Ads Right Header

Buy template blogger

CHAMA CHA UPINZANI CHA UDP kumnadi Mgombea Urais wa CCM Rais Dkt.John Magufuli Uchaguzi Mkuu.

CHAMA CHA UPINZANI CHA UDP kumnadi Mgombea Urais wa CCM Rais Dkt.John Magufuli Uchaguzi Mkuu.
*Dirisha la Uchukuaji fomu kwa Wabunge na Madiwani laanza Julai 4.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

CHAMA cha United Democratic Party, (UDP) kimesema kitanuunga mkono Rais John Magufuli endapo Chama chake kikimpitisha kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Kimesema Chama hicho kimefungua dirisha la wagombea Ubunge na Udiwani kuanza kuchukua  fomu katika Ofisi zao.

Mwenyekiti wa Chama hicho,John Cheyo (Mapesa) amesema kipaumbele cha Rais Magufuli kuwainua wanyonge na kuleta maendeleo nchini ndio sababu iliyowafanya kuwaunga mkono.

"Namsifu Magufuli kuweka Mazingira mazuri hospitali karibu na wananchi,kutuimarishia miundombinu ya Barabara na Reli," amesema na kuongeza kuwa

"Tumeamua kumuunga mkono Rais Magufuli endapo atapitishwa na Chama chake ila kama wasipompitisha tutatathimini kwanza ni nani tumpitishe alafu tutakuja na majibu kwa wananchi," amesema

Pia amesema wamefungua dirisha la uchukuaji wa fomu leo na siku ya mwisho wa uchukuaji wa fomu hizo watatangaza kuendana na ratiba ya Tume ya Uchaguzi (NEC).

"Natoa Rai kwa wanachama wa UDP, kuja kuchukua fomu ili kuweza kupata nafasi ya  kuingia katika baraza la maamuzi," amesema


Mwenyekiti wa Taifa wa Chama United Democratic Party John Cheyo akizungumza kuhusiana na uchaguzi mkuu na hatima ya chama hicho kuunga mkono mgombea urais wa CCM.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4