Katibu mkuu wizara ya kilimo ageuka mbogo ukamilishwaji maghala ya nafaka Makambako
Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya amemuagiza meneja wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula mkoa wa Njombe na Iringa NFRA pamoja na mhandisi mkazi wa TBA kumsimamia mkandarasi anaye jenga maghala mawili ya kuhifadhi chakula mjini Makambako na kutaka maghala hayo kukabidhiwa mapema mwezi Disemba mwaka huu.
Kusaya amechukua uamuazi huo baada ya mkandarasi anaye jenga maghala hayo kusuasua kukamilisha ujenzi ambao mpaka sasa ulitakiwa uwe umekamilika na kuanza kuhifadhi nafaka mbalimbali jambo ambalo limekuwa kinyume na makubaliano ya mkataba.
“Chukueni hatua TBA tunachotaka ikifika disemba 31 mimi nije hapa tarehe moja mwaka 2021 mnikabidhi majengo yangu hicho ndicho tunachotaka”alisema Kusaya
Awali kaimu meneja wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula mkoa wa Njombe na Iringa NFRA Frank Felix amesema mpaka sasa kanda hiyo yenye mikoa miwili ina uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 22 na kuongeza kuwa ukasanyaji nafaka utaongezeka mara baada ya maghala mawili yanayo suasua kujengwa yakikamilika.
“Tumepangiwa jumla ya kununua tani elfu 30,ndani ya tani hizo tani elfu tano tutanunua mpunga na elfu 25 tutanunua mahindi,lakini maghala haya mawili yatakuwa na uwezo wa kuchukuwa tani elfu kumi kumi kwa hiyo jumla sasa ya mradi huu ni tani elfu 40”alisema Frank Felix
Akizungumzia changamoto za mradi wa ujenzi wa maghala mawili ya kuhifadhi nafaka mhandisi mkazi wa TBA Eng.Pedon Mushobozi anasema uzembae wa mkandarasi,hali ya hewa pamoja na kusuasua kwa malipo,yamepelekea kuchelewa kukamilika kwa ujenzi huo.
“Changamoto kubwa hapa ni malipo kwa mkandarasi na imepelekea mkandarasi kuishiwa fedha”alisema Eng.Pedon Mushobozi
Katika hatua nyingine katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya amewataka wafanya kazi wote wanao fanya kazi chini ya wizara yake kujiendeleza kielimu kwani kufanya hivyo kunaongeza ufanisi kazini.
Katibu mkuu wizara ya kilimo Gerald Kusaya akikaua maghala pamoja na kuzungumza na watumishi katika wizara hiyo mara baada ya kufika eneo la ujenzi wa maghala hayo kanda ya Makambako.
Maghala yanayojengwa katika kanda hiyo ya Makambako mkoani Njombe.
Baadhi ya nafaka zilizohifadhiwa katika maghala hayo ya kanda ya Makambako.
Kaimu meneja wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula mkoa wa Njombe na Iringa NFRA Frank Felix akitoa taarifa ya ujenzi wa maghala
Eng.Pedon Mushobozi akitoa taarifa ya ujenzi mbele ya katibu mkuu wizara ya kilimo.
Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment