MIJI YENYE WATU WENGI ZAIDI DUNIANI 2020, CHINA, INDIA WAONGOZA
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LICHA ya virusi vya Corona (Covid -19) kuathiri zaidi katika mataifa makubwa hasa kwa kusababisha maelfu ya vifo bado baadhi ya miji mikubwa duniani inashikilia takwimu za kuwa na wakazi wengi zaidi na hiyo ni kwa mujibu wa "population review" ya mwaka 2020.
Nchi za India na China bado zimeendelea kuwa vinara wa kuongoza kwa kuwa na watu wengi zaidi ulimwenguni huku nchi za Afrika zilizokuwa katika nafasi za juu ni pamoja na Nigeria, Ethiopia, Misri na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Katika miji mingi ya nchi za India na China idadi ya watu kuwa wengi haishangazi na hiyo ni kutokana na uwingi wa watu katika mataifa hayo mawili, nchini China mji wa Shanghai una watu wapatao milioni 25 na Beijing ina watu wapatao milioni 22 huku miji mikubwa nchini India ikiwemo Delhi ina watu wapatao milioni 27 huku Mumbai ikiwa na watu zaidi ya milioni 21.5.
Mji mkubwa duniani Tokyo, Japan una wakazi zaidi ya milioni 38 huku mji wa Osaka ukiwa na watu wapatao milioni 20.5.
Miji mingine iliyovunja rekodi ya kuwa na watu wengi zaidi ni pamoja na Mexico (watu milioni 19.5) na Buenis Aires nchini Argentina wenye watu milioni 15.5.
Pia katika miji mingi ambayo imekuwa ikipokea mamilioni ya watalii kila mwaka imeonekana kuwa na watu wengi zaidi na hiyo ni pamoja na instanbul, Uturuki yenye wakazi milioni 14.5 ikifuatiwa na Moscow Urusi yenye watu zaidi ya milioni 12 na Paris, Ufaransa ikiwa na watu milioni 11.
Vilevile miji maarufu na yenye utajiri imeonekana kuwa na watu wachache zaidi na hiyo ni kutokana na gharama za maisha katika miji hiyo ambayo ni Barcelona nchini Spain, Sydney nchini Australia na Berlin Ujerumani ambapo miji yote hiyo ina wakazi chini ya milioni 5.
Baadhi ya miji midogo maarufu ya kitamaduni na historia imeonekana kuwa na watu wachache na hiyo ni pamoja na Sarajevo (314,000) Edinburgh (502,000) na Venice (631,000.)
Kwa ufupi miji iliyovunja rekodi zaidi kwa mwaka 2020 ni Tokyo, Japan yenye watu milioni 37.28, Mumbai India watu milioni 25.97, Delhi India watu milioni 25.83, Dhaka Bangladesh milioni 22.81, Mexico City, Mexico watu milioni 21.81, Sao Paulo, Brazil watu milioni 28.81 na barani Afrika Lagos, Nigeria imekamata nafsi ya Saba kati ya miji 100 iliyoorodheshwa ikiwa na watu milioni 21.51 huku Tanzania kwa mji wa Dar es Salaam umekamata nafasi ya 68 ikiwa na watu milioni 5.2.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment