Wednesday, 19 March

Ads Right Header

Buy template blogger

UKUSANYAJI MAPATO SEKTA YA MADINI WAMKOSHA WAZIRI DOTTO BITEKO, AIMWAGIA SIFA GGML KWA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI KATIKA MKOA WA GEITA

UKUSANYAJI MAPATO SEKTA YA MADINI WAMKOSHA WAZIRI DOTTO BITEKO, AIMWAGIA SIFA GGML KWA UWEKEZAJI WA KIMKAKATI KATIKA MKOA WA GEITA
 Makamu wa Rais anayeshughulikia Maendeleo Endelevu katika Kampuni ya GGML, Simon Shayo akizungumza katika ziara ya Waziri wa Madini, Dotto Biteko aliyetembelea miradi ya kampuni hiyo inayotekelezwa chini ya mpango wa kusaidia jamii (CSR) mkoani Geita.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akitoa pongezi za serikali kwa GGML baada ya kutembelea miradi hiyo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel  na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Josephat Maganga wakati kushoto ni baadhi ya maofisa wa mji wa Geita.
Waziri wa Madini Dotto Biteko akielekea kukagua soko kuu la Geita huku akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Josephat Maganga (kulia) pamoja na maofisa wengine wa mji wa Geita.

========   =======  =======  =========

UKUSANYAJI MAPATO SEKTA YA MADINI WAMKOSHA WAZIRI DOTTO BITEKO, AIMWAGIA SIFA GGML KWA UWEKEZAJI WA  KIMKAKATI KATIKA MKOA WA GEITA

Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko ameipongeza Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya dhahabu - Geita (GGML) kwa kuwa mdau wa mfano katika kuchangia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Geita huku akielezea kufurahishwa kwake na Serikali ya Mkoa wa Geita inavyosimamia ukusanyaji mapato katika sekta ya madini.

Biteko ametoa kauli hiyo katika ziara fupi aliyoifanya mkoani Geita na kukagua miradi inayotekelezwa na Kampuni ya GGML chini ya mpango wake wa kusaidia jamii (Corporate Social Responsibility) katika Mji wa Geita.

Aidha, amesema lengo la Serikali ni kuona maisha ya watu katika maeneo yote yenye rasilimali madini, ikiwemo Geita yanabadilika kiuchumi na kwamba anafurahishwa na namna ambavyo Serikali ya Mkoa wa Geita inavyosimamia ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye sekta ya madini.
"Tayari tumeshafikia lengo la kukusanya zaidi ya Sh bilioni 400 kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 2020 kutoka kwenye sekta hii, na sehemu kubwa ya makusanyo haya imetoka Geita, hususan GGML. Inatia moyo sana kuona sekta hii sasa inachangia zaidi ya asilimia 5 ya uchumi wa nchi yetu. Lengo ni kuhakikisha kwamba sekta ya madini inachangia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025,"amesema Waziri  Biteko.

Mojawapo ya miradi ambayo ilikaguliwa na Biteko katika ziara yake hiyo ni ujenzi wa Kanda maalumu ya uwekezaji "Special Economic Investment Zone" ambao utasimamiwa na Mamlaka ya ukanda maalumu wa Uwekezaji (EPZA) na Halmashauri ya Mji wa Geita.Pia ametembelea miradi mingine ya kimkakati inayofadhiliwa na GGML, ikiwemo ujenzi wa Soko Kuu la Geita Mjini na soko la Katundu.

Kwa upande wake Makamu wa Rais anayeshughulikia Maendeleo Endelevu katika Kampuni ya GGML Simon Shayo amesema utekelezaji wa miradi ambayo imetembelewa na Waziri Biteko ni sehemu ya mpango wa mwaka 2018/19 unaoenda sambamba na mojawapo ya tunu za kampuni hiyo inayoelekeza kwamba jamii inayozunguka shughuli zake sharti ifaidike kwa uwepo wake.

Ameongeza kuwa GGML ambayo ni sawa na kampuni-raia inawajibika ipasavyo kwa jamii kwani hutumia Sh bilioni 9.2 kila mwaka kugharimia miradi ya jamii mkoani Geita na kuifanya kampuni hiyo kuwa ya kipekee kutokana na mchango mkubwa inayotoa kusaidia jamii.

"Kama Kampuni-raia ndani ya Tanzania, GGML iliyoko chini ya AngloGold Ashanti itaendelea kuunga mkono na kusaidia jamii zinazotuzunguka. Utekelezaji wa miradi ya CSR na shughuli zingine kama hizo.

"Ni ushahidi wa wazi kwamba kampuni, serikali na jamii zikifanya kazi pamoja zinaweza kuboresha maisha ya watu kupitia uwekezaji endelevu katika miundomuni ya biashara na huduma.Tunataka kuona maisha ya mtu wa kawaida katika jamii yetu yakiwa bora zaidi kupitia uwekezaji endelevu wa Kampuni yetu,"amesema.

Aidha katika kipindi cha mwaka 2018, GGML iliwezesha utekelezwaji wa miradi kadhaa kupitia mpango wake wa kuwekeza katika jamii.

"Miradi hii inajumuisha; uwekaji wa taa za barabarani katika mji wa Geita, ujenzi wa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, ujenzi wa soko la kisasa Geita mjini, umaliziaji wa majengo zaidi ya 600 ya afya na elimu na ujenzi kamili wa shule tatu mpya na vituo vya afya vinne. Pia GGML imetenga Sh. bilioni 18 kwa ajili ya miradi mingine kama hiyo katika kipindi cha kati ya mwaka 2019/20 na 2020/21.

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4