Ads Right Header

Buy template blogger

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHASHIRIKI MAONESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA JIJINI DAR

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHASHIRIKI MAONESHO YA 44 YA KIMATAIFA YA BIASHARA JIJINI DAR

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Bi. Sarah Goroi(kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Jeshi la Anga Meja Jenerali George William Ingram(kushoto), kuhusu kozi mpya zinazotarajiwa kuanza kufundishwa na chuo hicho mwezi Oktoba, 2020 wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara  jijini Dar es Salaam.

Afisa Udahili wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sekunda Titus(kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu usajili kwa njia ya mtandao na kozi mpya zinazotarajiwa kuanza kufundishwa na chuo hicho mwezi Oktoba, 2020  kwa mwananchi aliyetembelea katika banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Afisa Udahili wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Sekunda Titus(kulia) akitoa ufafanuzi wa kozi zilizopo na kozi mpya zinazotarajiwa kuanza kufundishwa na chuo hicho mwezi Oktoba, 2020  katika chuo hicho kwa mwananchi aliyetembelea katika banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Chuo cha Uhasibu Arusha Bi. Sarah Goroi, akitoa  maelezo kwa wananchi kuhusu kozi mpya zinazotarajiwa kuanza kufundishwa na chuo hicho mwezi Oktoba, 2020 waliotembelea katika banda hilo katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar es Salaam.

Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4