Ads Right Header

Buy template blogger

HUKO ENGLAND NAKO VITA YA KUSHUKA DARAJA NI MBICHI, ASTON VILLA KAZI IPO

HUKO ENGLAND NAKO VITA YA KUSHUKA DARAJA NI MBICHI, ASTON VILLA KAZI IPO
ASTON Villa inayoshiriki Ligi Kuu England ni miongoni mwa timu tatu ambazo leo zinapambana kujinasua kushuka daraja.

Timu nyingine ambazo zinaungana na Villa anakokipiga
nyota wa Tanzania, Mbwana Samatta ni pamoja na Watford na Bournemouth ambazo hazina uhakika wa kubaki ndani ya Ligi hiyo pendwa mpaka watakapokamilisha dakika 90.

Leo Jumapili, Julai 26 msimu wa Premier unafika tamati huku ule mpya wa 2020/21 ukitarajiwa kuanza Septemba 12.

Aston Villa ina pointi 34 ikiwa nafasi ya 17 itakuwa ugenini kucheza na West Ham United ambao hawana cha kupoteza na inatakiwa kushinda ama kuwaombea njaa wengine ambao ni Watford na Bournemouth wapoteze mechi zao.

Watford ipo nafasi ya 18 ikiwa na pointi 34 wametofautiana bao moja tu na Villa itamenyana na Arsenal huku Bournemouth ikiwa nafasi ya 19 na pointi 31 ina kazi mbele ya Everton na ina kazi ya kushinda kwa mabao mengi ili kuzipoteza zile zilizo juu yake.

Mechi zote leo zinatarajiwa kupigwa kuanzia majira ya saa 12:00 jioni.
Previous article
Next article

Leave Comments

Post a Comment

Ads Post 4