MATUKIO MBALIMBALI MAPOKEZI YA NEW MV VICTORIA KATIKA BANDARI YA BUKOBA MKOANI KAGERA
Muonekano wa Meli iliyokarabatiwa kisasa ya New MV Victoria ikisogea eneo la Bandari ya Bukoba kabla ya kutia Nanga.
Chombo kikiwa tayari kimetia Nanga Bukoba kikingoja mizigo ya kwenda Mwanza Bila malipo ikiwa ni ofa ya majaribio kabla ya kuanza kwa safari zake za Mwanza Bukoba.
Viongozi na Wananchi wakiwa tayari kuupokea msafara uliowasili na Meli ya New MV Victoria ukiongozwa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Siasa wa CCM.
Pichani New MV Victoria ikitia Nanga katika Bandari ya Bukoba katika safari yake ya kwanza ya Majaribio Mara baada ya kusimama takribani miaka sita kwa marekebisho.
Sehemu ya Wakazi wa Bukoba na maeneo ya jirani wakishuhudia Meli yao ikitia Nanga bandarini
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa anaonekana kupongezana na aliyekuwa Mbunge Viti maalum Mkoa Kagera Bi. Oliva Semunguruka baada ya kuwasili kwa Meli ya MV Victoria
Shangwe la Vijana chipukizi kutoka Mwanza waliosafiri na Meli ya MV Victoria wakionekana kutia hamasa kwa nyimbo na vidokezo Mara baada ya kuwasili bandarini Bukoba
Ndege hakuwa mbali kupitwa na tukio la historia akionekana kutabasamu kazi nzuri iliyofanywa na Rais Magufuli.
Mgeni Rasmi Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Humphrey Polepole akiwasilisha ujumbe alioagizwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa wakati akitoa Salaamu zake.
Kakau Band wakitoa Burudani ya aina yake kuikaribisha Meli Iliyokarabatiwa ya New MV Victoria katika Bandari ya Bukoba.
Vijana wa Chipukizi kutoka UVCCM Manispaa ya Bukoba wakiingia kwa mtindo wa mchakamchaka
Hata kwa kukaa chini au Kusimama Wakazi wa Mkoa Kagera wakionekana kuisubiri kwa Hamu Meli yao walioikosa kwa muda mrefu
Kwa kutembea au kwa Baiskeli Wananchi wanazidi kuwasili Bandarini Bukoba kushuhudia tukio la Kihistoria la Safari ya Kwanza ya Majaribio ya Meli New MV Victoria
Mshereheshaji wa leo Afisa Michezo Manispaa ya Bukoba Ndg. Cletus akizidi Kusherehesha na kuweka utaratibu wa matukio ya leo
Previous article
Leave Comments
Post a Comment