NAMUNGO KUKIWASHA KESHO DHIDI YA JKT TANZANIA, TAMBO ZATAWALA

NAMUNGO FC iliyo chini Kocha Mkuu, Hitimana Thiery, kesho, Julai 4 itakuwa na kibarua cha kumenyana na JKT Tanzania inayonolewa na Abdallah Mohamed, 'Bares' Uwanja wa Majaliwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
JKT Tanzania ipo nafasi ya saba ikiwa na pointi zake 47 inamenyana na Namungo iliyo nafasi ya nne na pointi zake 56.
Timu zote mbili zimecheza jumla ya mechi 32 za Ligi Kuu Bara.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu na ninajua kwamba utakuwa mchezo mgumu, kikubwa ambacho tutakifanya ni kutafuta matokeo chanya ili kubaki na pointi tatu muhimu," amesema.
Ofisa Habari wa JKT Tanzania, Jamila Mutabazi amesema kuwa wachezaji wana morali kubwa na wana nia ya kutafuta ushindi.

Previous article
Next article
Leave Comments
Post a Comment