SHUGHULI ZA MAHAKAMA KUREJEA KAMA KAWAIDA, MAWAKILI KUPATA WASAA WA KUONGEA NA WATEJA WAO
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaeleza mawakili katika kesi ya kusafirisha kilo 268.50 za dawa za kulevya na utakatishaji wa zaidi ya Sh. Milioni 27 kuwa hivi karibuni shughuli za mahakama zitarudi kama kawaida na hivyo watakuwa wanapata wasaa wa kuongea na wateja wao.
Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi, amesema hayo leo Juni 29, 2020 wakati kesi hiyo inayomkabili Kigogo wa biashara ya dawa za kulevya raia wa Nigeria David Ochuku (38) mkazi wa Makasi na watanzania wawili Isso Lupembe (49) mkazi wa Mbezi Luis na Allistair Mbele (38) mkazi wa Mbezi Kibanda cha Mkaa ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Hivi karibuni mahakama zitarudi katika utaratibu wake wa kawaida na hivyo mtapata wasaa wa kuwa mnaongea na wateja wenu.
Mapema wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon alidai mahakamani hapo kuwa upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika hivyo ameomba tarehe nyingine ya kutwa.
Hata hivyo mawakili wa utetezi wakiongozwa na wakili Jeremiah Mtobesya alidai ni zaidi ya miezi miwili sasa haki ya upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa wotebqako gerezani tunaomba mahakama iwaeleze waharakishe upelelezi kwani haki inayocheleweshwa na haki inayonyimwa.
Aidha mawakili hao waliomba wapatiwe nafasi ya kuongea na wateja wao kwani tokea walipokamatwa hajawahi kuongea nao.
Akijibu hoja kuhusu upelelezi Wankyo amesema, kiasi cha dawa kinachodaiwa kisafirishwa ni kingi na upelelezi unahusisha ndani na nje ya nchi hivyo hauwezi kukamilika kwa haraka ila muda utakapofika wataeleza juu ya hali ya upelelezi.
Awali ilidaiwa kuwa Aprili 15, mwaka huu maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa eneo ambalo lipo katika wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao kwa pamoja walikutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin zenye uzito wa Kilogramu 286.50.
Pia inadaiwa, kati ya Januari Mosi, 2016 na Aprili 15,2020 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam washitakiwa hao walijihusisha na miamala ya fedha kiasi cha Dola za Marekani 61,500 na Shilingi za kitanzania 17,835,000, huku wakifahamu kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la usafirishaji wa dawa za kulevya.
Washtakiwa wote wamerudishwa rumande.
Leave Comments
Post a Comment