi leo Juni 18,2020.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa  na Rais mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye wakati Rais Ndayishimiye alipokuwa akipokea Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Burundi baada ya kuapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Igoma Stadium Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shughuli hiyo.
Makamu wa Rais wa Jarmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye mara baada ya Rais Ndayishimiye kuapishwa kuwa  Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Stadium Nchini Burundi Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais  Mpya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye  akikaguwa Gwaride baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Nchini Burundi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais  Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye  mara baada ya kuapishwa  kuwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Burundi leo Juni 18,2020 katika Uwanja wa Ingoma Nchini Burundi. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa Rais wa Burundi Mhe. Gasten Sindimwo alipowasili  kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura Nchini Burundi kwa ajili ya kumuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye shughuli ya kuapishwa Rais Mpya wa Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye  leo Juni 18,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4