Ugonjwa wa Ebola waripotiwa tena kaskazini magharibi mwa Congo DR
Maafisa wa afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza kuwa, maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yamerejea tena nchini humo.
Wizara ya Afya ya Congo DR imeongeza kuwa Taasisi ya Taifa ya Uhakiki wa Biomedical (INRB) imethibitisha kuwa, watu kadhaa waliofanyiwa vipimo katika mji wa Mbandaka wamepatikana na homa ya virusi vya Ebola.
Miezi miwili iliyopita Mkurugernzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alitahadharisha kuhusu uwezekano wa mlipuko wa virusi vya homa ya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wimbi la maambukizi ya homa ya virusi vya Ebola lilianza tarehe 8 mei mwaka 2018 katika mji wa Bikoro mkoa wa Équateur uliko kaskazini magharibi mwa Congo DR na baadaye ikasambaa kwa kasi katika mji wa Mbandaka ambao ni makao makuu ya mkoa huo na mashariki mwa nchi hiyo.
Virusi hivyo vimesababisha vifo vya watu wasiopungua 2,200.
Maambukizi mapya ya virusi vya Ebola yameripotiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo sambamba na janga la sasa la virusi vya corona ambavyo vimekwishasababisha vifo vya makumi ya watu nchini humo.
NAFASI MPYA ZA KAZI KWA WENYE ELIMU KUANZIA DARASA LA SABA ,KIDATO CHA NNE,CERTIFICATE,DIPLOMA,DEGREE NA KUENDELEA ZIPATE KUPITIA AJIRA FORUM APP 👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment