WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID MOHAMED ATEMBELEA KAMBI ILIOKUWA YA WAGONJWA WA CORONA ZANZIBAR.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed akizungumza na Maofisa wa Jeshi la kujenga uchumi mara baada ya kuwatembelea kwa lengo la kukagua kambi iliyokua ikitumika kwa kulaza wagonjwa wa Corona,hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa skuli ya JKU iliyopo Mtoni Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohammed (kulia)akisisitiza jambo wakati akiwa katika moja ya chumba kilichokua kikitumika kutoa huduma kwa wagonjwa wa Corona Skuli ya JKU Mtoni Zanzibar.
Waziri wa Afya Hamad Rshid Mohamed akipata maelezo kutoka kwa maofisa wa jeshi la kujenga uchumi Zanzibar [JKU] wakati akikagua maeneo mbalimbali yaliyokua yakitumika kwa ajili ya wagonjwa wa Corona.
Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohammed akikagua kituo cha Afya cha Selemu Mfenesini ikiwa ni miongoni mwa vituo vilivyoteuliwaa kutoa huduma za mwanzo kwa wagonjwa wenye dalili za Corona endapo wakitokezea .
Waziri wa Afya wa Zanzibar Hamad Rashid Mohammed akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa afya mara baada ya kukagua kituo cha afya cha Fujoni ambacho ni miongoni mwa vituo vilivyoteuliwa kutoa huduma za mwanzo kwa wagonjwa wenye dalili za Corona endapo wakitokezea .PICHA NA-FAUZIA MUSSA/MAELEZO ZANZIBAR.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment