Joycer- Wanawake tugombee nafasi za uongozi
Joycer- Wanawake tugombee nafasi za uongozi
Na Woinde Shizza, Kilimanjaro
MWANAHARAKATI wa haki za wanawake hapa nchini, Joyce Kiria the Super woman kutoka Shirika la haki za wanawake Tanzania amewataka wanawake wote nchini kuendelea kusimamia imara katika kugombea nafasi mbali mbali za uwongozi mwaka huu wa 2020.
Akizungumza na vyombo vya Habari mwanaharakati huyo alisema kuwa kwa muda wa miaka mitano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kumekua na mwamko mkubwa kwa wanawake kufanya kazi kwa bidii katika nafasi walizo pewa bila kuwepo na utumbuaji
Kiria alisema kwamba wanawake wa kaskazini wajitokeze kufanya mabadiliko katika kugombea nafasi mbali mbali kuanzia ngazi ya udiwani ubunge kwa lengo la kushika nafasi na kusaidiana na Makamu wa Rais katika kupambani haki na uwajibikaji wa mwanamke.
"Namshukuru, Rais kwa kututhamini na kutupa nafasi katika uongozi wake kutupa nafasi akiwemo mama Samia Suluhu, ummy mwalimu, mama Joyce Ndarichako pamoja na wanawake wengi walioko katika wizara mbali mbali wanafanya vyema sana kusimamia haki za wanawake na maendeleo ya wa Tanzania kwa ujumla." Alisema Joyce
Mwaka huu wanawake tumeona maboresho ya vituo vya Afya pamoja zahanati na kupungua matukio makubwa ya akinaMama kujifungulia njiani na kupata huduma za kitabibu kuanzia kata mpaka hospitali za rufaa jambo ambalo limesaidia kupungua vifo vya Mama na mtoto .
Amefafanua kwamba licha ya serikali ya awamu ya tano kutoa kipaumbele kwa wanawake kushika nafasi za kuu serikalini pia wanawake kwa sasa wanajitambua na kujituma katika kujiendeleza kielimu na kutatua changamoto za kifamilia.
Joyce Kiria licha ya kuwa mwanaharakati za haki za binadamu amekuwa mwanamke mwenye uthubutu wa kufatilia matatizo ya wanawake na kuyaibua katika jamii na kujizolea umaharufu makubwa na kuaminika na baadhi ya wanawake wamekua wakiomba kuona siku moja anakua katika wizara ya Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto.
Ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi kwani amekua mfano mkubwa wa kuigwa katika kuwasaidia wanawake kujitambua na kupambana kupata haki zao pale ambapo wanadhulumiwa na hata kushinda kupata nafasi za uwajibikaji mpaka watoe rushwa ya ngono kwa waajiri wao.
Mwanaharakati wa haki za wanawake hapa nchini, Joyce Kiria the Super woman kutoka Shirika la haki za wanawake Tanzania akizungumza na waandishi wa habari.
Previous article
Next article

Leave Comments
Post a Comment