KASI YA MANCHESTER UNITED INAFURAHISHA
LICHA ya Junior Stanisiasi nyota wa Bournemouth kufunga bao la kuongoza dakika ya 16 halikuwazuia Manchester United kuvuna pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Trafford, jana.
United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer ilianza kushusha mvua ya mabao kupitia kwa Mason Greenwood kinda mwenye miaka 18 aliyefunga mabao mawili dakika ya 29 na 54 huku Marcus Rashford akifunga dakika ya 35 kwa penalti, Anthony Martial dakika ya 45 na Bruno Fernandes dakika ya 59.
Bao la pili kwa Bournemouth iliyokubali kichapo cha mabao 5-2, ikiwa nafasi ya 19 na pointi 27, lilipachikwa na Joshua King dakika ya 49 kwa mkwaju wa penalti.
Ushindi huo unaifanya Manchester United kuwa nafasi ya 5 na pointi zake 55 zote zikiwa zimecheza mechi 33 ndani ya Ligi Kuu England.
Solskjaer amesema kuwa anafurahi kuona vijana wake wanafanya kazi kwa juhudi kutafuta matokeo ndani ya uwanja.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment