MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA ILALA APIGA JEKI SHULE YA SEKONDARI YA VINGUNGUTI
MSTAHIKI Meya Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto amefanya Ziara yake ya kikazi katika shule ya Sekondari Vingunguti, katika Ziara hiyo Mstahiki Meya aliambatana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Vingunguti pamoja na Wajumbe wa Mashina.
Lengo la ziara hiyo ni kukagua Ujenzi wa Madarasa Manne yanajengwa katika shule hiyo. Mstahiki aliwapongeza Walimu wa Shule hiyo ya Sekondari Vingunguti kwa usimamizi wa Ujenzi wa Madarasa hayo manne.
Uongozi wa Shule hiyo ulimpongeza Mstahiki Meya kwa utendaji kazi wake pia walimshukuru kwa kuleta mtambo wa maji baridi kwaajili ya wanafunzi kwani umepunguza kwa asilimia kubwa changamoto ya upatikanaji wa maji safi ya kunywa.
Mstahiki Meya alikabidhi Masinki 12 kwaajili ya Vyoo vya wanafunzi, Masinki hayo yatasaidia kupunguza UTI kwa watoto wakike kwani shule hiyo ilikuwa inatumia mashimo yakawaidia bila masinki.
Imetolewa na Ofisi ya Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala.
Leave Comments
Post a Comment