TCRA yawashukia wasafirishaji wa vifurushi wasio na leseni Ubungo jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mhandisi Lawi Odiero akizungumza kuhusiana na operesheni ya wasafirishaji vifurushi Katika Kituo cha Mabasi Ubungo jijini Dar essalaam.
Mfanyakazi wa Kampuni ya kusafirisha vifurushi kwa njia basi Ya M Cargo akiwa ameshikiliwa na Polisi katika Operesheni yaTCRA ya kuwasaka wasafirishaji wa vifurushi wa sio na leseni katika kituo Cha mabasi Ubungo.
Msafirishaji wa vifurushi wa kampuni ya Suti Africa Gisela Paulo akitoa maelezo ya kuwa hausiki na usafirishaji huo wakati alijaza fomu ya usafrishaji.
Emmanuel Cornel akitoa maelezo namna ya changamoto iliyomkuta wakati aliosafirisha kifurushi ambapo Hadi tarehe 29 mwezi huu mlengwa hajifikiwa na huduma hiyo.
Baadhi ya vifurushi vinavyosafirishwa na kampuni ya M Cargo Transport.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki imefanya operesheni kwa kampuni yanayosafirisha vifurushi bila kuwa na leseni kutoka katika mamlaka hiyo hali ambayo inaleta usumbufu kwa wananchi pale wanapokuwa wametuma vifurushi hivyo.
Akizungumza na waandishi habari wakati wa operesheni hiyo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Lawi Odiero amesema operesheni hiyo ni endelevu kwa kampuni zinazosafirisha vifurushi bila ya kuwa na leseni hali ambayo inasababisha serikali kukosa mapato.
Amesema kuwa operesheni hiyo wanaifanya kwa kushirikiana na jeshi la polisi ambapo baada ya kuwakamata wasafirshaji hao wanafunguliwa mashitaka ya kufanya biashara ya usafirishaji vifurushi kwa njia ya basi bila kuwa na leseni
"Hii ni operesheni endelevu kwa wasarishaji vifurushi bila kuwa na leseni nia ni kutaka wafanyabiashara ya usharishsji wa vifurushi wafuate matakwa ya sheria kwani kazi hiyo wanaiokosesha serikali mapato"amesema Odiero.
Aidha amesema kuwa utaratibu wanaohitaji leseni upo wazi hivyo kwa wale wanaohitaji wafuate sheria na kama wataendelee kutoa huduma hiyo bila kuwa leseni sheria itashika mkondo wake.
Kampuni zilizokuwa zikifanya biashara ya kusafirisha vifurishi bila ya kuwa na Leseni ni M CargoTransport, pamoja na Suti Afrika katika kituo cha mabasi ubungo.
Aliyekamatwa wa Kampuni Suti Afrika Gisela Paulo amesema kuwa yeye sio wa kampuni hiyo alichokifanya ni kujaza fomu ya kusafirishia mzigo kwani kampuni hiyo wako katika ofisi moja hakujua kama hawana leseni.
Mmoja ya wananchi aliyepata huduma M Cargo Transport Emmanuel Cornel amesema kuwa alipata huduma ya kusafirsha kifurishi lakini hadi leo hakijafika huku hakuna majibu sahihi ya nani alipokea fedha kwa ajili ya usafirshaji wa kifurushi.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment