Ads Right Header

Buy template blogger

WAZIRI WA MAJI PROFESA MBARAWA AREJESHA FOMU YA KUWANIA URAIS ZANZIBAR, ASHUKURU CHAMA CHAKE

WAZIRI WA MAJI PROFESA MBARAWA AREJESHA FOMU YA KUWANIA URAIS ZANZIBAR, ASHUKURU CHAMA CHAKE
WAZIRI wa Maji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa amerejesha fomu ya kuwania uteuzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wake wa urais Zanzibar.

Profesa Mbarawa alichukua fomu Juni 19,  mwaka huu katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Unguja, akiwa mwanachama wa 10 kufanya hivyo.

Hivyi leo Juni 27,2020  amerejesha fomu hizo katika ofisi hiyo na kupokewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Zanzibar, Galous Nyimbo.

Wakati alipochukua fomu hiyo Profesa Mbarawa aliwaambia waandishi wa habari kuwa amemtanguliza Mwenyezi Mungu katika safari hiyo na kuwataka wamuombe jambo alilolianzisha likawe na baraka kwake.

Hata hivyo baada ya kurejesha fomu leo amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kusimamia vizuri mchakato huo wa kuwania uteuzi wa kugombea urais wa Zanzibar.

Mbali ya kuwa Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa amewahi kuhudumu katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika Serikali ya Rais John Magufuli.




Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4