Thursday, 20 March

Ads Right Header

Buy template blogger

SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MBEYA CITY

SIMBA YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MBEYA CITY

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa watakuwa na kazi ngumu mbele ya Mbeya City, Juni 24 ila watapambana kupata matokeo.

Leo Simba imewasili Mbeya kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni.

Bocco amesema:"Wachezaji tupo tayari na tunatambua kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji kupata pointi tatu.

"Tunawaomba mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kwani malengo yetu ni kuona tunapata pointi tatu," amesema.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4